Kupungua kwa njiti za viberiti

kwa hiyo unashauri mukulu aunde tume kuchunguza thamani ya makanikia kwenye mabox ya viberiti?
 
Mimi ni mtumiaji wa hivi viberiti pasi kuangaria kampuni gani ina Tengeneza. Kwenye cover la nje kumeandikwa average sticks contents 40. Lakini kila nikinunua haifiki iyo idadi huishia 30 kwa 32. Maswali ya kujiuliza kwa nini kwenye cover waandike kwa lugha ya kigeni na sio kiswahili! Je hiyo sio mbinu ya kuwa ibia raia ambao hawajui kusoma na kuelewa hiyo lugha ya kigeni? Mimi naona huu ni wizi kama wizi mwingine tu
Du! Mkuu hadi unafikia kuhesabu njiti lazima ni sababau kati ya haya; either unavuta sigara, au a umeisoma namba.
 
Dah, ww ni mfuatiliaji zaidi ya Magu aisee..!! Kama unaweza ukahesabu mpk njiti za kiberiti, basi naweza nikaamini pasi na shaka kwamba huwa unahesabu mpk finyango za nyama kwenye sufuria jikoni...!!!
Pole sn kwa kazi nzito mkuu...!!!
Ulipaswa kumpa hongera na sio Pole!
 
Mara nyingi wanaofanya hivyo ni wenye maduka wasio waaminifu,wanapunguza njiti 5 na kuendelea ili wapate faida zaidi

Sasa wakipunguza hizo njiti huwa wanaziweka wapi ili waweze kuuza na kutengeneza hiyo faida unayosema?
 
Kuna mbinu nyingi mkuu,makasha mapya ya viberiti yanapatikana virahisi sana.
Sasa wakipunguza hizo njiti huwa wanaziweka wapi ili waweze kuuza na kutengeneza hiyo faida unayosema?
 
Mara nyingi wanaofanya hivyo ni wenye maduka wasio waaminifu,wanapunguza njiti 5 na kuendelea ili wapate faida zaidi
Una ushahidi Mkuu?.

Ni kweli wenye maduka ndio wanaopunguza au zinakuwa hazijatimia kuanzia kiwandani?.
 
Back
Top Bottom