Kura za Vyuo vya Vikuu: TAHLISO yamtuhumu Mwenyekiti wake 'kutumiwa'; atimuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura za Vyuo vya Vikuu: TAHLISO yamtuhumu Mwenyekiti wake 'kutumiwa'; atimuliwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 21, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, TAHLISO, umelikana tamko la Mwenyekiti wake aliloipa serikali saa 72 kuamua hatma ya wanafunzi hao, kwa kusema alijisemea kwa nafsi yake, na alilitoa kwa kutumwa na kikundi fulani bila kukitaja.

  Katibu Mkuu wa TAHLISO, amezungumza leo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Karimjee na kusema takwimu zilizotolewa sio takwimu halisi, kwani wanafunzi wa mwaka wa kwanza, watapigia kura walikojiandikishia, wakati wale wa mwaka wa 3 na wa nne, ndio wameshamaliza vyuo hivyo wasingepigia vyuoni.

  Hata wale wa mwaka wa pili, wako kwenye mafunzo kwa vitendo hivyo bado wasingepia vyuoni.

  Katibu huyo ametoa mwito kwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu, kuwa huru kupigia kura walikojiandikishia.

  Wametoa shutuma nzito kwa Mwenyekiti wao kutumiwa kwa kutoa tamko bila kuwashirikisha, hivyo amevunja katiba yao na kujifukuzisha kazi!.

  Nimehudhuria Press Conference hii na nilipowauliza kuhusu tuhuma za kutumiwa, viongozi hao waliishia kujikanyakanyaga, ila pia hata hiyo press release yao ya kurasa 4! sii bure!.
   
 2. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hawana akili nzuri hawa, si bure!!

  "Mtu mwenye akili akikwambia jambo la kipumbavu huku akitambua kuwa jambo hilo ni la kipumbavu, nawe ukalifuata, atakudharau sana" Mwl J.K Nyerere.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Fedha haramu madhara yake ndiyo hayo.Vijana wamechukua toka mafisadi mkwanja tayari.Hao ndo wasomi wa leo this is absolutely ridiculous
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (sura ya 343) 30 Juni 2010 chini ya AG Jaji Werema

  35C (3) Tume inaweza kutoa maelekezo na kuweka masharti ambayo mtu anaweza, katika siku ya uchaguzi wa Rais, kuruhusiwa kupiga kura katika kituo cha kupiga kura mbali ya kile alichopangiwa

   
 5. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  "Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. " (Kutoka 23:8).
   
 6. m

  mbea Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilisema toka mapema Chadema forums imetanda hadi vyuoni,ona sasa kamwaga ugali kwa ujinga!
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nasikitika kuona hii TAHLISO tulioiasisi tulihangaika sana kupata usajili na tukatarajia kwamba ingekuwa mahali sahihi kwa wasomi wa kitanzania kuwa mfano kwa watanzania wengine lakini imegeuka kuwa kijiwe cha wahuni tu kama walioko vijiweni mitaani.

  Yani TAHLISO imekuwa ya hovyo kabisa, wanatumiwa sana na wanasiasa na kushindwa kujua misingi ya kuanzishwa kwake.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm imejaa wafanya mizaha, wanawatumia watoto hao kufanya nao mizaha, mwenyekiti wao mleta mizaha, ndio maana nasema kile chama kimejaa wasanii tupu.
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Hii kauli siyo sahihi kisheria. Huyu Mwenyekiti wao akienda mahakamani atawashinda tu. Ni kikao kilichomchagua tu ndicho chenye mamlaka ya kumwondoa hawezi kuhukumiwa na viongozi walio chini yake hata kama kweli makosa ameyafanya.....Ule usemi usemao "Mwiba uingiliako ndiko utokeako" ni sahihi hapa.....Ninamwona huyo katibu wa TAHLISO kuwa yeye ndiye anayetumiwa na CCM ili kupunguza makali ya tuhuma ya NEC kuwanyima wanafunzi kushiriki kwenye uchaguzi...Hoja zake zipo wazi kabisa...........

  Ukitaka kumjua kiongozi ana matatizo angalia nyendo zake mara nyingi utamwona ana papara papara kama za huyo katibu tajwa......Ni utovu wa nidhamu kuzungumzia hatma ya bosi wako nje ya vikao ambavyo na huyo bosi wako hakuwa ameshiriki ili kulinda haki yake ya asili ya kusikilizwa...........Kama huyo Katibu ni mkweli mbona tunasikia wamekwenda kufungua kesi ni ya nini sasa?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Vuguvugu la ukombozi afrika lilianzia na kuendelezwa na wasomi waliokusanyika dar UDSM. lakini leo tanzania ndiyo inayohitaji kukombolewa na kwani mpaka wasomi wameshakula sumu kwa hiari yao
   
 11. C

  CAIN Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fikiri kabla ya kutenda na kumbuka uliyosema leo utaulizwa kesho. Kalagabahooo
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kuna wa mwaka wa kwanza wanoa ingia mwaka wa pili,intake ya 2009/2010 walijiandikishia chuoni (naongelea udsm),pia kuna mwaka wa pili kuingia wa tatu,intake ya 2008/2009 hawa pia walijiandikishia chuoni.

  Mwaka wa kwanza udsm walikua takribani 6,000 tukadirie na mwaka wa pili ni 6000 pia,....6000+6000=12,000!

  Hii ni udsm peke yake,na TAHRISO sio udsm ni umoja wa vyuo vikuu Tanzania,kuna vyuo vingapi nchini?

  Hawa wametumwa,sio bure!!!
   
 13. K

  Kwanini Senior Member

  #13
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAMKO LA TAHLISO KWA UMMA KUTAARIFU JUU YA UPOTOSHWAJI
  WA HABARI ZINAZOHUSU UPIGAJI WA KURA KWA WANAFUNZI WA
  VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA.
  UTANGULIZI:
  TAHLISO ni umoja huru wa wanafunzi, wa Vyuo vya Elimuya ya Juu Tanzania na umoja huu ulianzishwa na kusajiliwa rasmi tarehe 5/5/2004 na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na namba ya usajili wake ni SO No. 14245 ina wanachama wapatao 53 (Vyuo). Hivi karibuni mjumbe wake mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa TAHLISO ametoa taarifa katika vyombo vya habari kuhusiana na suala la upigaji wa kura kwa wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania. Na hivyo basi suala hili kuchukua kasi katika vyombo vya habari kila siku.TAHLISO inasema ndugu Katongo amezungumza kama mtu binafsi bila kuitisha kikao cha Kamati ya Utendaji (EX-COM), na huu ni ukiukwaji wa katiba ya TAHLISO kama chombo chetu. Baada ya EX-COM kukutana kwa dharura kuhusiana na matamko haya ya Mwenyekiti wa TAHLISO, imetafakari kwa kina na kwa kuzingatia katiba ya TAHLSO ikaibaini mapungufu yafuatayo;
  1.Ni kwamba mwenzetu huyu amekurupuka katika kutoa matamko haya, tunasema hivi kwa sababu, kwa mujibu wa katiba yetu ya TAHLISO wa Ibara ya 19 inayozungumzia kazi na wajibu wa Katibu Mkuu wa TAHLISO Ikiwa ni pamoja kutoa matamko,taarifa katika vyombo vya habari, mwenyekiti TAHLISO amevunja kipengele hicho na kufanya kazi ambayo si yake kinyume na katiba, kanuni na taratibu za TAHLISO.
  2.Mwenzetu huyu ameonyesha ubabaishaji mkubwa kwa kutokuwa makini katika tamko lake kwa kuhusisha Tume ya vyuo vikuu (TCU) na hoja ya upigaji kura kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. Tunasema hivi kwa sababu yeye ni mjumbe wa bodi ya TCU kwa mujibu wa katiba yetu ya TAHLISO, na katika kikao cha TCU kilichofanyika mwezi wa nne ambacho yeye alihudhuria tulitegemea kuwa katika suala hili kama halidhiki nalo angeanza kupinga kwenye kikao kwanza na kama ingeshindikana angekuja kutushawishi sisi wajumbe wa EX-COM kuhusiana na hoja hii ili kama ni maandamano ya amani tuyafanye kipindi hicho. Hata hivyo wakati tunapokea taarifa ya mjumbe kutoka bodi ya TCU katika mkutano wetu wa senate ambao ulifanyika pale chuo kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) ndugu Katongo alidiriki kusema hana taarifa yoyote ya kuhusiana na utendaji wa bodi hiyo. Iweje leo aje na kauli hii ya bodi ya TCU kuwa imehusika katika kupanga vyuo vifungue lini ili wanachuo hawa wa elimu ya juu wasipige kura? Kufanya hivi kwanza ni kukiuka msimamo wa bodi hiyo. Hivi ndugu zangu waandishi wa habari mjumbe akitaka kuzungumzia msimamo wa bodi/kikao cha baraza la mawaziri si lazima ajiuzulu ndipo azungumzie msimamo wa baraza hilo? Si mnakumbuka Mh. Mrema alipotaka kupinga msimamo wa baraza la mawaziri alijiuzuru kwanza ndipo akayazungumzia.
  Hivyo basi sababu za wanafunzi kutopiga kura kama alivyobainisha katika tamko lake si za kweli.
  Aidha, tunachokiona sisi kama TAHLISO huenda mwenzetu huyu anatumiwa na watu kutufikisha hapa tulipo. Tunasema hivi, Kwa kuwa tunashangaa kwanini hakutuita sisi wenzake EX-COM atueleze haya na tumpe baraka za kuzungumzia haya kikatiba.

  Fungua attachment kuendelea.
   

  Attached Files:

 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wao wanakuja kila wakati kuchakachua maamuzi ya wenzao.. ndivyo ilivyokuwa hata wakati ule wakati DARUSO wamefanya hivi TAHLISO wanafanya vile.. yawezekana vyombo hivi viwili vina mitazamo yenye itikadi za kisiasa na hivyo kuwagawa wanafunzi wa elimu ya juu?
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ni njia nzuri sana kufarakana hadharani. Ilitakiwa wakutane wenyewe walimalize ndani ya TAHLISO kabla ya kulifanya kuwa PUBLIC................ haya hayakuwepo enzi zetu............. kati yao kuna wanaotumiwa na baadhi ya watu kwa manufaa yao. NGOJA TUSUBIRI ILI TUONE MWISHO WAKE.
   
 16. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu katibu wa TAHILISO inamaana haoni kama wanachuo wananyimwa haki ya msingi na serekali au anafikiri rais atakuwa JK tarehe moja.
  Huyu jamaa tunamfahamu ni mamluki wa siku nyingi, ni Kada wa sisiem kwahiyo tusisubiri jipya kutoka kwake.

  Chamsingi ni kama alivyosema Dr. Slaa demokrasia ni gharama, sisi wanafunzi tujitahidi kurudi maeneo tuliyojiandikisha then tupige kura.

  Au kama mtu ameshindwa kabisa kurudi chuoni awe Wakala wa kulinda kura za upinzani zisiibiwe.

  SLAA RAIS 2010-2015: visit online polls: mwananchi.co.tz,mwanahalisi.co.tz,majira.co.tz
   
 17. K

  Kwanini Senior Member

  #17
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Jamii Forums na Wazalendo Forums au Simba na Yanga.
   
 18. K

  Kwanini Senior Member

  #18
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK anapata kura za Moshi,Arusha,Lindi,Mwanza,Mtwara,Mara,Dar es salaam,Morogoro,Mbeya..............................Zanzibar.Wewe piga za mtandaoni afu Slaa awe president wa Jamii Forums.Lmao
   
 19. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2010
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  alichopewa huyu jamaa huenda ni chini ya milioni moja tu, kauza wenzake hivi hivi
   
 20. semango

  semango JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  aliekwambia jk atapata kura sehemu zote hizo nani?au ndio hayo macontainer ya kura zilizochakachuliwa tunayoyasikia yameingia nchini ndio yanawapa jeuri na kiburi cha kusema hivyo?
   
Loading...