Kuruhusu Dowans wauze mitambo ni uhuni wa kisiasa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuruhusu Dowans wauze mitambo ni uhuni wa kisiasa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  dowans..jpg

  Habari kwamba mitambo ya kufulia umeme ya Dowans imeshauzwa kwa kampuni ya kigeni wakati sakata lao na Serikali ya Tanzania halijaisha ni habari za kukera, kuuddhi na zenye kukejeli uwezo wa Watanzania kusimamia maslahi yao. Kwa muda mrefu sasa tangu sataka la Richmond tumeweza kudokeza na kuonesha jinsi gani kampuni ya Dowans iliingia nchini kiulaghai na kufanikiwa kuchotewa mabilioni ya fedha za walipa kodi wa nchi yetu.

  Siyo hivyo hivyo tu tumeshuhudia katika muda huu wote ni jinsi gani Rais Kikwete na serikali yake wamekuwa dhaifu kama mbwa mbele ya chatu inapokuja kampuni ya Dowans kwa sababu ambazo sote tunazijua kuu ni kuwa mmiliki wa Dowans ni rafiki wa karibu wa Meneja wa kampeni ya Urais ya Kikwete 2005 Brig. General Al-Adawi wa UAE na alikuwa mfadhili wa mamilioni ya fedha wa kampeni hiyo.

  Tulionesha huko nyuma jinsi gani kampuni hii ya Dowans iliingizwa kinyemela na kupewa urithi wa mkataba tata wa Richmond ambayo kesi yake sasa imehamishiwa Dubai, UAE!! na jinsi gani serikali ilikuwa na kila haki ya kisheria kuichukua mitambo hiyo na kuitaifisha kama tu ingekuwa na ujasiri wa kuongoza.

  Matokeo yake kama watoto waliodekezwa serikali yetu ikaendelea kuremburiana machona Dowans hadi imefika mahali kuwa mitambo hiyo imeweza kuuzwa huku Waziri Ngeleja, Waziri Mkuu PInda, na Rais Kikwete wakiangalia wasijue la kufanya. Haya yote yamefanyika kwa sababu ya kiburi cha watu wachache, kiburi ambacho bila ya shaka kitaendelea kuligharimu taifa letu zaidi katika sekta hii ya nishati ya umeme.

  Hii imetuacha wapi?

  mitambo ya Dowans imeshauzwa kwa kampuni ambayo haitajwi (natabiri kuwa tutalazimika kununua umeme kutoka kwa kampuni hiyo mpya pindi wakianza mgao tena - muda si mrefu ujao); matokeo yake:

  a. Hata kama tukitaka kuikamata mitambo hiyo sasa hivi hatuwezi kwani siyo ya Dowans tena

  b. Kama tukitaka umeme tunaweza sasa kununua kwani tutakuwa tunanunua kutoka kwa kampuni nyingine na siyo Dowans.


  c. Fedha ambazo tumeshawalipa kwa kusafirisha mitambo.. Bil. 40 ndio zimeshaliwa na siyo Kikwete wala Ngeleja watakaozipigania zirudi.


  d. Kampuni ya Dowans itaanza mchakato muda si mrefu wa kufilisiwa na kutokomea nchini kama ilivyo kawaida ya kampuni za kitapeli.


  e. CCM wataomba kura tena wakiahidi kutatua tatizo la nishati na watanzania kama waliorogwa watawapa tena!!


  Kuna kila dalili kuwa Watanzania ni watu wa ajabu zaidi duniani kwani hawahusishi matatizo yao ya maisha ya kila siku na uongozi wa kisiasa uliopo madarakani. Wengi wao wanaamini yote yametokea
  kwa "mapenzi ya Mungu" na kwa "bahati mbaya" na hukesha wakiombea kuwa hali ije kugeuka kuwa nzuri.
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Na Zito Kabwe anatumia lugha ya kejeli eti "Tayari mitambo ya Dowans imekwishauzwa nje ya nchi. Katika hili wanaotakiwa kulaumiwa ni sisi wanasiasa na si vinginevyo kwa kuwa walipinga Tanesco kununua mitambo hii,".
  Hivi kahongwa shilingi ngapi?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa walikuwa wanatoa pendekezo moja tu la kununua mitambo lakini sijaona wakitoa pendekezo la kutaka Dowans irudishe fedha zetu walizopewa kusafirisha ambazo ni karibu theluthi mbili ya gharama za mitambo yenyewe! Kosa la wanasiasa ni kushindwa kuongoza kwa kutupendekezea suluhisho moja tu ambalo nalo ni kuwalipa Dowans licha ya ushahidi wote kuwa ni kampuni iliyoingia nchini kiulaghai na iliyotumia uongo kusajili.
   
 4. G

  Gobelagobela New Member

  #4
  Apr 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chai ya richmond/dowans ilikua ya moto sana sasa ishapoa wadanganyika washasahau.... jamani TRA vipi mmeshapata kodi ya capital gain toka ktk uuzwaji huo... au ndo tax exemption kwa wawekezaji?
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mambo yanayofanywa na viongozi, sorry watawala katika nchi yetu yanatia hasira sana. Ninashindwa kabisa kuelewa lengo lao nini na wanatafuta nini. Ukitafakari sana sio njaa, kwa sababu wameshajilimbikizia vya kutosha. Utakuta kuwa ni ulimbukeni, ubinafsi na upumbavu ndio sifa kuu za watawala wetu. Watu wanalishwa kwa kodi yetu, hivi kwa nini wasifanye mambo ya kututumikia tunaowalisha?
  Tazama wameshindwa kufanya jambo pale walipotarajiwa kufanya kitu, na sasa wanachekelea tu kuwa mitambo wameshauza. Natamani wote tupate hasira kwa mara moja na tuchukue uamuzi, CCM na makapi yake tuwanyofolee mbali kabisa.
   
 6. D

  Dotori JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilishaamua kuacha kushangaa
   
 7. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Mbele ya pesa, utu na mustakabali wa Taifa ni vitu vilivyopewa kisogo miaka mingi na viongozi wetu. Wako radhi kujinasibu kama "nyumba ndogo" za majangili wa kimataifa na mawakala (makuwadi) wao wa ndani almuradi watukoge kwa nyumba, magari, pamba, matanuzi na vinginevyo (petty assets) vya aina hiyo vitokanavyo na hongo wanazoambulia. Tukilalamika, basi wachovu siye tunawaonea gele, wivu na chuki kwa "mafanikio" yao kimaisha. Huo ndio ukomo wa fikra za kiongozi wa Tanzania leo. Na viongozi ni kielelezo cha jamii wanayoiongoza. Hivyo, tujiulize ni wapi tulipoteleza? kwa nini tunaendelea kurejesha uozo kwenye ngazi za uongozi wa nchi?
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa hatujari tena maslahi ya nchi mbele ya hawa wafadhili wa siasa zetu na tamaa zetu binafsi. Cha kutia moyo ni kuwa ni mtu mpumbavu tu atakayefikiri kuwa ni salama kwa kuendeleza mambo haya ya hujuma in this great propotions. Yatarudi bila huruma wala kuangalia sisi ni kina nani. Tubadilike maana tunajitafutia shida tuu kwa deal hizi za wizi na kifisadi.
   
 9. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaani unataka tuache kuiombea nchi yetu kisa mafisadi du! kwa taarifa yako tusingekuwa tunakesha na kuomba nchi hii ingekuwa imekufa fuatilia
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Apr 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  yeah.. tuendelee kuiombea tu.. itabadilika tu kwa miujiza tusifanye lolote..
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  MKJJ Kama ni kweli unashangazwa na unataka mabadiliko,basi nakushauri anza wewe ama tuanze sisi....Kwanza kabla ya kuwaambia wananchi whats wrong,tuanze kuangalia namna ya kuwaeleza whats wrong....

  Why am i saying this?

  Rejea heading yako kuwa hii issue ni "Uhuni wa kisiasa"

  MKJJ ukweli ni kwamba issue yoyote ile muhimu iwe ya kijamii ama kiuchumi na yenye maslahi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla,ukisha sema kuwa ni "Siasa" basi machoni pa wananchi wengi inakuwa ni issue ambayo wana option ya kutokuifuatilia kwasababu ni rahisi kuconclude kuwa "Haya ni mambo ya siasa"

  Si kila mtu anapenda siasa,lakini siasa iko kila mahali kwenye maisha ya mtanzania.....Hilo wananchi bado hawajui hilo bado kwasababu hawajui kuwa siasa ziko kwenye karibu kila maamuzi yanayoyaathiri maisha yao kwa namna moja ama nyingine!

  Hata hivyo yale mambo ambayo yameonekana kuwa na umuhimu kwenye maisha ya wananchi,wanasiasa hutumia mbinu ya kuwasahaulisha ama kuwapumbaza watanzania kwa kusema so and so ni mambo ya siasa na hivyo hayawahusu,na kimtizamo wananchi wengi hawachukulii siasa kama ni kitu serious hivyo kuwa rahisi kulaghaiwa na wanasiasa ambao wanatumia siasa kuomba kura,wanaongoza kisiasa lakini wakiwaambia wananchi wasijihusishe na siasa kwani hazitawaletea maendeleo....Watasema "msikalie politiki"

  Kwahiyo basi labda tuanze kwa kusema huu ni uhuni kwa maisha na uchumi wa mtanzania,uhuni ulioletwa kisiasa,na uhuni unaotumia siasa kuwaangamiza wananchi na uchumi wa Taifa lao!

  Tuanzie hapo?
   
 12. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hii nchi nashidwa kujua mwenye mamlaka ya mwisho ni nani? Ni kweli wameshauza kinachofuata watakuja kuong'oa mitambo and that is it! Dowans wanadaiwa hilo deni nani atalilipa! Halafu Zito unapolalama wa kulaumia ni wanasiasa ulitaka nini? Tuinunue! Tuizuie isuzwe? ama walipe deni? Manake kinachofanyika Richomond waliiba pesa ya serikali wakaleta mitambo, walipogunduliwa wanataka kutuuzia!! Huu si upuuzi kabisa
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  halafu unaambiwa eti kesi ya dowans kusikilizwa Dubai, hivi kweli tanzaniakama nchi bado ipo? kwani kosa na mkataba ulifungwa dubai?
   
 14. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  du mkiandika kuzeni basi hizo silabi tuzione
   
 15. T

  Tom JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  'mafisadi tu', naona hujajua ufisadi kua ndio tatizo kuu. Sasa kama huko unakoomba wamekupa na uwezo wa kufanya kazi ili ule, na kwa nini usifanye kazi pia ya kuwaondoa mafisadi wanachukua chako. Huwezi kuombea ati upate chakula bila kufanya kazi, vile vile huwezi ombea nchi mambo mema wakati wanaoihujumu unawaona si kitu na unawaacha waendelee na uharamia wao.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  siyo tu unawaacha waendelee na uharamia.. unawaombea kwa Mungu wabarikiwe!
   
 17. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,897
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Nafikiri hii statement ni ya kweli kabisa. Ukitafakari hizi habari za dowans na richmond ni wazi kwamba Watanzania ni watu wa ajabu.
   
 18. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sehemu pekee iliyobaki kwa Watanzania kudai haki zao ni kwa kutumia kura zao vizuri katika uchaguzi mkuu unaokuja,kuchagua viongozi wanaojali maslahi yao wananchi na si wabinafsi na waroho wa kujilimbikizia mali.Mungu wape roho ya uzalendo Watanzania katika uchaguzi mkuu ujao.
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unapoomba siyo kwamba unataka miujiza kwani miujiza ni maamuzi ya Mungu na Mungu pekee. Sisi tunaomba kwa Mungu ili atupe nguvu, busara na hekima. Sasa kama wao wanatumia shetani kufanikisha mambvo yao, sasa sisi tutaendaje kichwa kichwa? Mkuu inabidi ukubari tu kuwa hata hizo nguvu unazotumia katika kutoa michango hapa JF zisinge kuwapo kama sio kwa maombi ya Watanzania, shetani angekuwa ameshakupa doze long time ili washikaji wake watanue si unajua tena hiki ndiyo kipindi cha kumwaga damu?
   
 20. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hawa utafikiri wapo sayari nyingine tofauti kabisa na tuliyopo sisi. Jamaa wameona Rais hafanyi lolote dhidi ya mafisadi, wameamua kumuondoa madarakani. Watanzania hatuwezi kujikomboa mikononi mwa CCM hivi hivi. Kumbuka CCM haiwezi kubadilika. Hata CCJ haiwezi, kitakachofanyika ni kuipa kashi kashi kama ilivyokuwa 1995 lakini si kushinda kwani CCM ina dola, NEC nk.

  CCM itaondoka kwa kulazimishwa tu, kulazimishwa kutakakofanywa na wananchi waliojitolea, waliotayari kufanya kile Steve Biko (cry my country) alikifanya South Africa... to confront... vinginevyo uhuru wetu upo mbali kama miaka 25 ijayo.
   
Loading...