Kuscratch kwa ITV kupitia Star Times

Kuscratch kwa ITV kupitia Star Times

Mkuu hizo ni habari za kweli kabisa na imefanya mimi nihamie ting, isitoshe jana imetoka katika vyombo . ukweli ni kwamba taarifa ya ITV haina ubaguzi wa vyama wala propaganda,kwa hiyo watu wengi huipenda na ndo maana inafanyiwa saboteji. Kwa kuwa wewe unatumia DSTV za ninyi wakubwa, huwezi kujua kadhia hii.

Mkuu Dstv sasa hivi haina ukubwa, ukiwa na Tsh. 99,000 tu unaunganishwa. Bei sawa na simu ya mchina.
 
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kuna maeneo kadhaa hapa nchini pamoja na nyumbani kwangu, ambapo matangazo ya ITV & EATV (Startimes) yamekuwa yanakwama sana na kutoa picha mbaya na tena ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Sasa ni hivi kwa upande wangu ninapoona matangazo ya ITV hayaonekani vizuri huwa ni bora nikazima TV kuliko kuangalia habari ya TBC.

Nawasilisha wakuu.
KILAKA.

Safi sana na hongera kw kujitambua mimi nilisha acha kuangalia tbc ccm siku nyingi maana hawajitambui na hicho king'amuzi cha startimes nilishakitupa siku nyingi nilikitumia wiki moja tu baada ya hapo nilikitupa kule
 
Arusha ndio hamna kabisa matangazo, nyie washenzi star times kama mmeshidwa biashara timueni mlikotoka

Huu ushabiki maandazi wa startimes utafanya ving'amuzi vyao vikose soko na kushindwa kibiashara.
 
Sijajua kwa nini umeamua kuja kutudanganya, wewe ni mfanyakazi wa startimes???
Nimekudanganya nini? Unakataa kwamba ITV/EATV na Star Tv walishawahi kuziondoa stations zao Startimes lakini wakalazimishwa kuzirudisha? Unakataa kwamba IPP Media hawamiliki ving'amuzi vya Digitek? Unakataa kwamba Star Tv hawamiliki ving'amuzi vya Continental? Unachoona umedanganywa ni nini?
 
Unamaanisha star tv,itv eatv wao ndio wanavuruga matangazo yao???
ili iweje???

Simple, wanataka watu walazimike kununua vingamuzi vya IPP Media au StarTV, tangu mwanzao Kampuni hizo zilikuwa hazitaki matangazo yao yapitie STARTIMES.
 
Huu ushabiki maandazi wa startimes utafanya ving'amuzi vyao vikose soko na kushindwa kibiashara.
Hilo ndio swali la msingi uliotakiwa kujiuliza... itakuwaje Statimes waifanyie hujuma ITV wakati wanafahamu kwamba ITV ndio kituo kinachoangaliwa na wengi kiasi kwamba hata DStv ilikuwa kila siku malalamiko kwavile tu hakukua na ITV hadi pale walipoamua kuuingiza hivi majuzi!
 
Simple, wanataka watu walazimike kununua vingamuzi vya IPP Media au StarTV, tangu mwanzao Kampuni hizo zilikuwa hazitaki matangazo yao yapitie STARTIMES.
Ukweli ndio huo... nashangaa wengine tunausema mleta mada anasema tunadanganya! Ina maana Startimes ni wapumbavu waifanyie hujuma ITV wakati wanafahamu inaangaliwa na watu wengi!!!
 
KILAKA

Ni kwamba ITV na EATV wanahujumiwa na Startimes au ni wao wanaihujumu Startimes? Kumbuka kwamba, IPP Media waligoma kuweka stations zao kwa Startimes na ilifikia wakati wakaziondoa lakini baada ya kukomaliwa na TCRA, ndipo wakazirudisha! Na si hao tu, hata Star TV nao waliondoa channel kwenye Startimes lakini wakarudisha kwa kulazimishwa! Wote hao, yaani ITV, Star TV na EATV zinapatikana kwa shida sana Startimes... lakini kupitia DSTV, hakuna matatizo!

Hivyo basi, kama kuna hujuma basi hujuma hizi ni kinyume na hivyo unavyosema!

Swadakta mkuu
 
Last edited by a moderator:
Simple, wanataka watu walazimike kununua vingamuzi vya IPP Media au StarTV, tangu mwanzao Kampuni hizo zilikuwa hazitaki matangazo yao yapitie STARTIMES.

aisee....now i get it....ndio maana startimes wameweka tangazo linapita kuwa KUNA MUINGILIANO KWENYE CHANNELS ZA ITV/EATV AMBAZO ZIKO NJE YA UWEZO WAO NA WAMESHAWATAARIFU TCRA WASHUGHULIKIE HIO ISSUE......aisee hii hujuma ili watu waichukie startimes na startimes wametoa taarifa very professional!
 
Mkuu Dstv sasa hivi haina ukubwa, ukiwa na Tsh. 99,000 tu unaunganishwa. Bei sawa na simu ya mchina.

Nakubaliana na wewe mkuu, lakini malipo yake kwa mwezi yanaanzia 17000/, 34000/,54000/ steheni za kawaida kabisa. Ukitaka stesheni za michezo unaanzia 92000/ mpaka 142000/ hapo masikini kama mimi nitamudu?.Wakati Startimes inaanza na bundle ya 3000/.
 
aisee....now i get it....ndio maana startimes wameweka tangazo linapita kuwa KUNA MUINGILIANO KWENYE CHANNELS ZA ITV/EATV AMBAZO ZIKO NJE YA UWEZO WAO NA WAMESHAWATAARIFU TCRA WASHUGHULIKIE HIO ISSUE......aisee hii hujuma ili watu waichukie startimes na startimes wametoa taarifa very professional!

Mkuu kwa mtu mwenye weledi mkubwa katika nyanja za mawasiliano especially yanayo husu BROADCASTING, kuna kanuni kwamba husitumie channel ambayo hipo channel tisa above na below ya kwako kwa upande wa picha na usitumie tano above na below upande wa sauti - hukifanya kosa hilo hakuna chombo chochote Duniani kinaweza kuondoa muingiliano ya mawimbi. Kwa hiyo mimi sishangai Wachina au TBC kulifikisha suala hilo TCRA, mimi siamini kama mafundi wa IPP Media hawalijui hilo, lakini kwa Tanzania everything goes wenda hikawa hawalijui hilo au ni maksudi tu.
 
Ukweli ndio huo... nashangaa wengine tunausema mleta mada anasema tunadanganya! Ina maana Startimes ni wapumbavu waifanyie hujuma ITV wakati wanafahamu inaangaliwa na watu wengi!!!

Mkuu NasDaz, kitu nilicho kuja gundua katika Taifa letu - kuna baadhi ya Wazalendo wenzetu ambao wako overy selfcentered hawataki ushindani,sometimes wana-behave like Demi-Gods wanakuwa na an inflated view of their importance katika Taifa letu - wakilazimishwa na Serikali ku-comply na sheria za nchi katika masuala ya Mawasiliano - wanakubali kwa shingo upande lakini behind the scene wanatafuta mbinu mbadala za kuweka spana katika efforts za Serikali yetu za kuwachia Wananchi wachangue Mrusha matangazo wanae mtaka, mark you mbinu ziko nyingi.
 
And you know what? Let's call a spade a spade! Kama utakumbuka, wakati TCRA wanazima analojia kwa mara ya kwanza Dar es salaam, "Mzalendo" Mengi alipiga kelele sana kwa gia ya kuwatetea wananchi wasio na uwezo wa kununua ving'amuzi vya Startimes kwamba wanegenyimwa uhuru wao wa kupata habari! Wapo ambao walimuamini lakini kwa upande wangu niliona is just a big lie... nilifahamu wazi kwamba wananchi hapa tunataka kutumiwa tu! Bahati mzuri, TCRA walikomaa na muda si mrefu ikaja kubainika kwamba Mzalendo Mengi alikua anapinga kuzimwa kwa mitambo ya analojia kwa kuwa ving'amuzi vya Digitek vilikuwa njiani kuingia sokoni kwahiyo alichelea kwamba endapo mitambo ingezimwa, majority wasingekuwa na alternative zaidi ya kununua ving'amuzi vya Startimes to the point hadi kuingia kwa ving'amuzi vya Digitek, tayari majority ingekuwa wameshanunua ving'amuzi vya Startimes! Kwa kuliona hilo, ndipo Mzalendo Mengi akaingia na gia za kututetea akina NasDaz tusio na uwezo!!!

Maajabu yakaja pale baada ya Digitek kuingia sokoni... si tu kwamba Mzalendo Mengi aliachana na uwezo la kututetea maskini bali siku chache baadae akaamua kuondoa ITV/EATV toka Startmes wakati anajua kabisa wale maskini aliokuwa anatutetea kimbilio letu ndo lilikuwa kwa ITV/EATV kwavile zilikuwa zinapatikana bure hata usipokuwa na pesa ya kulipia monthly charges!

Kwahiyo, kama ni hujuma binafsi naamini hujuma inayofanywa na wenyewe ITV/EATV na Star Tv!
 
Last edited by a moderator:
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kuna maeneo kadhaa hapa nchini pamoja na nyumbani kwangu, ambapo matangazo ya ITV & EATV (Startimes) yamekuwa yanakwama sana na kutoa picha mbaya na tena ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Sasa ni hivi kwa upande wangu ninapoona matangazo ya ITV hayaonekani vizuri huwa ni bora nikazima TV kuliko kuangalia habari ya TBC.

Nawasilisha wakuu.
KILAKA.

habari yako

ni kweli tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa wateja wetu kuwa ITV na EATV zinasumbua wakati wa jioni hasa muda wa taarifa ya habari, sisi kama STARTIMES tunaamini kuwa ITV ni moja ya chanel pendwa Tanzania na hivyo tunaamini pia uonekano mzuri wa chanel hii utafanya wateja wetu wafurahie huduma za ving'amuzi vyetu. kwa hivyo SIO KWELI KWAMBA STARTIMES TUNAIHUJUMU ITV.

Tatizo la kukwama kwa ITV kwa kipindi hichi limetokea sana kwa wakazi wa dar es salaam hii imekuwa ni kutokana na interference ya mawimbi hasa wakati wa jioni kwa chanel hizi ambao upo nje ya uwezo wetu. Naomba nikujulishe kwamba TCRA TUMESHAWAJULISHA KUHUSU TATIZO hili na tunafanya nao kazi kwa ukaribu sana kutatua tatizo kwani pia inahitaji ushirikiano wa karibu na wahusika wa upande wa pili

Tunaomba ieleweke wazi kuwa STARTIMES ni kampuni inayopenda watazamaji wake wafurahie vipindi, na wala haina shida na ITV kama inavyoelezwa na baadhi ya watu. Kwa mara kadhaa tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa watamazaji wetu wanafurahia chanel zoote za ndani bure na ndio maana mara kadhaa ITV na baadhi ya chanel walipotoa chanel zao tulijaribu Kufanya kila linalowezekana kuhakikisha zinarudishwa kwa kushirikiana na mamlaka husika

STARTIMES tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanafurahia ulimwengu wa digital. Hivi karibuni kumekuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara na hivyo unafanya watu wasio waaminifu kueneza habari zisizo sahihi kwa wateja wetu.

KUMBUKA STARTIMES tumekuwa pia na huduma ya satelite dishi ambapo ITV na chanel zingine zimekuwa zikipatikana bila matatizo yeyote. TUNAOMBA WATEJA WETU waendelee kufurahia huduma zetu na sisi tunajitahidi kadiri tunavyoweza kuhakikisha tatizo hili linatatuliwa mapema iwezekanavyo.
 
Hata kwangu itv ni tatizo kweli taarifa ya habari ya saa 2 usk kutazama ni shida kubwa,startimes haitufai tena WATANZANIA na hao wafanyabiasha wa kichina wafanye biashara waache ujinga unless watapata hasara kwa upumbavu wao

Asanteni Star times tanzania.
Bila shaka tunaaamini tatizo hilo litakwisha soon na tunaamini tutashirikiana kwa karibu sana maana tuna wahitaji.
Asanteni kwa ufafanuzi.
 
ahsante kwa ufafanuzi ninaamini tatizo mutalitafutia ufumbuzi ili watazamaji tuendelee kupata matangazo na habari kama kawaida.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001: 2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU MUINGILIANO WA MASAFA YA EATV NA ITV KUPITIA KING’AMUZI CHA KAMPUNI YA STAR MEDIA KATIKA KITUO CHA KUSAMBAZA MATANGAZO MAKONGO JUU

A. UTANGULIZI
1. Masafa ni rasilimali muhimu katika shughuli za Mawasiliano (simu, wavuti, redio, na utangazaji). Masafa ya Mawasiliano (Spectrum) hugawanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (ikitambuliwa hapa kama Mamlaka) kwa kutoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni. Moja ya kazi za Mamlaka ni pamoja na kupokea na kusuluhisha matatizo ya muingiliano wa masafa kati ya watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano kwa kutumia ujuzi na wataalamu na teknolojia ya mitambo maalumu na mahususi ya kisayansi kufanya kazi hiyo. Kazi hizi zimeainishwa katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 (TCRA Act of 2003) na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act (EPOCA) ya mwaka 2010.
2. Mnamo tarehe 29 Januari 2015, Mamlaka ilipokea malalamiko kuhusu ubora wa matangazo ya vituo vya ITV na EATV yanayorushwa na Kampuni ya Star Media (T) Limited ambaye ni msambaza matangazo ya dijitali. ITV na EATV wana leseni ya Maudhui (Content Service Lisence) na Star Media wana leseni ya Miundombinu ya Utangazaji (Network Facility License as a signal distributor) kutoka TCRA. Leseni zote za Mamlaka zina masharti ya kuzingatia.
3. Huduma za Mawasiliano hutumia bendi ya masafa tofauti (Spectrum bands). Huduma za mawasiliano ya setilaiti (satellite) hutumia bendi 3.4 mpaka 4.2 GHz, inayofahamika kama C-Band. Ifahamike kuwa masafa ya setilaiti ya kupokea matangazo (satellite downlink frequency) ya 3.644 GHz yanatumika kupokea matangazo kutoka satelaiti ya Intelsat 906 (TP 10) kwa matangazo ya vituo vya utangazaji nchini kupitia mfumo wa dijitali ambao mitambo yake iko katika kilima cha Makongo Juu area. Hata hivyo, sehemu nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, hutumia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.5 GHz. Masafa haya yanafahamika duniani kote kwa uwezo wake wa kutumika kiteknolojia kati ya mfumo wa “Fixed Satellite Services (FSS)” na IMT kama vile mwendo kazi wa intaneti bila waya (Broadband Wireless Access (BWA) transmission) ikiwemopia teknolojia ya WiMAX.
4. Kufuatia malalamiko yaliyopokelewa na Mamlaka, TCRA iliteua timu ya wataalamu Wahandisi wa Masafa kufanya uchunguzi ili kubaini tatizo la muingiliano wa masafa yaliyosababisha ITV na EATV kutokuonekana vizuri katika king’amuzi cha Star Media, kwa kutumia utaratibu na jinsi sheria zinavyoelekeza. Timu hiyo ya wataalamu wa masafa iliwasiliana na Star Media na kutembelea eneo la Makongo Juu kwenye mitambo yao ili kubaini aina ya muingiliano, muda wa muingiliano na maeneo husika. Timu hiyo ilifanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu kwenye eneo lenye mitambo ya kurusha matangazo ili kubaini muingiliano wa masafa kupitia watoa huduma wa intarneti za mwendo kasi kupitia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.4 – 3.6 GHz. Aidha timu ilifanya tathmini ya vipimo vya matumizi ya masafa na watoa huduma katika bendi nzima ya C- ya kupokelea matangazo (downlink frequency) kutoka 3.4 GHz hadi 4.2 GHz.

B. MATOKEO YA UCHUNGUZI NA YALIYOJITOKEZA

5. Baada ya uchunguzi huo wa kitaalamu kwa kutumia vifaa maalumu vya teknolojia ya sayansi ya masafa, timu ya wataalamu walibaini kuwa muingiliano wa masafa ulikuwa unatokea kati ya saa 12 jioni hadi saa 6 usiku. Uchunguzi katika eneo la urushaji wa matangazo na mitambo ya Star Media ulibaini kuwa muingiliano ulikuwa katika mfumo wake wa kupokea matangazo (satellite receiver station) iliyoko kwenye eneo (S 06◦ 45’ 736 E 39◦ 12’ 632). Mfumo wa kupokea (Low Noise Block down converter - LNB) kutoka bendi 3.4 GHz to 4.2 GHz. Matokeo ya uchunguzi wa masafa ya bendi 3.644 GHz hayakuonesha aina yeyote ya muingiliano. Aidha masafa ya 3.4 GHz hadi 3.6 GHz yalionesha matumizi mbalimbali kutoka masafa ya bendi 3.5 GHz ambayo yanatumika na watoa huduma wanaotumia teknolojia ya WiMAX.

6. Kutokana na matokeo ya uchunguzi kama ilivyoelezwa katika no 5, ilibainika wazi kuwa hakukuwa na muingiliano katika bendi hiyo (In-band interference) kutoka katika mfumo wa matumizi ya inteneti ya mwendo kasi kwani masafa yote katika mifumo yote ya utoaji huduma haikuonesha muingiliano. Vile vile ilithibitika wazi kuwa hakukuwa na muingiliano katika mfumo huo (out-of-band emissions) Mfumo wa huduma wa mwendo kasi wa inteneti unaotumia masafa ya bendi 3.5 GHz huweza kusababisha muingiliano kwa mtoa huduma anayetumia bendi 3.6 – 4.2 GHz (FSS stations).

7. Matokeo ya vipimo vilionesha kuwa eneo la Makongo Juu hupokea mawimbi ya Mawasiliano kutoka kwa watoa huduma wote wanaotumia masafa ya 3.5 GHz kutoka meneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na eneo la Makongo kuwa juu. Hali hii inaweza kusababisha mawimbi ya mwendo kasi wa intaneti katika masafa 3.5 GHz kuibebesha mzigo mkubwa mtambo wa kupokea matangazo ya utangazaji (FSS stations) anayetumia bendi 3.4 – 4.2 GHz kama hakuna wigo wa kuzuia muingiliano kiteknolojia (band pass filter) au mfumo bendi mwembamba (narrow band LNBs).

C. KUTATULIWA KWA MUINGILIANO WA MASAFA

8. Kutokana na vielelezo vya matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa masafa kwa kutumia vifaa maalumu, Mamlaka ilitoa maelekezo kwa Star Media ili kutatua tatizo la muingiliano uliokuwepo katika mtambo wake wa urushaji matangazo Makongo Juu. Kwanza, kutumia kifaa kiitwacho IF attenuator/filter katika mitambo yake ya kupokelea mawasiliano ya matangazo ya setilaiti (FSS receiving station); Kutumia LNB converter katika bendi ya masafa 3.7 – 4.2 GHz badala ya kutumia masafa ya (C-band) yote (3.4 – 4.2 GHz); hata hivyo, masafa 3.664 GHz yamehifadhiwa kama wigo unaozuia matumizi kati ya watumiaji wa matangazo ya mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi (Terrestrial) - (3.4-3.6 GHz) na yale ya wanaotumia Satelaiti ya kupokelea matangazo (3.7-4.2 GHz). Pili, Mamlaka ingeagiza watoaji wa inteneti ya mwendo kasi katika mitambo yao (BWA) kuwa na nafasi ya kutosha kati ya mitambo ya “FSS” na kufuata utaratibu uliowekwa kulingana na matumizi ya masafa, ikizingatiwa kwamba mawimbi yaliyo mengi katika eneo la Makongo Juu hupokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka Jiji la Dar es salaam. Tatu, njia mbadala zitumike katika kupokea matangazo ya utangazaji katika kilima cha Makongo Juu kama vile teknolojia ya Mkongo wa Mawasiliano (fiber optic) satelaiti kutumia mfumo wa bendi ya Ku-Satellite band, au “microwave links”.

9. Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa kutumia vifaa maalumu vya sayansi na teknolojia mahususi kwa matatizo ya muingiliano wa masafa, imebainika pasina shaka kuwa hakukuwa na hujuma yeyote kutoka kwa Kampuni ya Star Media au kufanya kwa makusudi kwa nia ya kuharibu muonekana wa vituo husika vya ITV na EATV katika ving’amuzi vyake. Tatizo lilikuwa ni la kisayansi na kiteknolojia ambalo hutokea mara nyingi katika huduma za Mawasiliano kote duniani, na tatizo hilo limemalizika kwa kutumia njia za kisayansi na kiteknolojia kwa watoa huduma wote kwa kushirikiana na Mamlaka..

10. Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) inapenda kutumia fursa hii kuwakumbusha watoa huduma wote wenye leseni za Mamlaka kuwa inapotokea matatizo au malalamiko, basi wafuate taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa TCRA na kutoa ushirikiano katika kutatua tatizo husika kupitia sayansi na teknolojia ambayo hutumika katika kutoa huduma za mawasiliano.

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia dg@tcra.go.tz

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

5th February 2015
4
 
Back
Top Bottom