Kura 2011 nchini Russia; Putin arudi mamlakani!

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
Hi shughuli ya Putin na mwenzie ni kimeo yaani
sijui hii democrasia yao iitweje kama vile maigizo
Juzi Putin alikua Rais anataka tena agombee
awe rais kipindi kijacho sasa sijui medvedev atakua
waziri mkuu wake ?
 
UPDATES LEO TR 11/12/2011
MAMBO YA MIDDLE EAST YANATOKEA TENA HUKO URUSI:
waandamanaji wameipa serikali ya urusi siku chache mpaka tarehe 24/12 iwe imefanya mambo yafuatayo
1.Putin a resign
2.uchaguzi ufanyike upya
3.wafungwa wa kisiasa waachiwe wote bila masharti
4.wezi wa kura waadhibiwe...
wasipotekeleza haaya ndani ya wiki mbili wanaitisha maandamano mengine ambayo yatahudhuriwa na watu zaidi ya 150,000.
hiyo hapo chini ni nembo yao inamaanisha revolution..
z_13b8079b.jpg z_13b8079b.jpg
 
Na warusi wanasemaje? If they are happy, what else could we say? Happy Putin happy Russia
 
huu utaratibu wa miaka 10 urais haufai kwetu africa,kila rais akija anajifunza miaka 5 ya mwanzo kisha 5 ya kufisadi hatutapata maendeleo!embu fikiri kuna sababu gani ya kumtoa kagame rwanda kisa eti miaka 10 imeisha iwapo nchi inasonga mbele?
 
ni democracy kwa wazungu! lakini ingefanya afrika midege ya NATO isingecheleweshwa
 
Ilikuwa ni mipango ya Putin kurudisha uchumi wa Urusi uwe na nguvu kama zamani na yeye anauchungu sana kwa kuanguka kwa ujamaa wa kirusi hivyo anataka kuurejesha. Urusi ikiwa ni supplier wa gas Ulaya yote atatumia gas na makaa ya mawe kama njia za kujenga uchumi.
 
Hata mi ninamkubali Putin, acha aendelee kuongoza nchi, akitoka kwa mara ya pili yule mwenzake anakuwa rais tena! Hadi warusi waheshimike tena.
 
Hiyo ndiyo inaitwa Russian Democracy ni tofauti na ile ya umagharibini. Ila mi sioni shida kwasababu warusi wanampenda sana na katika katiba yao kikomo cha kugombea uraisi ni miaka miwili mfululizo ila hakuna panapo sema huwezi kugombea baadae.

Ila huyu jamaa kwakweli tunamuhitaji katika dunia hii ili kuleta uwiano na nchi za kimagharibi.
 
Ngoja awape kazi wamarekani...jamaa ana ambitions kubwa kwa nchi yake na ni patriot mzuri sana,nazikubali sana siasa zake
 
na Putin keshatangaza vita na marekani ...anawamind sana NATO kwa kumuua gadaffi
 
Ilikuwa ni mipango ya Putin kurudisha uchumi wa Urusi uwe na nguvu kama zamani na yeye anauchungu sana kwa kuanguka kwa ujamaa wa kirusi hivyo anataka kuurejesha. Urusi ikiwa ni supplier wa gas Ulaya yote atatumia gas na makaa ya mawe kama njia za kujenga uchumi.

hakuna kitu kama hiki na wala hana mawazo hayo yeye anachotaka ni kulinda rasilimali zao kwa nguvuzote..marekani na nchi za ulaya wanamendea sana rasilimali za urusi
 
Putin ni mkuda tu, angeweza kumsaidia Ghadaff kama angetaka, mana ana nguvu kubwa ya kijeshi na technology lakini akamwacha yule mzee akiuwawa sasa Russia inabaki kuwa mpiga debe tu kama walivyo wale mazezeta wanajiita AU...hawana madhara mbele ya mashetani ya Ulaya na Us...
 
hakuwa madarakani
 
Putin ni jasusi wa hali ya juu ktk shirika la kijasusi la urusi(KGB) na anaisumbua sana marekan ndo maana hatoki ktk madaraka ya juu ya uongoz ndani ya Russia!
 
Hata kwetu nafikiri inakubalika, katiba inakataza kuunganisha, lakini leo Mkapa ama mwinyi wakitaka kugombea wanagombea tena, ama nimekosea?

Katiba ya ccm ndo inachanganya tu, kwamba rais ndo mwenyekiti wa chama. Kwa kawaida chama kinachokuwa na wabunge wengi automatically kiongozi wake anakuwa waziri mkuu.
 
Ya kwetu yanatushinda tunabaki kuengelea ya wenzetu... sisi Wtz bhana mmmh
 
Hi shughuli ya Putin na mwenzie ni kimeo yaani
sijui hii democrasia yao iitweje kama vile maigizo
Juzi Putin alikua Rais anataka tena agombee
awe rais kipindi kijacho sasa sijui medvedev atakua
waziri mkuu wake ?
Hata Katiba ya Tanganyika huru, inamruhusu Mzee Mwinyi, Mkapa kugombea uraisi tena. Soma katiba uijue.
 
Back
Top Bottom