Kurudi kwa UDA (daladala) hii maana yake nini?

Na Mimi Jana nilikuwa pale posta mpya nimeziona UDA kama NNE zimefufuliwa nikashangaa "kwanini sasa?!"

Niliidhani mshangao huu ninao peke angu kumbe hili tumeliona wengi!
wanakwambia eti mwenye UDA kapokea KIKOBA kwahyo ndo mana kaenda fata mzigo mpya,kikoba chake Kijumbe alikua Magu
 
kwanza mkuu uelewe UDA inamilikiwa na serikali asilimia 100 rejea report ya CAG ukaguzi maalum 2018/2019 na maana ya UDA ni usafiri dar es salaam tukija upande wa UDART Ni usafiri dar es salaam rapid transit ni kampuni tanzu ya UDA ila inamilikiwa na serikali asilimia 85 huku kampuni nyingne ikimiliki 15 zinazobaki
sasa kama ni ya serikali imekuaje aivyoingia JPM uda zikapotea,ina maana aliamua zipoteza kwa manufaa ya nani wakati ile ni mali ya uma? (kama unavyodai)
 
Nimalizie kwa kusema "Anaye stream youtube sasa hivi ni kidume", Ukimuona mtu yuko Online Muheshimu, Ma group yangu sioni cha admin wala member anatuma tuma vi meme leo ni kimyaaaaaa, WAZIRI WA NCHI MWANACHAMA WA DATA amejua kututembelea huu mwaka, halafu ndio kwanza April 2..
😂😂😂😂😂
 
ingekua kuboresha usafiri, Daladala zisingekatazwa kwenda k.koo,kitendo cha kuzuia daladala wakati wanajua uwezo wa kumudu usafiri hawawezi huko ni kuua na kudhohofisha usafiri.
Solution sio daladala bali ilikuwa kuongeza mabasi ya BRT na wawe na ratiba zisizoyumba!! Kuboresha ilikuwa na lengo la kuwafanya watu wawahi kufika wanakoenda, na daladala hazitaweza kufanikisha hilo la kuwahisha abiria kwa sababu zingetumia barabara (za kawaida) zinazotumia magari mengine na hivyo kuathirika na msongamano!!!
 
Mkuu sio kwamba yanaegeshwa kwa wema
Ni ubovu
Tunaweza kusema "kwa wema" kwa sababu, kwa utaratibu waliojiwekea, ikifika mchana baadhi ya magari yanaegeshwa na yanaanza tena route jioni. Kwahiyo, kama ni wema, ndo huo hapo lakini sio kwamba yanakuwa mabovu! Kwa tafsiri nyingine, HAWATAKI kuendesha magari yao yakiwa level seat, bali wanataka wakati ambapo watu watakuwa wamerundikana, hata kupumua hawawezi! Sasa matokeo yake, wakati wanaamini mchana abiria sio wengi, kinachotokea ni kuwafanya abiria warundikane vituoni kusubiria yale yaliyo barabarani!
 
Ama kwa hakika tumerudi tulikotoka kwa speed ya 5G, mimi naomba tu Mungu asaidie Miradi iliyoanzishwa walau imaliziwe tu jamani kisha ndio waendeleee kuzila hela zao maana hii nchi ina wenyewe.
Ina maana kuna mtu ameshika remote anatuhamishia stesheni anazopenda yeye
 
ingekua kuboresha usafiri, Daladala zisingekatazwa kwenda k.koo,kitendo cha kuzuia daladala wakati wanajua uwezo wa kumudu usafiri hawawezi huko ni kuua na kudhohofisha usafiri.
Sasa kama hukatazi, kulikuwa na sababu gani tena ya kutumia mabilioni ya shilingi kuanzisha Rapid Bus Transport?! Usisahau tatizo la Daladala sio Daladala per se, bali mfumo unaotumika! Barabara nyembamba, maelefu ya magari barabarani, matokeo yake, mtu unatumia saa 1+ kutoka Kimara hadi Kivukoni!!!

Kupitia BRT, nina uhakika mmoja safari yake ianzie Kimara kwa kutumia BRT, na mwingine safari yake ianzie Ubungo kwa kutumia daladala, na wote watoke at the same time during peak hours!!! Huyu wa Kimara atawahi kufika mjini kabla ya yule wa Ubungo! Ukifahamu hilo ndo utagundua solution sio kuruhusu daladala bali kuongeza magari ya BRT na yawe yanatoka kwa muda!!
 
sasa kama ni ya serikali imekuaje aivyoingia JPM uda zikapotea,ina maana aliamua zipoteza kwa manufaa ya nani wakati ile ni mali ya uma? (kama unavyodai)
Mkuu kumbe inaelekea huifahamu vizuri BRT! UDA na Mwendokasi ni kitu kile kile; hawa ni ndugu wa Baba mmoja, mama mmoja! Hivi huoni hata magari yao (ya mwendokasi) yameandikwa UDART? Yaani UDA Rapid Transport.
 
Si kweli samia ataongoza hii minne iliyobaki then atapata fursa moja tu 2025 hadi 2030 akimaliza kwisha katiba haimruhusu! Katiba inasema kama rais atafariki au kujiuzulu na huku kabakisha miaka mitatu ya utawala wake basi makamu wa rais ataongoza nchi miaka hiyo mitatu na pia atakuwa na fursa ya kugombea vipindi viwili vya miaka mitano mitano,
ila rais akifariki au kujiuzulu ikawa imebaki miaka minne au zaidi inahesabika ni awamu moja nzima hivyo makamu wa rais atapewa fursa moja tu ya kugombea tena.
sasa hivi imeongezeka imekua 14,tunamalizia mi 4 iliyobaki halafu tunapiga 10 mingine,msipohama Nchi nyie vidume
 
Mkuu kumbe inaelekea huifahamu vizuri BRT! UDA na Mwendokasi ni kitu kile kile; hawa ni ndugu wa Baba mmoja, mama mmoja! Hivi huoni hata magari yao (ya mwendokasi) yameandikwa UDART? Yaani UDA Rapid Transport.
UDA ni mradi wa serikali uliobuniwa na kigogo flani (asiegusika ila magu alimgusa) hela zikawa zinaenda kwake na sio kurudi ktk maendeleo ya nchi.

UDART
ni mradi wa serikali ulioendeleza UDA lakini UDART hela zinarudi serikalini na zinafanya maendeleo ktk nchi

nadhani sasa umeelewa UDA na UDART zimetofautiana wapi na kwanini tunashangaa UDA kurudi kipindi hiki na si kipindi cha uhai wa JPM. (nyundo)
 
UDA ni mradi wa serikali uliobuniwa na kigogo flani (asiegusika ila magu alimgusa) hela zikawa zinaenda kwake na sio kurudi ktk maendeleo ya nchi.

UDART ni mradi wa serikali ulioendeleza UDA lakini UDART hela zinarudi serikalini na zinafanya maendeleo ktk nchi

nadhani sasa umeelewa UDA na UDART zimetofautiana wapi na kwanini tunashangaa UDA kurudi kipindi hiki na si kipindi cha uhai wa JPM. (nyundo)
Unanielewesha mimi wakati mimi ndie nimetangulia kukuelimisha wewe kwamba UDA na UDART ni baba mmoja, mama mmoja!! Inavyoelekea unadhani UDART ni exclusively kampuni ya serikali, kumbe umiliki wa serikali kwa UDA na UDART ni wa aina ile ile!!!

Nilichogundua umeleta mada kumpamba JPM huku ukiwa huna taarifa za kutosha! UDA ipo tangu enzi za Nyerere, na kutokana na kubinafsisha mashrika ya umma, serikali ndo wakabaki na 49% stake halafu unasema "mradi uliobuniwa na kigogo fulani"! Btw, huyo Kigogo aliyeguswa na JPM ni yupi? Ukweli mchungu kwa watetezi wa JPM ni kwamba, Magu HAJAWAHI kumgusa Kigogo yeyote hadi umauti unamkuta, unless kama Robert Kisena ndo unataka kuwaambia watu kwamba ndie Kigogo!! Magu huyu huyu aliyekuwa anaishia kuongea kwa mafumbo kwamba "kule Lindi kuna mtu katafuna 20Billion" bila kutaka jina, ndo useme "kamgusa kigogo asiyegusika"!

Lakini kwa upande mwingine, sijui nani alikudanganya kwamba wakati wa Magu UDA haikutakiwa kutoa huduma! Sasa unaipiga vipi nyundo kampuni ambayo serikali na yenyewe ina hisa zake?! Unaizuia kwa faida ya nani?
 
Mwendokasi ina pata faida sasa kwasababu ya "marufuku" ya magari ya kawaida kwenda Kariakoo to Mbezi ila Uda Ikianzisha ruti za K.koo to Mbezi Mwendokasi wameumia.
Biashara ya dala dala hainaga hasara kama usimamizi uko vizuri mkuu
 
Hii kweli ni yajayo yanahuzunisha maana watu ni watajichotea Awamu hii yani miaka mi 4 hiii naamini nitaanza okota vi hela barabarani maana nina muda sana sikuwahi okota hela, Pesa ndio inarudi kwa wananchi ama kwa hakika nimeona sasa.
Mkuu naomba ukipata muda uniulizie budget ya msiba ilikuwaje.
 
Na kwa kurudi kwa UDA ndio JIPU litaendelea kukwiva maana naona kabisa namna ambavyo UDA wataanzisha ruti za K.koo - Mbezi na hakuna trafik ataeuliza wala kuzikamata hizo dala dala, hatima ya MWENDOKASI siijui ni ipi kwakweli
Mwendokasi ni Mashetani kabisa wale.
Inashangaza kuona una huruma nao washenzi wale.
Hao UDA wakianzisha ruti ya Mbezi -Kkoo nitawaombea waishi maisha marefu, maana watakuwa wakombozi Wa wanyonge wanaoteswa na Mashetani yanayojiita UDART..
 
Back
Top Bottom