Kurudia Uchaguzi Zanzibar, CUF watoa tamko

Kurudia Uchaguzi Zanzibar, CUF watoa tamko

Huo uchaguz utakua wa Rais peke yake au na wawakilishi??,,,,kwann wao wasiendelee kutawala wasiwachoshe wananchi.huku walishasema nchi ya kimapinduz haitwaliwi kwa karatasi.



CUF wanasema kurudia haina shida,,,tatizo lipo pale ni la kisheria,,,wanahoji mamlaka hayo mwenyekiti kapata wap?? Wakikubali maana siku zijazo utakua ndio utamaduni,,,wnaopenda uchaguz urudiwe waseme kwa sheria #fulan inaruhusu kufutwa kwa uchaguz hii kweli ajab had uchaguz wa wawakilishi kuna wengine walishinda na walipewa certificate na kutangazwa mwenye mamlaka ya kutengua hua ni mahakama baada ya mpinzani kushtaki.

Utaratib huu haufai hata kidogo marudio hayo ni batili.
 
Wacha moto uwake,naifuatilia kwa karibu hii Series. CUF nawaaminia sana katika maamuzi na misimamo yao.
Labda kama una miaka 20,mambo hayo yapo tokea 95 na maisha yaliendelea,fanya kazi badala ya kusubiri moto uwake
 
Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
Uchaguzi ni wa Zanzibar, kwa nini mkutano usifanyike huko huko? Hii ni janja ya nyani jusa kufanya mkutano bandari ya salama Dar halafu wachochee waliopo Zanzibar waandamane, wapigwe yeye Jusa apunge upepo Starlight hotel! Very clever jusa!
 
Kama wana uhakika walishinda sasa tatizo liko wapi? Uchaguzi urudiwe na tumalizane na hii movie.
Kwanini tupoteze fedha za walipa kodi na mda kwa madai ya CCm ambayo hadi hii leo wameshindwa kuleta ushahidi au kwakuwa Jecha chama chake kimeshindwa warejee uchaguzi ili waibe kura
 
Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO

Tunaelewa tosha kuwa sababu ya kurejea uchaguzi ili CCM waibe kura na waseme wameshinda ushindi wa kishindo.
Sasa suali langu je CCM mkishindwa kuiba kura na mkashindwa tena mtafuta tena Uchaguzi na kurejea?
 
Hivi mpaka nchi ifikie hatua gani ndio united nations iingilie kati .hizi jumuia za kimataifa mpaka watu wauane ndio utakuta zinajifanya ku wakeup .huyu jecha na wengine kama kumi tu kule zanzibar waanze kuwekea international sunctions .then wapelekwe the hague
 
Back
Top Bottom