Kurudishwa kwenye Government Payroll

Watu wanakula hela na wewe ni miongoni mwa wafanyakazi hewa,
 
wanajadili watu kama sisi waweze kutuajili ambao hatukuripoti
 
Asante,na hongera kwa kujielewa kijana
 
Hoja ya msingi ulipoajiriwa mara ya kwanza vyeti vya elimu, fomu ya maelezo binafsi uliyojaza na barua ya ajira viliwekwa kwenye Lawson. Unatakiwa kuomba kwanza kibali kwa Chief Secretary ukieleza na mazingira ya kuacha yakiwa na uhalali itakuwa nafuu kwako. Vinginevyo omba ajira kwenye Taasisi nyingine ambazo haziko katika Lawson mfano TANAPA, TANESCO na NHC. Kifupi Lawson inalenga kuwa na labour stability Serikalini ili wafanyakazi wasiache na kurudi at their will.
 
Mie binafsi imenikuta Iyo niliondoka kazin Ila Jamaa hawakuniondoa kwenye payroll sasa nmepata ajira sehem nyngne nikaambiwa nikahamishe data sang nna mpka barua ya katibu mkuu,Ila Hr was Iyo halmashaur ameniondoa kwenye payroll
 
Aisee kiukweli kama ushawahi ajiriwa na ukapata cheque namba ni kazi kurudi serikalini...

System ya LAWSON ni noma...njia pekee ni kuomba kibali kwa katibu mkuu kiongozi ili akuruhusu kuajiriwa upya ila na hiyo inachukua muda....Mimi nilikiomba April 2014 akanipa December 2015...process imefanyika na nikaingia payroll June mwaka huu...Ile naingia tu JPM akasitisha ajira mpya na mimi malipo ya salary yakasitishwa nipo nasikilizia...
 
Unaweza kupata nafasi lakini tatizo linakuja wanapotuma jina hazina kwa ajili ya malipo system inaonyesha mtu huyo alishaajiriwa
Yawezekana kuwa inaonesha na mshahara analipwa?!
 
Mmesha haribu,
 
Ulifanikiwa ama?tupe mrejesho mana jamaa angu ana tatizo kama lako na wamemwambia aende tamisemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…