Kwani, msingi wa ukokotoaji wa 2/3 katika pande zote za muungano ulikuwa unazingatia idadi ipi ya wajumbe wa BMK? Huyu mama from the beginning aliwekwa upande upi wa Muungano bila kujali asili yake ni Tanzania Bara/Tanganyika au Zanzibar?........Hapa iwe isiwe, Zakhia Meghji ni lazima ilikuwa apige kura kuwakilisha upande mmoja tu wa muungano pasipo kujali asili yake na wala si vinginevyo......na kamwe tusidanganyane kabisa hapa!!
Aidha,kama idadi ya wajumbe wa BMK kutoka pande zote za Muungano haikuwekwa wazi toka mwanzo na sheria iliyoliweka hilo Bunge katika operation, then Samwel Sitta na watu wake watakuwa walitumia ipasavyo weakness hiyo kufanya kweli katika uchakachuaji wao kwa kadiri busara ya mwenyekiti ilivyoona na kwa maana hiyo BMK liko sahihi, hakuna kosa hapo....bali ni kosa la sheria yenyewe kwa kutokuelekeza!
Mwisho katika BMK kulikuwa na wajumbe wa aina mbili; Mosi ni wale kundi la 201 ambao waliteuliwa na Marais wote wawili (Kikwete - JMT na Shein - Zanzibar), na pili ni wale wa wabunge wa Bunge la JMT (wa majimbo,kuteuliwa na Rais na viti maalumu) pamoja na wale Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Hapa baadhi ya wachangiaji wanamchanganya Zakhia Meghji kuwa aliingia katika BMK kuwakilisha kundi gani. Jibu ni kuwa Zakhia Meghji ni mbunge wa viti maalumu katika bunge la JMT na kwa hiyo aliingia kwa tiketi hiyo na wala hakuwa miongoni mwa wateule wa Marais kutoka katika kundi la 201.
Sasa hapa, swali la msingi hapa ni je, katika 2/3 alikuwa anahesabiwa kama Mzanzibar au Mtanganyika/Tanzania Bara?.....Mwenye Orodha rasmi ya wajumbe wote toka Zanzibar na Tanzania Bara/Tanganyika walioshiriki katika BMK na kuainishwa/kutambuliwa na sheria atuwekee hapa. Hii pekee ndiyo itafunga mjadala huu na tutaelewa kura ya Meghji ni halali au si halali na toka katika upande upi.
Lakini personally, siamini na sidhani kama uongozi wa BMK unaweza kuwa wa kipuuzi na kizembe wa kiwango hiki kuwa wamchukue mtu asiye halali upande ule apigie kura upande huo badala ya ule wa kwake kisheria ili mradi tu eti kuhalalisha wanachokitaka kukipitisha huku wakijua ni kinyume cha matakwa ya kisheria. If so, then they must be put into account!!
CC. Tpmazembe, Mzanzibar Halisi, Mpiga zeze, Gor, Vyamavingi and Respect wa Boda