Elections 2010 Kura za Vyuo vya Vikuu: TAHLISO yamtuhumu Mwenyekiti wake 'kutumiwa'; atimuliwa

wao wanakuja kila wakati kuchakachua maamuzi ya wenzao.. ndivyo ilivyokuwa hata wakati ule wakati DARUSO wamefanya hivi TAHLISO wanafanya vile.. yawezekana vyombo hivi viwili vina mitazamo yenye itikadi za kisiasa na hivyo kuwagawa wanafunzi wa elimu ya juu?

HAPO MKUU UMENENA...Siasa na njaa zinaleta shida kwenye umoja huu...Hii si mara ya kwanza viongozi kutofautiana.Baadae wenda tukawa na VYAMA VIWILI PINZANI...HAPO.
 
TAMKO LA TAHLISO KWA UMMA KUTAARIFU JUU YA UPOTOSHWAJI
WA HABARI ZINAZOHUSU UPIGAJI WA KURA KWA WANAFUNZI WA
VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA.

Fungua attachment kuendelea.
Kwanini asante kwa tamko hili. Invisible naomba nisaidie kuliatach kwenye posti yangu ya mwanzo, natumia mobile, options za attachment bado hazijawa activated.
 
Mi niliwashangaa sana hawa madent, where where they? vyuo vilifungwa, june, july, wanakuja lalamika octoba, to me they were not serious na naweza amini kuna mtu nyuma yao, walikuwa hawajui? hata kama wako right kiasi gani kudai haki yao sasa ni kuonekana walalamishi na wanatumiwa? Nakumbuka niltuma post ya kuongelea hili suala mwezi april or march, watu walipuuza, if they were seroius they colud act that time wakati vyuo havijafungwa, na ratiba hazijapangwa. eti wanajidai kutoa masaa 72, kwanani? TZ, kwa umuhimu gani walionao? anyway....... mi sipendi kusema kwamba walitolewa kisa ni kuogopa kura kwa upinzani, jamani vyuoni kuna wana ccm kibao? tena very active, there are branches za ccm, dent wanavaa sare kwenye vikao proudly kabisa, amini usiamini nenda kafanye sensa, jumuiya zote zipo vyuoni kuanzia wazazi, Uwt, vijana wapo. what I believe ni kuwa wameibana pesa za kuishi chuoni wamepeleka kwenye uchaguzi.
 
Uongozi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, TAHLISO, umelikana tamko la Mwenyekiti wake aliloipa serikali saa 72 kuamua hatma ya wanafunzi hao, kwa kusema alijisemea kwa nafsi yake, na alilitoa kwa kutumwa na kikundi fulani bila kukitaja.

Katibu Mkuu wa TAHLISO, amezungumza leo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Karimjee na kusema takwimu zilizotolewa sio takwimu halisi, kwani wanafunzi wa mwaka wa kwanza, watapigia kura walikojiandikishia, wakati wale wa mwaka wa 3 na wa nne, ndio wameshamaliza vyuo hivyo wasingepigia vyuoni.

Hata wale wa mwaka wa pili, wako kwenye mafunzo kwa vitendo hivyo bado wasingepia vyuoni.

Katibu huyo ametoa mwito kwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu, kuwa huru kupigia kura walikojiandikishia.

Wametoa shutuma nzito kwa Mwenyekiti wao kutumiwa kwa kutoa tamko bila kuwashirikisha, hivyo amevunja katiba yao na kujifukuzisha kazi!.

Nimehudhuria Press Conference hii na nilipowauliza kuhusu tuhuma za kutumiwa, viongozi hao waliishia kujikanyakanyaga, ila pia hata hiyo press release yao ya kurasa 4! sii bure!.
lazima utaratibu ufuatwe sio anaibuka na kuanza kutoa matamko kwa watu wanaomsomesha.....
 
lazima utaratibu ufuatwe sio anaibuka na kuanza kutoa matamko kwa watu wanaomsomesha.....
Asante Joyce, naungana na wewe, kwa heshima ya kiafrika mtoto hatoi amri kwa mzazi wake na kumpa altimatum ni ukosefu wa nidhamu ndio maana akaonekana kama anatumiwa. Hii press conference ya jana ya katibu wa Tahliso, na yeye alikuwa akiisoma karatasi huku anajiuma uma, ishara inayoonesha ameandikiwa!, hivyo na wao pia wanatumiwa.

Hivi vyama vya wanafunzi maranyingi sana hutumiwa kwa malengo ya kisiasa, nikiwa mwanafunzi Mlimani, nilishuhudia jinsi DARUSO ilivyojigeuza mamluki wa CCM!.

Hii ni kawaida, hizi njaa zinatupeleka kusiko, ila wakati wa uchaguzi, ndio wakati wa mavuno, acha vijana vijvunie kidogo dogo wawe fit kabla shule hazijafunguliwa.
 
TAHLISO ni kiinimacho jamani,mbona tumesema siku zote sisi wanafunzi? Kwanza haiungwi mkono na wanafunzi, pili tangu imeanzishwa imekuwa inatumika kupunguza makali ya vuguvugu za wanafunzi kudai haki zao. Kuanzishwa kwake kunatia shaka sana. Viomgozi wake hawawajibiki moja kwa moja kwa wanafunzi japo wanajidai kuwawakilisha.

DARUSO mara nyingi sana imetofautiana na TAHLISO kwani mara nyingi DARUSO inapochukua uamuzi kudai haki ya wanafunzi pale UDSM TAHLISO inaingilia wakati hayo ni mambo ya ndani ya chuo.
 
Huyu jamaa anaposema wanafunzi wa mwaka wa pili wangekuwa field anakosea kwani field tayari zimeisha, pili engineering wanafanya kozi miaka 4, hivyo mwaka wa tatu walitakiwa kuwa vyuoni pia.

Kwa maana nyingine waliotakiwa kuwa vyuoni ili wapige kura ni kama ifuatavyo
-Mwaka wa kwanza wanaoingia mwaka wa pili.
-Mwaka wa pili wanaoingia mwaka wa tatu
-Mwaka wa tatu wanaoingia mwaka wa 4 (Engineering,medicine na baadhi ya kozi pale SUA)
-Mwaka wa nne wanaoingia mwaka wa tano (Medicine na baadhi ya kozi pale SUA)

Pia hao viongozi wa TAHLISO hawawakilishi wanafunzi kwani karibu wote walimaliza vyuo tayari. Mfano huyo mwenyekiti alimaliza chuo, sasa anawakilisha wanafunzi wapi? Ili uwe kiongozi wa TAHLISO sifa ya kwanza lazima uwe mwanafunzi. Uanafunzi unapokoma na uongozi unakoma siku hiyo hiyo, nafasi inakuwa wazi mpaka uchaguzi ufanyike.

TAHLISO ni wachakachuaji sana tunawajua,wanatumiwa sana na chama fulani cha siasa. Kuna mtoto wa kiongozi mkubwa wa chama fulani ndiye anatumika kuunganisha chama na hiyo TAHLISo. Siku za karibuni baada ya janja yake kujulikana amekuwa anamtumia kijana mwingine ambaye alimaliza mlimani 2008 na aligombea ubunge mtwara mwaka huu kwenye chama ila kura hazikutosha.

Mimi nilishangaa sana mwaka huu TAHLISO ilianza kuonekana kuchukua mtazamo tofauti na tuliouzoea pale mwenyekiti wake alipoanza kutoa matamko kuhusiana na wanafunzi kutopiga kura. Kumbe alikuwa anapingwa hata na wenzie (mamluki) kwenye TAHLISO.
 
Me sikubaliani na wewe.....Vyuoni siyo safe haven kwa CCM. CCM huwa inatumia baadhi ya viongozi wenye njaa ili ionekane inakubalika vyuoni. Kwa taarifa yako, ukiwa unagombea uongozi chuoni hasa mlimani na ikajulikana au ikahisiwa una uhusiano na CCM, huwezi kupata kura za kutosha. Lakini ni vigumu kujua yupi ana uhusiano na CCM ndiyo maana CCM huwa inafanikiwa kupandikiza viongozi. Yaani swali ambalo kila mgombea anaulizwa ni uhusiano wake na vyama vya siasa hasa CCM. Wagombea huwa wanalijua hilo kuwa CCM haikubaliki vyuoni hivyo huwa anajiweka nayo mbali sana wakati wa kampeni.
 
Siku hizi hakuna serikali ya wanafunzi, kuna mamluki tu ambao wanafikiri uongozi ni price tag au pengine ni jina la ubatizo. Kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa elimu ya juu unapokuwa mwoga na kukubali kutumiwa na CCM ili umpinge mwanaharakati kama mwenyekiti wa TAHLISO unakuwa huna tofauti na mtu anayejiuza mwili wake na hasa mashoga.

Enzi zetu serikali ingetia adabu....kwanza saa hizi tungekuwa vyuoni. Na ndo maana kuna kunji tuliwahi ipiga siku nne kabla ya uchaguzi kudadadeki. Enzi zile wananchi ndo walikuwa wanatupinga, wangekuwa na mwamko kama sasa, saa hizi CCM ingekuwa imesha 'surrender'.

Katibu wa TAHLISO na makenge wenzako acheni ushoga.
 
Huyu jamaa anaposema wanafunzi wa mwaka wa pili wangekuwa field anakosea kwani field tayari zimeisha, pili engineering wanafanya kozi miaka 4, hivyo mwaka wa tatu walitakiwa kuwa vyuoni pia.

Kwa maana nyingine waliotakiwa kuwa vyuoni ili wapige kura ni kama ifuatavyo
-Mwaka wa kwanza wanaoingia mwaka wa pili.
-Mwaka wa pili wanaoingia mwaka wa tatu
-Mwaka wa tatu wanaoingia mwaka wa 4 (Engineering,medicine na baadhi ya kozi pale SUA)
-Mwaka wa nne wanaoingia mwaka wa tano (Medicine na baadhi ya kozi pale SUA)

Pia hao viongozi wa TAHLISO hawawakilishi wanafunzi kwani karibu wote walimaliza vyuo tayari. Mfano huyo mwenyekiti alimaliza chuo, sasa anawakilisha wanafunzi wapi? Ili uwe kiongozi wa TAHLISO sifa ya kwanza lazima uwe mwanafunzi. Uanafunzi unapokoma na uongozi unakoma siku hiyo hiyo, nafasi inakuwa wazi mpaka uchaguzi ufanyike.

TAHLISO ni wachakachuaji sana tunawajua,wanatumiwa sana na chama fulani cha siasa. Kuna mtoto wa kiongozi mkubwa wa chama fulani ndiye anatumika kuunganisha chama na hiyo TAHLISo. Siku za karibuni baada ya janja yake kujulikana amekuwa anamtumia kijana mwingine ambaye alimaliza mlimani 2008 na aligombea ubunge mtwara mwaka huu kwenye chama ila kura hazikutosha.

Mimi nilishangaa sana mwaka huu TAHLISO ilianza kuonekana kuchukua mtazamo tofauti na tuliouzoea pale mwenyekiti wake alipoanza kutoa matamko kuhusiana na wanafunzi kutopiga kura. Kumbe alikuwa anapingwa hata na wenzie (mamluki) kwenye TAHLISO.
katibu katumwa.............. hebu katibu tupe kifungu kinachokupa nafasi ya kutamka mabaya ya bosi wako kama ulivyofanya........... ALIYECHAGULIWA KWA KURA HUONDOLEWA KWA KURA NA SI VINGINEVYO.

HIVI KATIBU UNAJIFANYA HUJUI KUWA KUNA KOZI ZINAKWENDA ZAIDI YA MIAKA MITATU........????
 
Mi nashangaa TAHLISO wanaingiaje kwenye haya mambo

Kinachoendelea hivi sasa kina wafanya wanafunzi wote kuonekana wajinga na wasaliti. Unless mtu aniambie walikuwa hawajui mapema kuwa siku ya uchaguzi watakuwa chuo ama wapi.

Zanzibar miaka yote wanafunzi waliokuwa bara walikuwa wanarudi visiwani kwenda kupiga kura

Itikadi zetu za ukombozi hazijamnoa mwanafunzi huyu kujua umuhimu wa kura kuwa unaweza kusafiri kwenda kupiga kura no matter what??

after all kwa tunaojua vizuri wanafunzi hawa maneno mengi tu wengi wao ni CCM damu.

However, kama alivyogusia hapo juu mtu mmoja. Hizi siku nane wanafunzi waende kwenye tume ya uchaguzi, waombe mwongozo wa kupiga kura. WANAWEZA KUPIGA KURA POPOTE PALE WALIPO KWA RUHUSA MAALUMU, SIJAONA TATIZO
 
Huyu jamaa anaposema wanafunzi wa mwaka wa pili wangekuwa field anakosea kwani field tayari zimeisha, pili engineering wanafanya kozi miaka 4, hivyo mwaka wa tatu walitakiwa kuwa vyuoni pia.

Kwa maana nyingine waliotakiwa kuwa vyuoni ili wapige kura ni kama ifuatavyo
-Mwaka wa kwanza wanaoingia mwaka wa pili.
-Mwaka wa pili wanaoingia mwaka wa tatu
-Mwaka wa tatu wanaoingia mwaka wa 4 (Engineering,medicine na baadhi ya kozi pale SUA)
-Mwaka wa nne wanaoingia mwaka wa tano (Medicine na baadhi ya kozi pale SUA)

Pia hao viongozi wa TAHLISO hawawakilishi wanafunzi kwani karibu wote walimaliza vyuo tayari. Mfano huyo mwenyekiti alimaliza chuo, sasa anawakilisha wanafunzi wapi? Ili uwe kiongozi wa TAHLISO sifa ya kwanza lazima uwe mwanafunzi. Uanafunzi unapokoma na uongozi unakoma siku hiyo hiyo, nafasi inakuwa wazi mpaka uchaguzi ufanyike.

TAHLISO ni wachakachuaji sana tunawajua,wanatumiwa sana na chama fulani cha siasa. Kuna mtoto wa kiongozi mkubwa wa chama fulani ndiye anatumika kuunganisha chama na hiyo TAHLISo. Siku za karibuni baada ya janja yake kujulikana amekuwa anamtumia kijana mwingine ambaye alimaliza mlimani 2008 na aligombea ubunge mtwara mwaka huu kwenye chama ila kura hazikutosha.

Mimi nilishangaa sana mwaka huu TAHLISO ilianza kuonekana kuchukua mtazamo tofauti na tuliouzoea pale mwenyekiti wake alipoanza kutoa matamko kuhusiana na wanafunzi kutopiga kura. Kumbe alikuwa anapingwa hata na wenzie (mamluki) kwenye TAHLISO.

Vunjeni sasa hiyo TAHLISO mnasubiri nini.
 
Nilisema toka mapema Chadema forums imetanda hadi vyuoni,ona sasa kamwaga ugali kwa ujinga!
kamwaga ugali upi, viongozi wa TAHLISO huchaguliwa kutoka na Maraisi wa vyuo mbali mbali na mara nyingi hufanya kazi kwa kujitolea
 
wananiudhi hawa wanaojiita wasomi wa siku hizi, fake mind just like ccm
 
Back
Top Bottom