Kurudi Clouds Fm; Masudi Kipanya ajigamba, ni pesa tu!

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Masoud Kipanya amerejea tena Clouds FM baada ya kupita muda mrefu takribani miaka minane tangu aondoke. Mchoraji huyo maarufu wa katuni ya Kipanya, anasikika kwenye kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast.

IMG_7231.jpg

Akizungumzia kurudi kwake, Masudi anasema, “Sijui kama unajua kuwa mimi Clouds nilifukuzagwa kazi! Msingi wa kutoka Clouds ni kwamba sikutoka kwasababu nilikuwa labda niko hivi hapana, tulikuwa tunafanya kazi zetu kama kawaida baadaye kuna mambo yaliyotokea tukaonekana [Yeye na Fina Mango] ni watovu wa nidhamu tukafukuzwa,” alisema Kipanya wakatik akihojiwa kwenye kipindi cha Danga Chee cha Channel 10.

“Kwahiyo I was fired, nilifukuzwa kazi. Sasa miaka minane baadaye watu hao hao wakikuapproach kufanya nao kazi kwa terms ambazo mnakaa chini sasa kama watu wazima, watu ambao wanaona kabisa kwamba miaka minane umekaa bila wao na ya kwako yanakuendea. Kwanza hapo kuna heshima kubwa sana, katika hali ya kawaida nilitakiwa niwe nimeshadondoka, sipo, sifai, siwezekani tena. Lakini kama watu wamekuona kwamba unahitajika kwenye ile sehemu ni kipimo kingine cha kuonesha kwamba ‘okay kumbe kitendo cha kubaki kwenye media kama mchoraji katuni thamani iko pale,” alifafanua.

“Lakini namba mbili ni kwamba ninapofuatwa nirudi Clouds, tumekaa mezani tumezungumzia masuala ya mkwanja wa kutosha, wakati huo huo project zangu zote hakuna hata moja inayovunjika, kuna tatizo gani mimi kutengeneza extra money katika masaa matatu au masaa manne?”

Maoni yangu: Vijana mmesikia?! Kama mnajiamini mna vipaji au uwezo wa mnavyovifanya, komaeni tu. Pesa zipo ukiwa na thamani yako.

Inahamasisha sana!
 
Hakuna kitu kizuri kama kujibland,inatakiwa uwe juu ya redio na sio redio iwe juu yako.ukushakuwa bland huwi na hofu kwa sababu unajua kabisa kwamba ukitoka tu basi hicho kipindi lazima kitadoda
 
Vizuri Masudi ji brand then wape uhuru as kuchagua kama wana uwezo wa kununua brand yako
 
Kiukweli hakuna kitu kilichowafrustrate Clouds media kama kuondoka kwa Gerald Hando. Yule jamaa ni kichwa sana nje ya utangazaji.

Ruge alifanya kosa sana kumwachia. Sasa clouds ina struggle sana kujiimalisha maana ata waliorudi bado hawajakata kiu ya waskilizaji.

Kiufupi Gadna na Kipanya wamekuta generation yao imeacha kusikiliza radio ni kama wanaanza upya kuendana na hii era.
 
Nimesikitika sana kuondoka kwa Gerald Hando. Jamaa anajua sana kutangaza. Power breakfast aliiwezea sana, zaidi zaidi yupo vizuri kichwani, anajua kuhoji kwa weledi na kuchambua mambo vizuri sana, kujenga hoja...nk, nk.

Sidhani kama Kipanya ataweza kuvaa viatu vya Hando.

Fredwaa nae ndio hata sielewi anachofanya pale.
 
nimeona si vema kutumia picha za watu wengine.

kwa sasa na kuendelea nitakuwa natumia profile image ambazo zina picha zangu Mimi mwenyewe.

Nilikuwa sijui kama kumbe na Wewe una sura za Vijana wa Dar es Salaam! Hata Mimi nimeona sasa si vyema kutumia picha za Watu na nimeamua kuitumia hiyo hapo ambapo ndiyo Mimi mwenyewe hutaki shauri yako.
 
Hiyo yote washukuliwe washindani wa hiyo redio kwani ndipo hapo thamani ya kina Kipanya ilipoonekana.

Back
Top Bottom