Kurusha Mtoto Darasa . . .

Kurusha Mtoto Darasa . . .

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
35,987
Reaction score
24,234
Jana nilipeleka kijana kufanya mtihani wa kuanza kidato cha kwanza, wakati niko pale kukawa na akina mama wengine. Katika maongezi mama mmoja akasema kaleta binti yake wa darasa la sita kufanya mtihani huo, akifaulu anaruka la saba na kuanza kidato cha kwanza.

Na kuwa wakati, kuna mama mmoja tunafanya naye kazi alimrusha binti yake toka darasa la tatu na kuingia la tano, maana yake hakusoma darasa la nne kabisa.

Sasa mie nataka kujua kutoka kwa wadau.

  1. Unapomrusha mtoto darasa hakuna hasara yeyote? iwe kielimu, mahusiano yake na wanafunzi wenzie na saikolijia nzima ya mtoto(Ukizingatia mchana na usiku anakula ugali-kuna sred niliona mtu kasema ugali unasababisha mtu awe kilaza)
  2. Kuna faida yeyote kurusha mtoto darasa?

Next week nitakuja na 'kupeleka watoto shule za bweni (kwa elimu ya msingi na shule za awali)

cc EMT Dark City King'asti gfsonwin snowhite Kaizer Kaunga watu8
 
faida ipo sana,una save muda(mwaka) na fedha pia so far kwa hao watoto wa kike ni vizuri kwa sababu hawachelewi kuharibikiwa kabla hawajajijenga kimaisha(kielimu),hasara for sure hamna hata moja
 
Nyerere aliruishwa madarasa..

kama mtoto ni 'genius' ni bora arushwe darasa
ili 'asiboreke' kusoma na vilaza
na pili afike juu mapema kabla ya kubaleghe au kuvunja ungo na kujifunza 'interest' zingine

elimu ya Tz ni mbovu na ndeefu mno na masomo meengi mno
inachosha

hata wahindi wengi huwarusha watoto wao madarasa
ukienda shule za Mzizima na Shaaban Robert wengi wametoka la sita na kuanza form one

wanasema ni vizuri mtoto afike chuo kikuu akiwa hata 16 years old
ili concentration na 'dreams' zake za utoto ziende sawa

many scientists including Bill Gates walijua nini wasome wakiwa hata miaka 10
hawafikia ....na hawakupata interruption zingine za life.....

ukisha balehe unaanza interest zingine zinaleta 'distraction' na 'dreams' za utotoni..
 
Una save muda wa nini? Nani kasema kachelewa na kwa vigezo gani?

Ni kweli watoto wanaorushwa madarasa hawaharibikiwi?

Watoto wanaorushwa madarasa wana mafanikio zaidi ya watoto ambao hawakurushwa madarasa?

Na mafankio ya mtoto yanapimwa kwa 'monetary value' tu? Vipi saikolojia ya mtoto? Kumpokonya utoto wake? Hivi Michael Jackson alifanikiwa?

Nyerere aliruishwa madarasa..

kama mtoto ni 'genius' ni bora arushwe darasa
ili 'asiboreke' kusoma na vilaza
na pili afike juu mapema kabla ya kubaleghe au kuvunja ungo na kujifunza 'interest' zingine

elimu ya Tz ni mbovu na ndeefu mno na masomo meengi mno
inachosha

hata wahindi wengi huwarusha watoto wao madarasa
ukienda shule za Mzizima na Shaaban Robert wengi wametoka la sita na kuanza form one

wanasema ni vizuri mtoto afike chuo kikuu akiwa hata 16 years old
ili concentration na 'dreams' zake za utoto ziende sawa

many scientists including Bill Gates walijua nini wasome wakiwa hata miaka 10
hawafikia ....na hawakupata interruption zingine za life.....

ukisha balehe unaanza interest zingine zinaleta 'distraction' na 'dreams' za utotoni..
 
Cha muhimu ni kupima uwezo wa mtoto, Kama mtoto ana uwezo na uelewa wa Haraka, unaweza kabisa kumrusha Darasa, hakuna hasara yoyote
 
^^
Hapo ndipo lilipo tatizo la uelewa kwa wazazi..wanaoandaa Curriculum si kwamba hawajui kuwa kuna watoto bright! Faida za mtoto kutorukishwa darasa ni hizi
....
ELIMU INAHUSU KUPATA UZOEFU
Mtoto hafundishwi kukariri tu notisi badala yake anajifunza ushirikiano,uvumilivu,upendo na kusameheana na wenzake.
....
ELIMU INAHUSU MAKUZI
Shule ni taasisi ya pili baada ya ile ya nyumbani,,taasisi hii imepangwa kimpangilio kulingana na umri wa mtoto.Itakuwa kioja mtoto amalize darasa la saba kwa miezi 7 kisa tu ana uwezo wa kunatisha vitu kichwani,matokeo yake siku hizi mtoto anafika First Year Chuo Kikuu akipata laki nne na nusu ya Bodi ya mikopo anajiona amewin maisha..anasa kama dozi ukimuuliza unajivunia nini? "Najivunia kufika chuo kikuu na miaka 17" Utoto @work
....
ELIMU INAANDAA "MATURED INDIVIDUALS"
Miaka mingi shuleni ina maana pana..moja ni kuepuka kupata watakaojenga familia,taifa,au jamii wakiwa na miili mikubwa akili za mkopo.Shule unajifunza mengi na ndio maana hata kama mtoto amepata Division Four Form Four lakini yuko tofauti na yule aliyeishia form two au la 7
....
Siungi mkono wazazi wa aina hiyo kwa moyo wangu wote na kwa uelewa wangu mdogo huu nilionao
Kongosho mwambie asiwafundishe walimu kazi yao
^^
 
Last edited by a moderator:
Cha muhimu ni kupima uwezo wa mtoto, Kama mtoto ana uwezo na uelewa wa Haraka, unaweza kabisa kumrusha Darasa, hakuna hasara yoyote

^^
Huu ni mtazamo wa Plato aliyeamini kuwa kuna gold children na matokeo yake mawazo yalipokubaliwa upesi nchi zikajenga mifumo ya kitawala kwa familia za kifalme na kupuuzia vipaji vingine vya familia duni..kama anafikiri kuliko uwezo wa anachofundishwa mpe kazi nyingi za kufanya..
^^
 
Hata mie nasita sana kukubaliana moja kwa moja na hii dhana ya kurush mtoto.

Ndio maana nikauliza, mtoto anaweza fanya vizuri darasani, lakini saikolojia yake inakuwa imelindwa?

Na mafanikio ya kielimi ni kupata A tu kwenye masomo?

^^
Huu ni mtazamo wa Plato aliyeamini kuwa kuna gold children na matokeo yake mawazo yalipokubaliwa upesi nchi zikajenga mifumo ya kitawala kwa familia za kifalme na kupuuzia vipaji vingine vya familia duni..kama anafikiri kuliko uwezo wa anachofundishwa mpe kazi nyingi za kufanya..
^^
 
On ma side naona betta kumuwaisha kuanza shule i mean aanze darasa la kwanza akiwa na miaka mitano ili amalize primary xul akiwa na miaka kumi na miwili ila co kumrusha darasa
 
Mie mwenyewe sikusoma la saba. Sijaona any side effects on my part. La saba ni marudio. Sema shida labda inaweza kuja kama waajiri hasahasa serikalini wakitaka vyeti vya la saba (mfano pccb).
 
Kwani lazima uone 'side effect' wewe mwenyewe? Unaowazunguka?

Saikolojia nzima ikoje, ugumu wowote ulioupata ku-cope na wenzio wa kidato cha kwanza?

Na labda kwa nini ulirushwa darasa? Kama hujatali ku share

Mie mwenyewe sikusoma la saba. Sijaona any side effects on my part. La saba ni marudio. Sema shida labda inaweza kuja kama waajiri hasahasa serikalini wakitaka vyeti vya la saba (mfano pccb).
 
Nyerere aliruishwa madarasa..

kama mtoto ni 'genius' ni bora arushwe darasa
ili 'asiboreke' kusoma na vilaza
na pili afike juu mapema kabla ya kubaleghe au kuvunja ungo na kujifunza 'interest' zingine

elimu ya Tz ni mbovu na ndeefu mno na masomo meengi mno
inachosha

hata wahindi wengi huwarusha watoto wao madarasa
ukienda shule za Mzizima na Shaaban Robert wengi wametoka la sita na kuanza form one

wanasema ni vizuri mtoto afike chuo kikuu akiwa hata 16 years old
ili concentration na 'dreams' zake za utoto ziende sawa

many scientists including Bill Gates walijua nini wasome wakiwa hata miaka 10
hawafikia ....na hawakupata interruption zingine za life.....

ukisha balehe unaanza interest zingine zinaleta 'distraction' na 'dreams' za utotoni..

^^
Kuna tofauti hapa naiona..kama unataka mawazo haya yafanye kazi basi kuna mambo mawili ya kuzingatia
1.MFUMO WA ELIMU
Mfumo wa elimu wetu ni 7:4:2:3+
tofauti na nchi nyingine kama Kenya wenye 8:4:3+ India,Sweeden n.k
Hapo ndipo mfumo wa kikoloni tulioubeba na kuanzia hapo malezi ya watoto yakafuata mkondo huo hata Maandalizi ya walimu wetu katika vyuo yanawaandaa ktk dhana ya Child Development ambapo hatua ya adolescence inapewa kipaumbele.
Kama mfumo huu ikiwemo masomo mengi umepitwa wakati ufanye hivyo.
Rejea yako ya Mwalimu Nyerere its a bit more different maana ukifuatilia usomaji wa Mwl Nyerere tangu akiwa pale Mwisenge Musoma ni wazi he was more bright.
....
2 NATURE YA WATOTO WENYEWE
Watoto wetu hawa wa kiafrika asilimia kubwa wanaathiriwa sana na mazingira.Sisemi hawana akili Hapana..lakini kwa sehemu kubwa lishe,umasikini,exposure na mengineyo yanalazimisha wakati mwingine mtaala uchukue muda mrefu kujitahidi kuwaandaa.Mf rahisi sheria ya viboko ya mwaka 1978 ilipotiliwa mkazo na kuondolewa kwa viboko..nidhamu ya watoto imeenda likizo.Hatimae taaluma imepotea hadi serikali imejificha kwenye kampeni za zimamoto za B.R.N. Huko ulaya wenzetu wanafanya specialisation ya masomo na hawana culture ya kubeba extended families ambazo ndizo walimu wetu wanaandaa ku-shape watoto wenu wakidhi matarajio yenu kwao
^^
 
Una save muda wa nini? Nani kasema kachelewa na kwa vigezo gani?

Ni kweli watoto wanaorushwa madarasa hawaharibikiwi?

Kuna shule nyingine za senti meri meri, mfumo wake mwisho ni grade six. Kwa hiyo baada ya hapo nafikiri mzazi atatafuta tu sekondari ili mwana akaanze form one...
 
^^
Huu ni mtazamo wa Plato aliyeamini kuwa kuna gold children na matokeo yake mawazo yalipokubaliwa upesi nchi zikajenga mifumo ya kitawala kwa familia za kifalme na kupuuzia vipaji vingine vya familia duni..kama anafikiri kuliko uwezo wa anachofundishwa mpe kazi nyingi za kufanya..
^^

Kim Ung Yong – 210 IQ

This South Korean has a tremendous capacity for both numbers and languages. He started speaking when he was only six months old. By the time he was three years old, he could read several languages already, including Korean, Japanese, German and English, as well as solve complex calculus problems. He also wrote poetry in Chinese and Korean and compiled enough essays and poems for two books. He was already auditing college courses when he was four. NASA then invited him to study in the U.S. when he was eight. By the time he was a teenager, he was already working for them. He then returned to Korea and switched fields from physics to civil engineering. He then published 90 papers about hydraulics.

Kongosho
 
Last edited by a moderator:
Kongosho... Kwakweli i did not experience anything of that sort. it was a walk in the park for me.
 
Last edited by a moderator:
Kwani lazima uone 'side effect' wewe mwenyewe? Unaowazunguka?

Saikolojia nzima ikoje, ugumu wowote ulioupata ku-cope na wenzio wa kidato cha kwanza?

Na labda kwa nini ulirushwa darasa? Kama hujatali ku share

Nilitaka kurushwa darasa. Dada yangu nae hakusoma darasa la saba na mie nikang'ang'ania.
 
Watu wa aina hii wako wangapi kwenye jamii?

Kim Ung Yong – 210 IQ

This South Korean has a tremendous capacity for both numbers and languages. He started speaking when he was only six months old. By the time he was three years old, he could read several languages already, including Korean, Japanese, German and English, as well as solve complex calculus problems. He also wrote poetry in Chinese and Korean and compiled enough essays and poems for two books. He was already auditing college courses when he was four. NASA then invited him to study in the U.S. when he was eight. By the time he was a teenager, he was already working for them. He then returned to Korea and switched fields from physics to civil engineering. He then published 90 papers about hydraulics.

Kongosho
 
Kim Ung Yong – 210 IQ

This South Korean has a tremendous capacity for both numbers and languages. He started speaking when he was only six months old. By the time he was three years old, he could read several languages already, including Korean, Japanese, German and English, as well as solve complex calculus problems. He also wrote poetry in Chinese and Korean and compiled enough essays and poems for two books. He was already auditing college courses when he was four. NASA then invited him to study in the U.S. when he was eight. By the time he was a teenager, he was already working for them. He then returned to Korea and switched fields from physics to civil engineering. He then published 90 papers about hydraulics.

Kongosho

^^
Tunao wangapi wa aina hiyo hapa Tanzania? Unadhani mazingira yanaruhusu wawe huru kuwa wawavyo?
Wakati fulani nilialikwa katika familia ya Mkuu wa wilaya moja hapa Tanzania (sitamtaja) wakati nimefika pale napata kinywaji,nilimwona mtoto wake wa mwisho about 5 years...isingekuchukua elimu ya digrii kujua ana IQ kubwa basi baba yake akamwita kwa lugha ya kiingereza ambayo mtoto alikuwa anaimudu vema kuliko hata lugha mama ya wazazi wake.."Hellow Alex come here!" Mtoto akamtazama baba yake juu hadi chini kisha akamjibu "..Daddy Can't you use a polite request?.."
Ndio ana akili,ndio anajua lugha pendwa,ndio yuko Medium school..Lakini hiyo ndiyo adabu kwa wazazi,je kama mzazi amejibu hivi mwajiri atamjibu vipi?
^^
 
Last edited by a moderator:
Kongosho,

Kati ya vitu ambavyo huwa nawalaumu sana wazazi au walimu wangu ni kutonirusha madarasa haswa yale ya shule ya msingi...

Nakumbuka wakati naandikishwa darasa la kwanza nilikuwa na uwezo wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu maana mama alinifunza kuanzia miaka miwili kabla ya kuanza shule...

Uwezo wa kuelewa na kuyakabili masomo nilikuwa nao, uwezo wa kutafuta mbinu mpya tofauti na zile za vitabuni nilikuwa nao mwisho wa siku shule nilikuwa naiona rahisi...

Binafsi sitasita kumrusha madarasa mwanangu au mtoto nimleaye if and only if he/she a wonder kiddo...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom