Kurudi kwa UDA (daladala) hii maana yake nini?

Hivi Robert Kisena na mkewe walishatoka ndani kweli? Maana walipigwa uhujumu uchumi. Yani bwana yule alikuwa akiona hana hela anakamata mtu anamkamua hela zake anamuachia dah. Wacha warudi maana nawadai pesa yangu nyingi niliamua kuacha kudai kulingana na hali halisi Ila mama ayurudishe kwenye nchi ya kazi na dawa hata bendi zitarudi maana watu wazima hata pa kwenda weekend hakina. Unaishia kwenye vi-pub tu mara 99 au sijui busca la vida ujana mwingi band hakina.
 
Mi ni mpandaji mzuri sana wa daladala hasa ruti za mbagala na Gongo la mboto na mahali napofanyia kazi ni rahisi sana kuona magari yanayopita barabara ya bagamoyo, ni muda mrefu sana sijaona magari ya UDA hivyo ukiniambia umeyaona sasa ni kweli yatakuwa yamerejea, lakini mtu akiniambia yaoikuwepo yanaendelea na kazi hilo nakataa nayajua magariya UDA kwa muda mrefu na rangi zake sijayaona barabarani for 2-3 years
Simon group inajulikana ya Nani, na jamaa na mkewe watatolewa gerezani soon.
Mr tabassmu kesharudi mjini

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Yalikuwepo zamani ila hayakua Mapya, Haya mapya yametokea wapi?
Kwani magari mapya huwa yanatoka wapi? Mbona swali lako hakina mantiki? Kwa hiyo Kama hawakuweka magari mapya wakati wa JPM, wakiweka Sasa Kuna kosa lolote linakuwa limetendeka?
 
Mwendokasi ina pata faida sasa kwasababu ya "marufuku" ya magari ya kawaida kwenda Kariakoo to Mbezi ila Uda Ikianzisha ruti za K.koo to Mbezi Mwendokasi wameumia.
Na tusisahau, lengo la Mwendokasi halikuwa kuua biashara ya daladala bali kuboresha usafiri Dar es salaam ili watu wawahi waendako! Lakini mara kwa mara yametokea malalamiko kwamba kuna uhaba mkubwa wa mabasi ya mwendokasi, na ujinga zaidi, unakuta mahali yamepaki wakati watu wamejazana vituoni!
 
Mm naomba warud tu, hawa mwendokas wanatukalisha vituoni kama watumwa afu gari linakuja moja mnagombania kama kuku wakat mengine yamepak tuu sjui wanatuonaje.
 
Nijuavyo Mimi baada ya muda wa Hayati JPM kuingia biashara nyingi zilifungwa. Mtakubaliana namimi magari/daladala nyingi nzur zikiondoka barabarani, nk nk mabiashara kufungwa...juzi Malkia Mh samiya akasema ni kisa kuwafukuza wafanyabiashara...

Tuanzie hapo kuonekana UDA si ajabu ameamua kurejea, swali ni riz au nani ni Kuu yao... Mzee mkapa wakati flan alizomewa maeneo ya bamaga...kea kuitwa Li thief ....Li thief... Hiloo....

Haikuwa poa sasa wenye macho ...wenye masikio...dunia tutaiacha
 
Na tusisahau, lengo la Mwendokasi halikuwa kuua biashara ya daladala bali kuboresha usafiri Dar es salaam ili watu wawahi waendako! Lakini mara kwa mara yametokea malalamiko kwamba kuna uhaba mkubwa wa mabasi ya mwendokasi, na ujinga zaidi, unakuta mahali yamepaki wakati watu wamejazana vituoni!
Mkuu sio kwamba yanaegeshwa kwa wema
Ni ubovu
 
Mwendokasi ina pata faida sasa kwasababu ya "marufuku" ya magari ya kawaida kwenda Kariakoo to Mbezi ila Uda Ikianzisha ruti za K.koo to Mbezi Mwendokasi wameumia.
Dar ni Jiji walikua hawana sababu ya kuzuia waliache soko huria ubora wa kila eneo ungeweka nafuu na kupunguza changamoto za kugombania usafiri na kutanua wigo wa ajira zisizo rasmi
 
Mwendokasi ina pata faida sasa kwasababu ya "marufuku" ya magari ya kawaida kwenda Kariakoo to Mbezi ila Uda Ikianzisha ruti za K.koo to Mbezi Mwendokasi wameumia.
Mwendokasi inamilikiwa na UDA,ndiyo maana kampuni hiyo ya mwendokasi inaitwa UDART.
 
Haya mabasi/daladala za UDA yalianza onekana kwa wingi sana kipindi cha uongozi wa Awamu ya 4 ila baada ya kuingia awamu ya 5 hizi daladala zilipotea zote moja baada ya nyingine na mwisho hatukuziona tena barabarani.

Tangu msiba uishe wa Aliyekuwa Rais awamu ya 5 Rais Magufuli UDA zimeanza kurudi barabarani, nimeshashuhudia UDA 3 mpya ruti ya MBEZI - MBAGALA/3, MBEZI-BUGURUNI, MBEZI-TEMEKE nk

Swali langu ni la mshangao, imekuaje tena haya magari kurudi wakati huuu? Yalikua wapi? Boss wake ni nani? Kwanini alikuwa hayarudishi barabarani kipindi cha uhai wa Magufuli na kwanini kayarudisha sasa hivi?

"Watanzania sisi sio wajinga, Tunaona"

Nimalizie kwa kusema "Anaye stream youtube sasa hivi ni kidume", Ukimuona mtu yuko Online Muheshimu, Ma group yangu sioni cha admin wala member anatuma tuma vi meme leo ni kimyaaaaaa, WAZIRI WA NCHI MWANACHAMA WA DATA amejua kututembelea huu mwaka, halafu ndio kwanza April 2..
Afu nauli jelo tu, na 150 inabaki
 
Na Mimi Jana nilikuwa pale posta mpya nimeziona UDA kama NNE zimefufuliwa nikashangaa "kwanini sasa?!"

Niliidhani mshangao huu ninao peke angu kumbe hili tumeliona wengi!
 
Back
Top Bottom