Barua kwa mama

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
Mama, sio kila mwanga unaweza kuonesha au kuangaza kile king'aacho katika uso wa Dunia...

Japo macho yako yana angaza na kuona hata punje ya mchanga...ILA Kuna viang'aavyo huvioni sababu Kuna Maumbo na kingo zinazo tengeneza vimvuli vinavyo "Over shadow" the brilliant sparkels...

Vimvuli hivi vinaweza kutokana na majengo marefu yanayojengwa Kibinadamu au maumbile ya kiasili ya vitu virefu kama milima na miti mikubwa...

Sio kosa lako au la mfumo,kwako kupendekeza na kuchagua dhahabu zilizo na mng'ao wa rangi uipendayo .

Tunajua asilimia kubwa baadhi ya hizo dhahabu hazijajichimba ila zimetokana na ukoo au familia zenye MABULUDOZA.

Japo kua najua kuna dhahabu zinazo elea juu ya ardhi kiasili au,zimejikuta kuonekana hadharani sababu ya mmomonyoko wa ardhi iliyo bomoka kwa kuchimbwa na maji.

Pia najua kuna dhahabu ambazo zimejitutumua zenyewe na kuonekana juu ya ardhi na ukapendezwa na rangi yake na ukaziteua.

Je ni vipi kwetu sisi mama????Sisi ni "DHAHABU" ambao hatuna familia zenye mabuludoza ya kutuibua ardhini????,ni vipi sisi ambao tumejaribu kujitutumua ila ardhi inayotuzunguka ina MIAMBA isiyo sogea wala kutikisika ili tufike juu utuoneee???

Unadhani hatuumii pale yule uliyemteua anafanya ujinga na kukuangusha..ila bado kesho kwa busara ya kibinadamu unampa kitengo kingine kuamini amejirekebisha....

Je nchi hii ina limited human resources kiasi hicho hadi kufikia kufanya RENEWAL PROGRAM OF HUMAN RESOURCE??!

Kama tunafanyia "service" spare kwa gharama kubwa ambazo tunaweza kufanya "repair" tena kwa gharama nafuu zaidi...Tunaweza tukajitafsiri VIPI???

Anyway nabaki kujiuliza,utatuona lini sisi dhahabu tuliobanawa chini ya ardhi,au hauta tuona milele??...

Sababu kilicho chini ya ardhi kina kipi cha kujulikana??

Kilicho chini ya ardhi hata kama ni almasi kisipo kaa sawa mwamba wa kibinadamu uitwao Barabara ya Lami unaweza jengwa juu yake na kisije chimbwa milele maana lile eneo tayari halitaruhusu uchimbaji...

Mjinga gani anaweza amka asubuhi na Kuichimba Lami na akajitetea amepoteza dhahabu au Almasi hapo????

Au ndo ile kauli ya kusema hata ukichagua mwingine ni wale wale...

Kama jamii yetu haiwezi kujibadilisha kinguvu kazi kwa uadilifu wa nguvu kazi kwa lugha ya imani ya neno "walewale" inamaana kwa Jamii yetu ya watu wetu ni wale wale,mfano mimi ni wale wale,watoto wangu ni wale wale,ndugu zangu ni walewale,majirani zangu ni wale wale,mtaa wetu ni wale wale,wilaya yetu ni walewale na N.k N.k

Nini maana ya uzao mpya..kama tunang'ang'ania ukale...

Natamani ungefanya mabadiliko kidogo ungewaweka watu tofauti ili kuepuka makosa..

Kwamfano mimi mama Ukinipa eneo la kilimo na sayansi hakika huta juta.

Sema tu nipo katikati ya miamba nashindwa kujitutumua au nipo pembezoni mwa Jengo kubwa lenye kimvuli ambacho kinayafubaza macho yako..


Kwa kuanzia unaweza nipa wilaya moja tu kuanzia nikaigeuza kuwa MISRI YA TANZANIA KATIKA KILIMO,NA UFUGAJI NA SAYANSI.



Tuna mengi ya kuipa nchi yetu ila ndo hivyo,tupo katikati ya miamba au vimvuli giza.
 
Back
Top Bottom