Kurudia Uchaguzi Zanzibar, CUF watoa tamko

Kurudia Uchaguzi Zanzibar, CUF watoa tamko

Ccm wamemwaga ugali bado cuf na ukawa kumwaga mboga, kama noma na iwe noma, liwalo na liwe tunasubiri maamuzi ya vikao
 
Kama kweli aliyeandika ni Jussa, basi kaandika kwa hasira sana. Apunguze jazba hawa wetu, roho tu ya Mungu.
 
Nina hamu ya kuona CUF wakisusa. Amani Karume alifanya kosa sana kuunda serikali ya mseto
 
Wacha moto uwake,naifuatilia kwa karibu hii Series. CUF nawaaminia sana katika maamuzi na misimamo yao.
acheni kuwadanganya wenzenu. hao wanaosema moto uwake watoto wao wote wapo ulaya na uarabuni na wake zao na ndugu zao wengi. wataowashwa na moto ni familia za wote waliopo hapa na ambao wataangamia. nashauri kabla moto haujawashwa waagize familia zao zote zitoke huko nje na wawe mstari wa mbele katika mapambano. ili kila mtu aathirike kwenye familia! hatutaki ujinga. msikae kutishatisha watu hovyo. tena nasema atakayeongoza uwashaji wa moto huyohuyo awe wa kwanza na yeye kuwashwa moto, maana atakuwa amechoka kuishi duniani
 
Ama kweli busara imetumika kubwa sana Maalim Seif na wenzake ,dunia imeona ulivyokua ukihangaika kuitafuta amani ,kwa tamko hili kama kweli ni Jusa kalitoa basi kuna kila dalili za kuonyesha uvumilivu umeanza kuwashinda ,na hakika hatima ya Zanzibar iwe mbaya au nzuri itakua juu ya vizazi vyenu watawala
 
Wakati mwingine hata sielewe.CUF kwanini hawakutuma wajumbe wenye nguvu na hoja wamsaidie maalim kwenye vikao vya usuluhishi?
Nilisema kuna kajambo hapa.
Kinachofuatia ni uchaguzi kurudiwa,CUF kugoma,CCM na vyama vingine vidooogo vitafanya uchaguzi na mtasikia CCM imeshinda kwa kishindo.
Maalim nadhani unalijua hilo na inawezekana ndio matokeo ya vikao vyenu hivyo.

Naichukia sana siasa
 
Ama kweli busara imetumika kubwa sana Maalim Seif na wenzake ,dunia imeona ulivyokua ukihangaika kuitafuta amani ,kwa tamko hili kama kweli ni Jusa kalitoa basi kuna kila dalili za kuonyesha uvumilivu umeanza kuwashinda ,na hakika hatima ya Zanzibar iwe mbaya au nzuri itakua juu ya vizazi vyenu watawala
KAKA MAMBO YATAKWISHA MACHI 20 UCHAGUZI UTAAMUA MSHINDI HALALI. HAKUNA VURUGU WALA NINI!
 
Ishu ya Zanziba kila nikitaka kuchangia moyo unaenda mbio......sijui kwa nini.
 
KAKA MAMBO YATAKWISHA MACHI 20 UCHAGUZI UTAAMUA MSHINDI HALALI. HAKUNA VURUGU WALA NINI!
Kama hilo ndio mmeona ni suluhisho la tatizo la Zanzibar sawa ila hakika hatma ya Zanzibar iwe mbaya au nzuri itakua juu ya vizazi vyenu
Mimi nimemaliza mkuu
 
Hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo dhuluma iliwahi kushinda haki .
 
Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
Tupo pamoja na uongozi wa cuf ktk kufikia maamuzi
 
Back
Top Bottom