Kongosho
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 35,987
- 24,234
- Thread starter
- #41
Umeongea jambo la maana sana.
Mzazi inabidi ajue anafanya nini na mtoto wake yuko hatua ipi, ndio maana wewe hukusita kumshawishi asome darasa la saba.
Sasa kuna wengine mtoto kupata A tu, anamrusha darasa. Kuna wakati mtoto anapata A ila nguvu aliyowekeza kwenye A hiyo ni kubwa mno, darasani, twisheni, kujisomea, na kadhalika.
Ukimrusha darasa inaweza leta matokeo tofauti.

Sioni shida sana ya kurusha mtoto darasa, ingawa kuna changamoto ya kuwa na wanafunzi wenzake ambao wanamzidi mno kiumri.
Mwanangu mimi alisoma shule ambayo ilikuwa wanaishia darasa la sita na kufanya mtihani wa cambridge then form one; alikuwa na miaka 10 akiwa darasa la sita, ina maana angeanza form one akiwa na miaka 11 ilahali wenzake wengi wana miaka 15. Niliona shida kidogo pindi atakapoenda boarding huko secondary hivyo nikaongea naye kuhusu kusoma mwaka wa 7 ili afanye mtihani wa Taifa, akakubali na hivyo akadelay kwa mwaka mmoja (ili amature kidogo); so now yu form one na he is 12 and he seems to be okay, na bahati njema sana shule yake hawachukui form one ambao ni over 14yrs.
Kama alivyosema The Boss hakuna ulazima sana wa kusoma madarasa yoote hayo kama mtoto ni genius, ila tunaweza kumnyang'anya mtoto hali ya kuwa na watoto wenzake wenye umri sawa +-2 years na kumfanya achangamane na watu wakubwa zaidi, ambayo yaweza:-
1: Kumpunguzia confidence (asiwe huru kutoa mawazo yake kwa kuwa mdogo hajui chochote)
2: Kumkuza haraka (kuongea, kureason, kuact like mkubwa)
3: Kumsababishia abuse (ingawa mara nyingi watoto wanakuwa everybody's favourite)