Kupostiana status huu ushamba nani aliuleta? Nini objective yake?

Kupostiana status huu ushamba nani aliuleta? Nini objective yake?

Kila mtu na starehe yake - Waswahili.

Binaadam tupo tofauti yaani kitu wewe unakiona cha kiupuuzi mwenzako akifanya anaona raha mustarehe na kile ambacho wewe unaona very positive mwingine anaona cha KIBOYA.
 
View attachment 3698954

Mambo ya kupostiana nayachukulia kama kuchapisha taarifa binafsi na kwenda kuzibandika kwenye miti ya mtaani kwenu. Yaani ili kuonyesha mkeo unampenda sana basi unaandika tangazo I love you my wife, unaenda kubandika kwenye kuta zote za kijiji na mbao za matangazo. Huu ndio uhalisia wake.

Sasa huu ni ushamba mwingine wa kawaida kabisa. Nani alileta huu ushamba?

Huu ushamba unatuletea kero Mamasta kuonekana mbona haukomenti status zangu? Mbona hujapost happy birthday ya mtoto? Mbona hunipost? Pumbavu kabisa

Mwanaume mzima na akili zako unampost mkeo status, nini malengo yako? Unamnadi ama vipi? Cant you text her i love you, haitoshi?

Kwa hiyo, ili kuondoka na hii kero, nilichagua kumute whatsapp status zooote, kasoro wale tu wanaopost matangazo ya biashara au nasaha za Mungu.
Mkuu kila mtu afanye kile nafsi yake inapenda huo ndio utamu wa maisha yenyewe,maisha yasingekuwa na maana kama watu wote tungekuwa tunafanya vitu vinavyofanana.
 
Back
Top Bottom