Kura ya Hapana yazidi kupaa CHADEMA , Humphrey Polepole, Prof. Lwaitama na Askofu

Hata kama ingekuwa kweli hayo ni ya wana-Chadema, wana uhuru wa kuamua kujiongoza jinsi wanavyotaka na yule anayekubaliana nao anaweza kujiunga nao na yule asiyekubaliana nao halazimiki kujiunga nao !

Hapa tunazungumzia katiba ya taifa la Tanzania, ambalo ni mali yetu sote na hamna option ya kujiunga au kutojiunga !. As long as sisi ni watanzania chochote kinachowekwa kwenye katiba kitatuathiri wote in a positive or negative way !

Tanzania ni zaidi ya CDM, CUF, NCCR, CCM etc.....huwezi kutaka Tanzania ifanye kile kinachofanyika CDM, CUF, CCM etc !. Katiba ya Tanzania inabidi iweke misingi ya kitaifa na iwe mfano ili vyama vilivyopo na vitakavyokuja viige kwenye hizo values za kitaifa !.

Katiba ya taifa ilikuwa Na bunge lake nani aliwatuma wawakilishi wenu wapokea bungeni?

Na itarudi mitaani na una haki ya kuikataa au kuikubali, tatizo lako ni nini?
 
Katiba hii pendekezwa ni mbaya kwa sababu;-

1. Tanzania upande wa Zanzibar kazi yao ni kutoa makamo wa rais , urais wenyewe Ngo`ooooo.

2. Maadili ya viongozi yaliyopendekezwa na tume ya kukusanya maoni yamefutwa, madhara yake mtumishi wa umma atataka kupata kiti tu na meza kwenye ofisi za umma hata asipopewa mshahara ndani ya mwaka mmoja tu wa ajira atakuwa amajenga nyumba , amenunua gari , amafanya harusi kubwa hadi kuchinja ngamia.

3. Madaraka ya rais kupunguzwa kama ilivyopendekeza tume ya Warioba imefutwa madhara yake,mashemeji wa mke wa rais, marafiki wa mtoto wa rais , mahawala wa mke wa raisi kabla hajaolewa na rais, waliokataliwa na wanainchi kwenye chaguzi kuu, waliofungwa wakatoka jela kwa msamaha wa rais woteee watapata vyeo kama ukurugenzi, ukuuwa wilaya na mkoa na vyeo vingine. Wanye kustahili na sifa za kutosha watakosa.

4. Ubunge au udiwani wawe na Elimu ingalao kidato cha nne imefutwa madhara yake, hii italeta madhara makubwa sana sana kwenye halimashuri kwa sababu wasimamizi ambao ni madiwani watazidiwa sana ki-elimu na watendaji wa halimashauri ambao ni mkurugenzi na wakuu wake wa idara. Fedha za kodi hukusanywa na TRA na zote hupelekwa hazina,kule hazina fedha hizo hurudishwa kwenye halmashauri ambako kuna watu kwa ajili ya kutekelezwa miradi mbali mbali ya maendeleo. Sasa kwa kuwa wasimamizi (madiwani) ambao wengi wao ni darasa la saba watashindwa kuzisimamia fedha hizo kutokana na umbumbu wao, watendaji(mkurugenzi na mkuu wake wa idara) watatumia mwanya huo watawaibia fedha zote mwisho wa siku miradi haitakamilika. Mfano hai halmashauri ya wilaya ya Mtwara chini ya mbunge Hawa Ghasia ina madiwani mambumbu tupu. Idara ya afya tulikula fedha zote za Semina za ukimwi, tulitengeneza semina hewa kwa maana waliohuzudhuria walikuwa ni hewa, attendance registar ilikuwa ni hewa, payment vocha tuliandika majina hewa na tukatia sahihi zao hao watu hewa na tukuchukua mshiko wote shs 60,000,000/= madiwani husika walitia sahihi zao kwenye ripoti tuliyowapelekea HAWAKUJUA CHOCHOTE MASKINI. Huu ni mfano wa halmashauri moja tu na zingine ni hivyo hivyo lakini kama madiwani wangekua na elimu ya kutosha kwa maana wangafanya monitoring kule site wangeangalia majina na kuwafuata wahusika lazima tungekamatwa.

5. 50 kwa 50 katika vyombo vya maamuzi wanawake na wanaume hii ina madhara makubwa sana kwa sababu muumba mwenyewe aliliona hili akaweka viwango na kila mtu anajua mungu alimpa mamlaka nani, hata hivyo hilo la 50 kwa 50 likitekelezwa kwenye majeshi, inchi itatekwa, Majambaji yatakuwa kila siku yanakimbia, Takukuru hawawezi kuwakamata wanaopokea hela za moto maana mala zote watuhumiwa watawashinda nguvu watakimbia na hela za moto zitapotea serikali itakula hasara.

Hii ni mifano michache tu ya ubovu wa katiba pendekezwa ya wabunge wa CCM,ILE YA WARIOBA ILIKUWA BOMBA WATU KAMA AKINA RAGE wasingepata uongozi tena ndani ya katiba ya tume ya Warioba.

Wale waliokuwa wanaitwa UKAWA walifanya makosa makubwa sana kususia wangebaki mule mule ila wakomae na rasimu ya WARIOBA, waliwaachia nyani shamba la mahindi.

Ikija KATIBA hiyo wanainchi tuikatae kabisa.

Umesahau kuwa wajumbe wa ukawa bungeni hawawazidi wa ccm na hata lile kundi la 201 asilimia 95 ni ccm. Kwenye bunge lile maalumu la katiba kubwa lililokuwa likizingatiwa ni maslahi ya chama tawala na viongozi walio madarakani na pia mwisho wa yote ni kura ambapo ukawa wasingeshinda. Hivyo kususia lile bunge ndio ilikuwa njia sahihi kuonyesha yaliyokuwa yakiendelea mle bungeni ni kinyume na rasimu iliyotoka kwa wananchi.
 
Kura ya maoni haina kuchagua vipengele vya kusema HAPANA au NDIO.......unatakiwa useme HAPANA kwa yote au NDIO kwa yote !

Na definetely nadhani kwa watu wengi si kwamba anapenda kila kitu kilichoko kwenye katiba au anachukia kila kitu....ila kura ni HAPANA kwa kila kitu au NDIO kwa kila kitu hakuna in between !

Kwa hiyo unachotegemewa kufanya ni kuangalia kama mambo ya msingi kwa mtazamo wako yamewekwa then unasema NDIO na kama mambo ya msingi kwa mujibu wako hayajawekwa then unasema HAPANA !

Definetely kwa huyo aliyesema HAPANA ni kwamba mambo ya msingi kwake hayapo kama ambavyo mimi nami nitapiga kura ya HAPANA na kuwashawishi wote ambao nina influence nao ili nao wapige kura ya HAPANA !

Fuatilia mijadala au hata baadhi ya posts hapa na utaona wadau wengi tu wanatoa sababu zenye mashiko kwa nini hii katiba inabidi ikataliwe ! Kama uliangalia kipima joto jana ITV sidhani kama utakuwa na doubt kwamba kura ya HAPANA ndio jibu sahihi kwa hii katiba ya CCM !

Mimi nitakupa sababu mbili kwangu ambazo ni kubwa :

1. Katiba haina maridhiano ya kitaifa hivyo hata bila kuangalia kilichomo ndani, hii katiba inaligawa taifa na kura yangu kwa kitu kama hiki ni NO

2. Katiba imepitishwa kwa kura za wizi wa wazi wazi, na kwa sababu mimi huwa sinunuagi vitu vya wizi, there is no way ninaweza nikasupport katiba iliyopitishwa kwa wizi, itakuwa nalitafutia taifa langu laana !

Hizo ni sababu mbili kwangu ambazo hata bila ya kuangalia content ya katiba, kura yangu ni ya HAPANA !.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
kwa kweli , tayari nimeanza kukuelewa kumbe lengo la kura yako ya hapana unataka madaraka ya Raisi yapunguzwe . Sasa yapi yapandishwe na kwa namna gani? Na pia , maridhiano ya kitaifa ulitaka yafanyikeje , kwani mimi nilichokuwa nafahamu maridhiano yalikuwa yakifanyikia Bungeni na wakati mwingine hata mzee alithubutu kuwasilikiza na kusikilizana na kuafikiana masualam ambayo yalikuwa yakiwa kwenye maudhui ya pa,moja kwa vyama vya siaa vyote vilivyounda TCD . So mbali na maridhiano hayo ulitaka yaweje ? au kilichokuwa kifanyike ni kukubaliana na matakwa ya mlengo fulani tu au iweje . Aisee naomba tsaidiane ili tuwe pamoja ili nami nitoke na kura kama yako , ila hadi sasa kwa kuwa nalipenda Taifa langu bado sijashawishiwa, hapo naona kama main point zako kama zote zilijibiwa na majibu yaka sahishwa siku nyingi. Som lets leave politics , twende na uhalisia . Ni yepi yanayoboa kwenye katiba pendekzwa kama kuna kipendele kinaruhusu masuala ya kuwekezana ndani au kuuana au kutoabudu au kutoheshimiana au kuruhusu ufisadi au kuruhusu kubakana au kugombana au kuibiana au kutoruhusu mfumo wa vyama vingi au n.k? twende pamoja kwa ushauri safi na wakitaalamu na kisheria ila siyo wa kisiasa ili nielewe nisipotoshwe...:deadhorse::flame::third:
 
Mwikemo Ntwa Gwa Kitangalala, tunapigira kura rasimu yote sio neno kwa neno, sentenso kwa sentenso, aa kwa aya, sura kwa sura au ibara kwa ibara. Tunasema HAPANA Rasmu yote ili ifanyiwe marekebisho.
Changa moto ni kuwa hapana zetu zitalindwa na nani maana mtu ambaye hakuwepo kupiga kura kwenye BMK ameorodheshwa kama alipiga kura ndiyo achilia mbali wale waliokuwepo nawakasema HAPANA. Tume ya uchaguzi bado ni ileile ya kuteuliwa na CCM. Tumeshuhudia kwa macho yetu Samweli John Sita alivyosimamia BMK kuhakikisha kile wanachokipenda CCM ndicho kinapitishwa na CCM imemsifu 6 kwa kuwa aliimba wimbo waliomfundisha.
Hivi kweli wewe Mwikemo ( mtakatifu) unaamini kura ya hapana itahesabiwa kama hapana sio ndiyo.
'''''''''''''''''''''
nasema hapana ina maana gani , kwani hutaki hata haki ya kuishi , kuabudu , kusoma , kuishi , kuenzi muungano , kuilinda Tanzania kwa gharama yoyote , Demokrasia , haki za binadamu kwa ujumla ,n.k. Naomba unieleweshe ili ikae vizuri . Na , tusaidie vipi ambavyo ni hapana kwenye katiba iliyopendekezwa ili tusije tukabatizwa hapana kw kila kitu tuakaonekana ni wehu kitaani .Please nieleweshe.
 
Ngoja nikwasemee CUF na NCCR kuwa wao watsema HAPANA...Halafu nikwambie tu kuwa msema kweli ni sanduku la kura baada ya daftari kuboreshwa......kati ya juni au julai 2015....hapo ndipo mtakapolia na kusaga meno mtakapoona NDIYOOOO...kwani wazalendo wa nchi hii wamekwisha kuelewa mbivu na mbichi..
Kura ya hapana imezidi kupata wafuasi na vyama vya siasa baada ya CHADEMA kutangaza wazi kuunga mkono kura ya HAPANA na ufunguzi kufanyika tarehe 14 kwa kongamano.

Kongamano litaoongozwa na viongozi wa CHADEMA , Profesa Lwaitama na mjumbe wa kamati ya kukusanya maoni Humphrey polepole.

Na hii imefanya watu waliojitoa waziwazi kuunga kura ya hapana kuongezeka baada ya askofu wa jimbo la rulenge askofu niwe mgizi kutangaza waziwazi.

Mtihani mkubwa bado hupo kwa baadhi ya vyama vilivyokaa kimya . Cuf na nccr katika umoja UKAWA.

Ambavyo havijasema lolote kama watashiriki au la
 
Hapo kwenye rangi nyekundu hujaeleweka. Sentenso ya pili tatizo lipo kubwa ingawaje umeamua kutoliona ingawaje una macho mazuri tena yanayomeremeta.Ni nadra sana kura za wananchi zilizo kinyume na matakwa ya watawala kuheshimiwa na kubeba maana halisi ya mpiga kura. Tume ya uchaguzi ni ileile inayoteuliwa na mpigiwa kura. Na wewe unajua fika ' Amlipaye mpiga zumari, ndiye huchagua wimbo' Haiwezekani kama Jakaya Mrisho Kikwete ndiye anayeteua Tume ya uchaguzi na anataka Rasimu hii ipite, itashindwa kupita. Hata ungalikuwa ni wewe ni lazima ungehakikisha unateua watu ambao hawawezi kukuangusha tena kwa ubinafsi ulionao ungejiteua wewe mwenyewe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ili uhakikishe mambo yako yanapita kiulaini. Tatizo ndiyo hili kubwa, mengine yote madogo. Kwa kuwa wewe ni jinsia tofauti na mimi, hata yale ninayoyaona makubwa wewe unayaona madogo na niyoyaona madogo wewe kwako ni sawa na mlima kilmanjaro
Katiba ya taifa ilikuwa Na bunge lake nani aliwatuma wawakilishi wenu wapokea bungeni?

Na itarudi mitaani na una haki ya kuikataa au kuikubali, tatizo lako ni nini?
 
Ngoja nikwasemee CUF na NCCR kuwa wao watsema HAPANA...Halafu nikwambie tu kuwa msema kweli ni sanduku la kura baada ya daftari kuboreshwa......kati ya juni au julai 2015....hapo ndipo mtakapolia na kusaga meno mtakapoona NDIYOOOO...kwani wazalendo wa nchi hii wamekwisha kuelewa mbivu na mbichi..

hayo matumaini yenu magamba mimi na wenzangu wanaojielewa -HAPANAAAA!!
 
Hapo kwenye rangi nyekundu hujaeleweka. Sentenso ya pili tatizo lipo kubwa ingawaje umeamua kutoliona ingawaje una macho mazuri tena yanayomeremeta.Ni nadra sana kura za wananchi zilizo kinyume na matakwa ya watawala kuheshimiwa na kubeba maana halisi ya mpiga kura. Tume ya uchaguzi ni ileile inayoteuliwa na mpigiwa kura. Na wewe unajua fika ' Amlipaye mpiga zumari, ndiye huchagua wimbo' Haiwezekani kama Jakaya Mrisho Kikwete ndiye anayeteua Tume ya uchaguzi na anataka Rasimu hii ipite, itashindwa kupita. Hata ungalikuwa ni wewe ni lazima ungehakikisha unateua watu ambao hawawezi kukuangusha tena kwa ubinafsi ulionao ungejiteua wewe mwenyewe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ili uhakikishe mambo yako yanapita kiulaini. Tatizo ndiyo hili kubwa, mengine yote madogo. Kwa kuwa wewe ni jinsia tofauti na mimi, hata yale ninayoyaona makubwa wewe unayaona madogo na niyoyaona madogo wewe kwako ni sawa na mlima kilmanjaro

Katiba ya taifa ilikuwa na bunge lake, nani aliwatuma wawakilishi wenu wapotee bungeni?

Na itarudi mitaani na una haki ya kuikataa au kuikubali, tatizo lako ni nini?
 
'''''''''''''''''''''
nasema hapana ina maana gani , kwani hutaki hata haki ya kuishi , kuabudu , kusoma , kuishi , kuenzi muungano , kuilinda Tanzania kwa gharama yoyote , Demokrasia , haki za binadamu kwa ujumla ,n.k. Naomba unieleweshe ili ikae vizuri . Na , tusaidie vipi ambavyo ni hapana kwenye katiba iliyopendekezwa ili tusije tukabatizwa hapana kw kila kitu tuakaonekana ni wehu kitaani .Please nieleweshe.

mkuu wananchi hatuipigii kura katiba kifungu kwa kifungu hivyo hata kama ibara moja ndo mbovu basi kura ni HAPANAAA! Hakuna figisufigisu hapa. Mimi nasema katiba ya sitta HAPANA
 
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
kwa kweli , tayari nimeanza kukuelewa kumbe lengo la kura yako ya hapana unataka madaraka ya Raisi yapunguzwe . Sasa yapi yapandishwe na kwa namna gani? Na pia , maridhiano ya kitaifa ulitaka yafanyikeje , kwani mimi nilichokuwa nafahamu maridhiano yalikuwa yakifanyikia Bungeni na wakati mwingine hata mzee alithubutu kuwasilikiza na kusikilizana na kuafikiana masualam ambayo yalikuwa yakiwa kwenye maudhui ya pa,moja kwa vyama vya siaa vyote vilivyounda TCD . So mbali na maridhiano hayo ulitaka yaweje ? au kilichokuwa kifanyike ni kukubaliana na matakwa ya mlengo fulani tu au iweje . Aisee naomba tsaidiane ili tuwe pamoja ili nami nitoke na kura kama yako , ila hadi sasa kwa kuwa nalipenda Taifa langu bado sijashawishiwa, hapo naona kama main point zako kama zote zilijibiwa na majibu yaka sahishwa siku nyingi. Som lets leave politics , twende na uhalisia . Ni yepi yanayoboa kwenye katiba pendekzwa kama kuna kipendele kinaruhusu masuala ya kuwekezana ndani au kuuana au kutoabudu au kutoheshimiana au kuruhusu ufisadi au kuruhusu kubakana au kugombana au kuibiana au kutoruhusu mfumo wa vyama vingi au n.k? twende pamoja kwa ushauri safi na wakitaalamu na kisheria ila siyo wa kisiasa ili nielewe nisipotoshwe...:deadhorse::flame::third:

hujielewi.
 
hivi ni lini Dr Lwaitama amepata Uprofesa? Maana najua mpaka anastahafu kufundisha pale mlimani alikuwa ni Dr
 
Pili katiba pendekezwa iliyopitishwa zaidi na CCM, imeondoa hukumu ya kifo.eti ni haki ya mtu kuishi, sasa ukifuatilia mauwaji ya walemavu wa ngozi (albino) lazima uifikirie hukumu ya kifo iwepo, ni kweli kabisa watu wengi huuwa kwa bahati mbaya , mfano kumfuma mtu anamenya mke wake, kujiteteaa ndani ya kipigo cha majambazi , ugomvi tu wa kawaida inafikia mtu anamuuwa mwenzake. n.k. . Ingalao katiba pendekezwa ingefafanua wanaoondolewa adhabu za vifo akina nani, Wanaouwa albino hakuna sababu yoyote ya kuwaondolea adhabu hii kwani ni stahiki yao kabisa. Hata misamaha ya rais hua inabagua, huwa wanasema rais kasamehe wafungwa wenye makosa fulani makosa mengine kama ubakaji na wizi wa silaha huwa hawanufaiki na misamaha hiyo, vivyo hivyo katiba ingetamaka adhabu ya kifo imeondolewa kwa mauwaji wengine lakini wanouwa albino adhabu hiyo iko pale pale. Kwa kipengele hicho tu kweli zeluzelu mwenye ulemavu wa ngozi ataipigia NDIYO katiba hii ya CCM?

Sio kweli. Hukumu ya kifo haijaondolewa na katiba pendekezwa. Ila haki ya kuishi imetambuliwa katika Ibara ya 32
 
Back
Top Bottom