Kurudi kwa Lowassa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,041
2,000
Dalili zote zinaoonesha kuwa kilio cha wabunge kutaka Pinda ajiuzulu na hivyo Baraza la Mawaziri livunjike lina dalili moja kubwa; Lowassa's comeback. Sidhani kama kuna mwanasiasa mwingine yeyote ambaye anaweza kupata kuungwa mkono na wabunge wa CCM kama Lowassa. Kurudi kwake itakuwa ni kupata second chance na kujipanga vilivyo kwa ajili ya 2015. Kama siyo Lowassa ni mbunge gani mwingine wa CCM kutoka majimbo ya kuchaguliwa anayeweza kupata support na heshima ya kuwa Waziri Mkuu? Haitakuwa mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu kurudia kiti chake mara ya pili.

Yetu macho.
 

Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Kinachoendelea bungeni ni maigizo tu ya CCM kwa krosi za kupasiwa wapinzani kwani ni planned strategy ya kuingiza watu fulani kwenye baraza la mawaziri akiwemo Migiro.

Kikwete hakwenda Marekani kwa dharura na pia tujiulize kwa nini kila sekeseke za bungeni zikitokea Kikwete anakuwa nje? Is it a merely coincidence??! Watanzania tuamke na kukataa upumbavu wa kisanii na kizandiki!
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,794
2,000
ccm can no longer help this country...ni kweli tunakua sympathetic kwa LOWASA kwamba NI JUMBA BOVU TU LILIMDONDOKEA...
Hivyo basi LOWASA KUREJEA NI KWAMBA CCM HAWANA SUB.
KUREJEA MATAPISHI.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,560
2,000
JK akikubali Lowassa kuwa PM tena atajionesha kwamba yuko weak kuliko vipimo vyote vya weakness vinavyoweza kupima.

Lowassa anaweza kuwa rais anayefuata. Umpende, usimpende, anaongelewa kama a serious contender. Lakini hana nafasi ya kuwa PM tena katika kipindi hiki. Kitakuwa ni kichekesho kikubwa.

Hata yeye mwenyewe, aliyejitoa u PM kwa sababu ya kuondoa mzozo akikubali kuwa PM tena ataonekana si tu hana msimamo, bali pia mroho wa madaraka asiye mahesabu ya kujua kwamba wa Tanzania wanamuheshimu sana rais na makosa yote ya uongozi anayabeba PM.

Lowassa ana chances za kuwa rais, kwa nini aharibu chances hizo kwa kurudi kuwa PM? Kazi yenye majukumu yenye majungu na mikingamo ya aina yote?

Kwa kutumia hesabu hizo hizo za kutoka kwenye limelight ili kujiepusha na habari za mikingamo na majungu ndiyo maana hata mtu kama Hilary Clinton, ambaye anaonekana anautaka urais wa Marekani na ana nafasi kubwa kuuwania, akaamua kukaa pembeni, hizi rabsha rabhsa mara Benghazigate mara nini sijui akaona zinampunguzia umaarufu.

Lowassa would do well to stay a backbencher for now if he is to look consistent, dignified and free of a wanton greed for power.

But then again that is just my logical analysis.

Who said Tanzanian politics is logical and subject to analysis?

Na Pinda kuondolewa pale ni kazi. Tanzania PM mzembe anaweza kupeta kwa sababu rahisi kama "tuna mawaziri wakuu wastaafu wengi - Msuya,Salim, Warioba, Malecela and even Lowassa fiscally is supported as a retired PM- tukiongeza itakuwa mzigo mkubwa kwa serikali".

Especially because the Kikwete administration has only about two years to go anyway.

And Kikwete's philosophy is "yatapita na upepo haya tu".
 

Sawana

Senior Member
Dec 19, 2013
130
0
Kuna wa-tz more than 45 million, why we should recycle wazee na walioshindwa akina Lowasa. Nipeni hiyo kazi halafu mtaona shughuli
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,794
2,000
jk akikubali lowassa kuwa pm tena atajionesha kwamba yuko weak kuliko vipimo vyote vya weakness vinavyoweza kupima.

Lowassa anaweza kuwa rais anayefuata. Umpende, usimpende, anaongelewa kama a serious contender. Lakini hana nafasi ya kuwa pm tena katika kipindi hiki. Kitakuwa ni kichekesho kikubwa.

Hata yeye mwenyewe, aliyejitoa u pm kwa sababu ya kuondoa mzozo akikubali kuwa pm tena ataonekana si tu hana msimamo, bali pia mroho wa madaraka asiye mahesabu ya kujua kwamba wa tanzania wanamuheshimu sana rais na makosa yote ya uongozi anayabeba pm.

Lowassa ana chances za kuwa rais, kwa nini aharibu chances hizo kwa kurudi kuwa pm? Kazi yenye majukumu yenye majungu na mikingamo ya aina yote?

Kwa kutumia hesabu hizo hizo za kutoka kwenye limelight ili kujiepusha na habari za mikingamo na majungu ndiyo maana hata mtu kama hilary clinton, ambaye anaonekana anautaka urais wa marekani na ana nafasi kubwa kuuwania, akaamua kukaa pembeni, hizi rabsha rabhsa mara benghazigate mara nini sijui akaona zinampunguzia umaarufu.

Lowassa would do well to stay a backbencher for now if he is to look consistent, dignified and free of a wanton greed for power.

But then again that is just my logical analysis.

Who said tanzanian politics is logical and subject to analysis?

Na pinda kuondolewa pale ni kazi. Tanzania pm mzembe anaweza kupeta kwa sababu rahisi kama "tuna mawaziri wakuu wastaafu wengi, tukiongeza itakuwa mzigo mkubwa kwa serikali".

Especially because the kikwete administration has only about two years to go anyway.

And kikwete's philosophy is "yatapita na upepo haya tu".

..tuweke siasa pembeni...
Ccm hawawezi kuwa na jipya.. Hata akija nabii 2015....
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,951
2,000
Dalili zote zinaoonesha kuwa kilio cha wabunge kutaka Pinda ajiuzulu na hivyo Baraza la Mawaziri livunjike lina dalili moja kubwa; Lowassa's comeback. Sidhani kama kuna mwanasiasa mwingine yeyote ambaye anaweza kupata kuungwa mkono na wabunge wa CCM kama Lowassa. Kurudi kwake itakuwa ni kupata second chance na kujipanga vilivyo kwa ajili ya 2015. Kama siyo Lowassa ni mbunge gani mwingine wa CCM kutoka majimbo ya kuchaguliwa anayeweza kupata support na heshima ya kuwa Waziri Mkuu? Haitakuwa mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu kurudia kiti chake mara ya pili.

Yetu macho.
Mhh, nimejiuliza sana hivi tumefikia mahali wabunge wa CCM wana uchungu na taifa hili kiasi cha kutaka waziri mkuu aondolewe? Then nikajiuliza hivi hakuna 'msukumo' kutoka sehemu nyingine ili kufagia njia?

Kurudi kwa PM waliopita hakukuwa na kashfa. Sokoine alirudi baada ya kutoka masomoni ilikosemwa alikuwa kwa matibabu. Msuya alirudi kwasababu alikuwa ni 'kiraka' pale ilipohitajiwa. Wote hawakuondolewa kwa kashfa bali kubadilishwa kwasababu tu ya kupanga safu.

EL ni kashfa ambayo inaunguruma hata kama inapuliziwa utuli wa kutosha.
Ningefurahi sana akirudi maana huo ndio ungekuwa mwisho wake.
Mahasimu wake watafunua bandeji za vidonda vyote !!!
 

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
1,195
Ni aibu na fedheha ya aina gani kwa Serikali yenye wabungezaidi ya 150 wa kuchaguliwa na wananchi miongoni mwao wakiwa ni ma-DR. na ma-PROF. bado ishindikane kumpata mmoja miongoni mwao wa kuwaongoza wenzake kama PM. Serikali ya aina hiyo itakuwa ilijitwalia na kujisimika yenyewe kwenye madaraka kwa namna inavyojua pasipo ridhaa ya wananchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom