Kura za maoni: CCM Mil. 220. CHADEMA Mil. 6.2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura za maoni: CCM Mil. 220. CHADEMA Mil. 6.2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Mar 10, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii imekaaje haya si matumizi makubwa mno kwa mujibu wa sheria mpya ya uchaguzi?
  Tendwa anasemaje kwa hili.

  Wajumbe CCM 1134.

  Wajumbe CHADEMA 880.
   
 2. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Nimesema mara nyinyi hapa jamvini. Hakuna aliye CCM bila kufuata pesa. Chadema wamempata mjombea kwa TZS 6.2m wao TZS 220m!! Hii inaonyesha jinsi gani wanachama wa CCM wapo kwa ajili ya pesa tu. Nadhani idea ya Mbowe kukataa ruzuku ya serikali itasaidia sana kujenga vyama vyote vya siasa na kupata watu wenye mapenzi ya kweli katika vyama na siyo kufuata pesa
   
 3. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaani kupata mgombea tu ndo kiasi chote hicho cha pesa ama kweli tanzania mafisadi wanapeta na tusishangae mshahara wa mwezi huu kulipwa may maana makusanyo yote yanaenda kununua kura huko
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Pamoja na zile alizohonga mzee wa mvi lazima ifike billion na bado wakamsimamisha aliyetoboa sikio
   
 5. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hii kali! nasuburi majibu jumatatu toka CCM
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  ccm kwa matumizi kiboko!hizo zingejenga bwawa la umwagiliaji kule arumeru
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tushawazoe sisiemu kwa matumizi mabaya,we angalia nyumba ya spika imetumia bil 1.5 wkt hata mil400 haifiki.
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  UNASHANGAA LEO WEWE ULIZALIWA WAPI WAKATI CCM ILIPOKUWA INAPWANYA MAPESA ENZI ZA CHAMA CHASHIKA HATAMU.uchaguzi wa kizota ghalama zake zilikuwa zinaweza kujenga secondari mia saba na labs zake lakini makada wakaona heri kuzitumia ktk uchaguzi kuliko elimu!
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hizi ni pesa zilizo kwenye vitabu je zisizo julikana ni ngapi achilia mbali zile za rushwa.
   
 10. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Pesa yote hii na ikamfanya bwana mkubwa akimbizwe hospital kulazwa..
   
 11. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawashangaaga sana watu wa vijijini ambao wanavaa ma Tshirt and kapelo za chama cha mapinduzi. CCM na ya wenye fedha na siyo maskini. watu wanafikirikiri Kikwete akisema "Kidumu chama cha mapinduzi" wao wanajibu kidumu, na kina weneyewe, na wenyewe ndiyo sisi, pamoja na wewe. Ile sisi ina maana akina Chenge, EL, RA, JK, Membe, Nahodha, Mkono, Kilango, Makinda na wengine wa aina hiyo. Walalahoi wanaosema wenyewe ni sisi, wanajipendekeza tu, na mara nyingi thamani yao kubwa ni wakati wa uchaguzi kama huu wa Arumeru.
   
 12. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  U
  Kashangae feri meli inaelea shilingi inazama! CCM ni Amani na utulivu, ukizingatia umoja wa kitaifa!!!! tuongee point muhimu za maendeleo ndio maana ya ushindani sio kashfa zisizomsadia mwananchi wa kawaida. Tusijenge chuki bila sababu.
   
 13. sodeely

  sodeely Senior Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Pumbavu gamba mkubwa wewe..
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuitetea chadema inahitaji uwe na akili ya sabato masalia (wanaomini kusafiri bila passport)
   
 16. J

  Juma Bundala Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi ninavyo jua mwizi kamwe huwa haachi hadi kuchomwa moto,na moto wa kisiasa ni kuwatoa CCM madarakani.Ni mimi na wewe mwana JF ndio tutakao wachoma moto hawa CCM kwa kuwatoa madarakani TUANZIENI ARUMERU MASHARIKI.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pelekeni ulokeole wenu hai..wameru hawana muda na chadema
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Hakika kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakika kuitetea chadema inahaitaji uwe na akili sabato masalia!!!
   
 20. Mwigulu Nchemba

  Mwigulu Nchemba Verified User

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 180
  Wana JF mimi naamini unafiki na uongo sio sifa nzuri, ukweli unatabia ya kujitokea juu ya uongo. Mimi ndiye mweka hazina wa CCM nawambien hatujatumia milion 220 kura za maoni. Hii nadhani ni matatizo ya macho ya MHE MBOWE labda aliacha miwani nyumbani million 22 anasoma 220.Na hizi ilikuwa nauli kwa wajumbe. Ukimpa kila mjumbe sh elfu kumi nauli yake tokea ngarenanyuki hivi kweli ni matumizi mabaya? Hivi kweli mara zote tunajisifu kwamba tupeni nchi tuboreshe maslahi ya watu tukimaanisha kumlipa kila mtu sitahili yake ku demonstrate kauli hizi kwenye cha ni kutokuwalipa wajumbe? Wana jf pigeni hesabu wajumbe 880 wakipewa elfu tano kila moja ni sawa na 4.4m na bado kukodi ukumbi, bado bodaboda, bado chakula, bado mafuta na nauli ya vipngozi wa chadema walioluja kura za maoni, bado garama za vikao vya kamati kuu. Nimeuliza kwa mjumbe mmoja aliye kwepo kato ya hao 880 akasema walipewa elfu 10 nao ukizidisha mara wajumbe niilioni nane nukta nane(8.8) ni kweli tumefila kutaja figure tu hata kama sip ya kweli? Mimi kama mweka hazina wa chama sioni ubaya kuwalipa wajumbe nauli zao na posho ya kikao na uwezo ukiruhusu natamani wajumbe jata walipwe zaidi per diem kabisa ndio kuongeza mzunguko wa pesa. Ni unafiki kusema kuwa ni haramu kuwalipa wajumbe wa chama changu elfu kumi halafu useme nikipata nchi notawalipa walimu marambili ya sasa nitawalipa posho madakitari mara tatu ya sasa. Stahili ya wajumbe wa chama ni hii na ya madaktari ni ya kutibu. Nachukia unafiki.
   
Loading...