Kushawishiwa kwa Jaji Ramadhani. Je, ni uthibitisho kwamba CCM imeoza na imeshindwa?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..tunaambiwa kwamba huyu bwana amebembelezwa ili agombee.

..taasisi yoyote inapoamua kutafuta mtu wa kuiongoza nje ya taasisi hiyo, basi uwezekano mkubwa ni kwamba walioko mle ndani wamekosa sifa za kuipeleka mbele taasisi hiyo.

..sasa ni nini kimeisukuma CCM kutafuta mgombea nje ya makada wake ambao wako-active?

..Je, ni kukiri kwamba makada na watendaji wa CCM kwenye chama na serikali wamechoka na hawana uwezo?

..kwanini wananchi wachague chama hiki, wakati wenye chama wenyewe wanakiri kwamba wameshindwa kiasi kwamba wamelazimika kwenda "nje ya chama" kutafuta mgombea?

..Je, Jaji Ramadhani atatimu makada wote wa ngazi za juu, kati, na chini, ili kusimika mfumo mpya utakaoendana na matakwa ya wananchi? Uwezo huo anao?

cc Rev. Kishoka, Kapwela, Mkandara, Ritz, Kobello, Kiranga, Nyani Ngabu, Mzee Mwanakijiji, Ngongo, zumbemkuu, ZeMarcopolo, VUTA-NKUVUTE, Mag3, Pasco, Nguruvi3
 
JokaKuu hapa ndio tutakapoona umakini wa Tanzania katika uchaguzi ulioyaeleza ni kweli kwa watu wenye maono hilo pekee lingekipumzusha ccm.
 
Last edited by a moderator:
Mmmh, naona dodoma kitanuka, kiukweli hata aletwe masihi Yesu au mtume muhamad, au malkia au nabii yeyote wa dini yeyote kuombwa kugombea kupitia CCM atakuwa ameombwa na mfumo wa kifisadi kulinda ufisadi wao, hakika na yeye atakuwa fisadi, huwezi kulinda mfumo wa kifisadi bila wewe kuwa fisadi
 
..tunaambiwa kwamba huyu bwana amebembelezwa ili agombee.

..taasisi yoyote inapoamua kutafuta mtu wa kuiongoza nje ya taasisi hiyo, basi uwezekano mkubwa ni kwamba walioko mle ndani wamekosa sifa za kuipeleka mbele taasisi hiyo.

..sasa ni nini kimeisukuma CCM kutafuta mgombea nje ya makada wake ambao wako-active?

..Je, ni kukiri kwamba makada na watendaji wa CCM kwenye chama na serikali wamechoka na hawana uwezo?

..kwanini wananchi wachague chama hiki, wakati wenye chama wenyewe wanakiri kwamba wameshindwa kiasi kwamba wamelazimika kwenda "nje ya chama" kutafuta mgombea?

..Je, Jaji Ramadhani atatimu makada wote wa ngazi za juu, kati, na chini, ili kusimika mfumo mpya utakaoendana na matakwa ya wananchi? Uwezo huo anao?

cc Rev. Kishoka, Kapwela, Mkandara, Ritz, Kobello, Kiranga, Nyani Ngabu, Mzee Mwanakijiji, Ngongo, zumbemkuu, ZeMarcopolo, VUTA-NKUVUTE, Mag3, Pasco, Nguruvi3

Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.
 
Jaji Ramadhani ametimiza miaka mitano kama mwanachama wa CCM ili kukidhi masharti ya kugombea urais kwa tiketi ya chama?

Si amestaafu Ujaji Disemba ya 2010?

Sasa ina maana alikuwa mwanachama wa CCM wakati akiwa Jaji?
Hapo sasa!
 
Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.
Kiranga anasema miaka 5 haijatimia. Maswali zaidi yanazuka, je aliwahi kuwa mwanachama wa CCM?
Je, uanachama wake ulikoma lini?
Je, uanachama mwingine ulianza lini?
Nini nafasi ya mahakama katika kutoa haki ikiwa majaji wanakuwa makada wa serikali? (chama legelege huzaa serikali legelege-JKN)

Hata kama hajawa mgombea, kutajwa tu jina lake kunatia ukakasi.
Kuombwa kugombea ndilo chimbuko la swali la ZeMarcopolo. Je CCM wamefikia hatua ya kutafuta tafuta wakiwa madarakani miaka 50?

Je, walioko hawafai na kama hawafai nini uimara na udhubuti wa chama?
Je, wanastahili muda zaidi au wapewe muda wa kupunzika ili wajaipange zaidi?
 
Hakuna matakwa ya kikatiba ya miaka mitano.
Hakuna ushahidi kuwa ameombwa na CCM.
Yeye ni mwanachama, huwezi kumtenganisha na wanachama wengine. Ana haki zote.
Ni kweli kuwa kugombea kwake kunaacha maswali, ila speculations pia zinaongeza maswali.
 
Mkuu ima nimechanganyikiwa au kuna kitu sielewi. Samahani naomba nisome uzi vizuri tena
 
Kadi yake ni ya 1993.
Mkuu haya niliyaandika sehemu fulani, ukipata nafasi yasome.

Kwa mujibu wa gazet la UHURU (Ukweli daima) la Alhamisi Juni 18, 2015 Toleo namba 22159 (ISSN 0876-3896), katika habari iliyopewa kichwa cha habari ya URAIS CCM 2015 Yametimia iliyoandikwa na Happiness Mtweve akiwa Dodoma na ikiwa inapatikana ukrasa wa kwanza baadaye ukrasa wa nne ni kuwa :

1. Jaji A. Ramadhani alilazimishwa kujiunga na TANU ya wakubwa kisa alikuwa anataka kujiunga na JWTZ mwaka 1971 (1969 alikuwa mwanachama wa TANU Youth Leage). Alilazimishwa kujitoa TANU 1992 (maana hatuelezwi alijiunga na CCM lini na kama alikuwa na kadi ya CCM wakati huo) kutokana na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kipindi hicho.

2. Jaji Agustino R. alijiunga na chama cha mapinduzi (CCM) mwaka 2011. Bahati mbaya hakueleza sababu na shabaha/lengo zilizomfanya ajiunge na CCM zaidi ya kusema alikuwa huru kujiunga na chama cha Siasa. Alitakiwa atueleze kwa nini hakujiunga na vyama vingine, Je. mwaka 2011 alikuwa anaridhishwa na mwenendo wa CCM kuwasaidia watanzania kujikwamua katika kupambana na kushinda vita dhidi ya maadui Ujinga, Umasiki, maradhi na sasa Rushwa(Ufisadi)...?

3. Jaji A. Ramadhan katika maelezo yake hakuna anapoonyesha kuwa aliwahi kuwa ama barozi wa nyumba kumi kumi (shina) wa CCM, mwenyekiti wa tawi (kijiji/mtaa) wa CCM, hadi ngazi zote za CCM kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taifa. Kwa mujibu wa taratibu za CCM ikiwa rais atachuguliwa akiwa mwanaCCM kuongoza nchi ni lazima awe mwenyekiti wa CCM taifa. Sasa huyu Jaji Agustino R. ambaye hana uzoefu wowote kwenye uongozi wa Chama cha CCM ataaminikaje kupewe jukumu zito hili la uenyekiti wa Chama. Katika kanunu kumi na tatu za CCM kupata mgombea kanuni ya Uzoefu imezingatiwa. Nina imani pia Uzoefu kwenye uongozi wa ndani ya chama cha CCM umezingatiwa. kama nina amini kwa usahihi Jaji, Brigedia Msataafu na mchungaji A. Ramadhan hastahili kupeperusha bendera ya cha CCM kwenye nafasi ya Urais wa nchi hii.

KUMBUKA:
Gazeti la UHURU (Ukweli daima) utolewa na Uhuru Publications Limited iliyopo Dar es Salaam na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo anapatika kupitia namba +255(0) 713 410008 (kama ilivyoonyeshwa kwenye ukrasa wa sita- chini kwenye kona kushoto wa Gazeti hilo toleo namba 22159 la tarehe 18/06/2015).
 
Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.

..hoja yangu ni kwamba hajawahi kushika nafasi yoyote ile kubwa ya kisiasa.

..kwa mfano hajawahi kuwa mbunge. hajawahi kutumikia serikalini.

..uzoefu wake uko kwenye mhimili wa mahakama.

NB:

..habari kwamba ameombwa agombee zilitoka kitambo kidogo ktk gazeti la raia mwema. nadhani ni jarida linaloaminika.

cc Pasco, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
....CCM....
Je, wanastahili (CCM) muda zaidi au wapewe muda wa kupunzika ili wajaipange zaidi?

Hili pia nililiandika sehemu fulani humu jamvini

Ili CCM iweze kujisafisha inatakiwa ikae nje ya Utawala kwa miaka 10. Hapo wale CCM imani/wapinga rushwa ndiyo wataonekana (watakao baki) na ndiyo watakao kipa uhai mpya wa kukubalika kwa wananchi. Vinginevyo hakiwezi kujichekecha kikiwa na majukumu mazito ya kiutawala...!
 
kama ameshawishiwa basi kashawishiwa na wapambe wake,ambao watafaidika na nafasi yake kama atapata,sio CHAMA
nasikia watu wanazungumza kuhusu Ujaji,hivi Warioba ni Jaji au,na ni mwanachama wa CCM
Jaji A.Ramadhani, kadanganywa na uchambuzi wa Mtatilo
 
Mpaka dakika hii sitaki kuamini kwamba Jaji Augustino Ramadhani kaamua kuchukua fomu kwa utashi wake mwenyewe. Ninachojiuliza ni mbinu gani wametumia mafisadi walioiteka CCM mpaka akawakubalia, what hold do they have on him maanake kwa vyovyote vile watakuwa wamempa offer he cannot refuse.

Hakuna watu hatari kama CCM wakinuia kukushughulikia if you don't toe the line. Ni siri gani wanayo mpaka wamemnasa kirahisi hivyo? Nasema hivyo kwa sababu sioni ni kwa vipi ameweza kuafikiana nao hadi kuchukua fomu kupitia CCM, je kasalimu amri kwa mafisadi? Since he couldn't fight them, he has joined them.

There is something very fishy here, Jaji yaonekana kalamba garasha.
 
Samahani mkuu,

Kwani kuna ajabu Jaji Ramadhani kuchukua form? Inamaana alikuwa anapingana nao siku za nyuma? Kwanini apingane nao?
 
kinachonifurahisha ni jinsi gani hata yule aliye safi anapigwa vita vya kiufundi. Je Watanzania mnamtaka nani? Maana hakuna hata mgombea mmoja ambaye hatazushiwa visababu vya mikingamo na mizengwe.

Kama tulidiriki kumpa Kada mzoefu na ameshindwa kabisa kukiongoza chama katika mstari ulionyooka na njia sahihi (Kikwete), iweje leo tumhofie Jaji Ramadhani eti ni shina gani aliwahi kuliongoza?

NI makada wangapi tena waliosomea Kivukoni na hata nchi za kijamaa ambao leo wamewageuka watanzania na wana CCM wenzao kwa kuabudu mali, utajiri na utegemezi na kuachana kabisa na dhana ya juhudi, maarifa, ujamaa na kujitegemea?

Mtu kuamua kuchagua chama ni utashi, sawa na kuchagua mume au mke, sawa na ushabiki wa Simba na Yanga, iweje tumhoji leo kwa nini hakwenda chama kingine?

Kama tutamhoji yeye kwa nini aende CCM chama kichafu, basi tuwahoji wanachama wote Milioni 7 kwa nini wanashabikia chama kinachoangamiza maisha ya Watanzania wengine Milioni 35?

Kama mtu ana dhamira ya kweli, ana busara, hekima na uimara wa kukemea, kuadhibisha, kukiri makosa na usikilivu akajitwisha mzigo huu mkubwa, basi na tumpe nafasi hiyo bila kutafuta visingizio vya kumnyima hiyo nafasi.

Mbona hatushangai umahiri wa mawaziri utitiri na watangaza nia wengine wa CCM ambao wamekaa ndani ya CCM kama vigogo na watendaji ndani ya NEC na CC, lakini bado CCM inakwenda mrama na Tanzania inaangamia katika lindi la umasikini?

Kumjibu JokaKuu- Serpent General swali lake je ataweza? nasema ni jukumu letu kumwezesha kuifanikisha kazi hii kwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita na kuuchukia mfumo wa kinyonyaji uliotuzalishia uvivu, uzembe, ufisadi na kulelea kutokuwajibika na kukomaza umasikini.

Yeye kutokuwa ndani ya NEC na CC ni jambo zuri kabisa tena sana maana akiupata uenyekiti, atakuwa hana makundi au kuburuzwa na mifarakano ndani ya chama, bali naomba Mwenyezi Mungu yeyote atakayeshinda, aisimamie haki kwa busara, hekima na uimara Taifa lisonge mbele.
 
..hoja yangu ni kwamba hajawahi kushika nafasi yoyote ile kubwa ya kisiasa.

..kwa mfano hajawahi kuwa mbunge. hajawahi kutumikia serikalini.

..uzoefu wake uko kwenye mhimili wa mahakama.

NB:

..habari kwamba ameombwa agombee zilitoka kitambo kidogo ktk gazeti la raia mwema. nadhani ni jarida linaloaminika.

cc Pasco, Nguruvi3

Jokakuu:

Alikuwa jeshini na kufikia cheo cha ubrigedia. Hivyo uzoefu anao wa kiserikali. Au jeshini haiingii kwenye hesabu za kiserikali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom