Kurusha Mtoto Darasa . . .

Kurusha Mtoto Darasa . . .

On ma side naona betta kumuwaisha kuanza shule i mean aanze darasa la kwanza akiwa na miaka mitano ili amalize primary xul akiwa na miaka kumi na miwili ila co kumrusha darasa

Mtot wangu alianza primary akiwa na miaka mitano,lakini kwa sababu alikuwa na uwezo mzuri darasani
alipoingia darasa la pili waalimu wake walishauri arushwe darasa yaani apelekwe la tatu,na pamoja na
kutosoma darasa la pili lakini alipoingia darasa la tatu aliendelea kushika namba moja mpaka ikatulazimu
tumtafutie shule ambayo wanafanya vizuri zaidi kitaifa akiwa la sita tukamhamisha,ni ile term ya kwanza
alishika namba sita,lakini mtihani uliofuata ameongoza mpaka amemaliza na kufanya mtihani last month.
Kiukweli sijaona madhara yoyote kwa mtoto kurushwa darasa nadhani inategemea na uwezo wa mtoto'
 
The Boss, Kongosho, mwekundu, watu8 na wengine mliochangia uzi huu. nawatahadharisha tu. nahisi huko mbeleni katika soko la ajira ili kushort list watu, waajiri wataanza kuomba vyeti vya darasa la saba kama wanavyofanya TAKUKURU.
darasa la cheti lazima afanye huwezi mrusha la 7 au form 4 au form 6 mkuu thats what i mean
 
Kuna dada mmoja nilizaliwa nae mwaka mmoja, mwezi moja, siku moja. Alikuwa family friend, mimi naanza darasa la kwanza yeye kaanzishwa darasa la tatu, alipomaliza akrushwa darasa la tano. mimi namaliza darasa la saba yeye ameshamaliza form four. Mi namaliza form six yeye anafanya kazi.
Nna mdogo wangu amezaliwa 2002, sahv yupo form three. Naona anaendelea vizuri tu bila shida. Sioni umuhimu wa kumwacha asome madarasa yote kwa kisingizio cha malezi.

HATA IKIWEZEKANA MWANANGU NTAMRUSHA HATA MADARASA YOTE YATAKAYOWEZEKANA.
 
darasa la cheti lazima afanye huwezi mrusha la 7 au form 4 au form 6 mkuu thats what i mean

Darasa la 7 wanarushwa kama kawa. Nani anahitaji darasa l 7 kwenye CV? Wakimaliza darasa la 6 hufanya mtihani wa kuingia K1. Wakifaulu imetoka hiyo. Na wengi hufaulu. Ni muhimu kuangalia upya mtaal wa elimu ya msingi. Inaonekana darasa la 7 mengi ni marudio ya darasa la 6.
 
Nitapitia michango mingine baadae (nina haraka kidogo)

Ila nachojua darasa la saba ni marudio tu; kama mwanao mzuri kichwani si mbaya kumrusha
 
Nimekumbuka mwalimu wa mwanangu alipotaka kumrusha mwanangu toka nursery kwenda primary (halikuwa wazo langu ni la mwalimu) alinambia mtoto mwenye akili uwa anakuwa bored kufundishwa vitu simple...ndio maana uwa wanajitahidi kuwatenga watoto tokana na uelewa wao
 
Back
Top Bottom