Kupita bila kupingwa - is this democracy too?

MMkjj narudi tena kukupata hongera kwa hoja.
Nilikuwa napanga kususia kusoma makala zako Raia Mwema sasa nimesitisha uamuzi huo.

Ila ninaushauri wewe kama mpiganaji katika harakati ya kukuza demokrasia nchini haitatosha barua hii kuwa kwa mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi,ungelifanya juhudi iwafikie vyama vyote vya siasa hasa yale yaliyoshiriki katika Uchaguzi wa mwaka huu iliwaweze kutambua kuwa kuna wanachama wao wamenyimwa haki.

Kwa Chadema ambayo mimi ni mumini wake ningeliwashauri kutumia nafasi hii kufungua kesi mahakamani kwa niaba ya wanachama/wapigakura wao kwenye majimbo yote ambayo wagombe wa ubunge wamepitishwa bila kupigiwa kura na wapigakura halali ambao kisheria ndio wanaotabulika wa tarehe 31/10/2010.
 
Asante MM, hata mimi naona kuna hoja ya msingi. Kuna haja ya kuifanyia barua hiyo kazi
 
Tatizo la kesi yoyote sasa hivi ya Kikatiba kufunguliwa ni maamuzi ya ya Mahakama ya Rufani kuhusu wagombea binafsi.. nadhani wamefanya almost impossible kufungua kesi yenye kuchallenge the constitutionality ya sheria yoyote ile.
 
22nd November 2010 | Nipashe

Chama cha Democratic Party (DP) kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopita bila kupingwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi uliopita kwa kuwa ushindi wao sio halali.

Kadhalika, chama hicho kimesema kinatarajia kuifikisha Serikali kwenye Mahakama.

Mwenyekiti wa DP, Christopher Mtikila, alisema jana kuwa maandalizi ya kufungua kesi hiyo yamekamilika na kwamba wiki hii wataifungua rasmi.

Wabunge hao hawakupigiwa kura kwa kuwa vyama vya siasa havikusimamisha wagombea wa kushindana nao kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mtikila alisema chama chake kitafungua kesi ili kuiomba mahakama itafsiri sheria ili kuona kama wabunge hao wanastahili kuwa wawakilishi wa wananchi wakati hawakuwachagua kupitia masanduku ya kura.

Kuhusu mgombea binafsi, Mtikila alisema hajakata tamaa na anaamini kuwa mahakama ya Afrika itakayokutana jijini Arusha itatenda haki na hivyo kuwapa wananchi uhuru wa kuchagua mtu ambaye hakupitia chama chochote.

Mwaka huu Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali kesi ya kudai mgombea binafsi ambapo jopo la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu, Augostino Ramadhani lilitaka shauri hilo likajadiliwe bungeni kwa kuwa hilo ni suala la kikatiba.

Aidha, Mtikila aliwasifu wabunge wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kwa kususia hotuba ya uzinduzi wa Bunge la Kumi mjini Dodoma wiki iliyopita.

Alisema kitendo hicho ni cha kijasiri na kwamba hiyo ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa mtu ambaye wanamini alipata ushindi bila uwazi.

Aliwashangaa wanachama wa CCM wanaopendekeza wabunge hao wafukuzwe bungeni kwa kosa la kutoka nje ya ukumbi wakati Rais alipohutubia na kusema kuwa kitu hicho hakiwezekani kisheria.

Alisema watu wanaotoa mawazo kama hayo uelewa wao ni mdogo kwa kuwa hata Rais hana uwezo wa kumfukuza kazi mbunge yeyote, ingawa yeye anaweza kufukuzwa na wabunge.

"Mbunge na Rais ni watu wanaofanya kazi zinazofanana kwa kuwa Rais ni sehemu ya Bunge hivyo CCM isipotoshe umma kwa propoganda za kisiasa," alisema.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa ni pamoja na Filikunjombe (Rudewa), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Mizengo Pinda (Katavi), January Makamba (Bumbuli), Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Magharibi), Anne Makinda (Njombe Kusini), William Ngeleja (Sengerema), Philip Mulugo (Singwe) na William Lukuvi (Ismani).

Wengine ni Celina Kombani (Ulanga Mashariki), Nimrod Mkono (Musoma Vijijini), Gregory Teu (Mpwapwa), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) na Jon Ndugai (Kongwa).
 
hapo ndipo tunapoona upungufu mkubwa katika Wizara mama ya Katiba na Mambo ya sheria, hapo kama sheria itafata mkondo wake kuna uwezekano mkubwa wa hayo majimbo kurudiwa uchaguzi wake,

Mi nakumbuka, NILIWAHI kupiga kura kumchagua rais Ally Hassan Mwinyi, ilikuwepo picha yake na kivuli, Picha yake UNa tick Ndiyo na kivuli Hapana, sasa nikashangaa kuona kwa nini leo hii kuna wabunge ambao hawapigiwi kura, kwa nini isiwepo hiyo dizain tuliyotumia kumchagua mzee Ruksa?

Unajua hata kama ukipewa ndiyo au hapana, inakupa imani kuwa wananchi wangu wananipenda au la na kujua jinsi ya kuwajibika kwa ajili ya jimbo.
 
MwanaJF Mzee Mwanakijiji naungana na Great Thinkers WanaJF kukupongeza kwa kuchukua nafasi ya kipekee kuelimisha umma wa Tanzania juu ya mada hii ya msingi kuhusu haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania. Kwa unyenyekevu mkubwa natoa pongezi kwa kila mwanaJF aliyechangia na kuipa mada hii umuhimu wa kikipekee!

Mimi kwa mara ya kwanza nilisoma makala yako katika gazeti la Mwanahalisi, Jumatano, Septemba 17, 2010, Ukurasa wa 6 kichwa "Wabunge Waliobebwa ni Batili". Kwa thread hii ya leo nimetiwa moyo zaidi kuona kwamba kumbe ulikwishafika mbali zaidi kwa kumwandikia Barua ya Wazi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi mapema zaidi, Agosti, 27, 2010. Huu ni ushahidi tosha ni kiasi gani umetoa maisha yako kuona haki ya msingi si jambo la kufanyia mchezo katika taifa hili. Jitihada zako pia zimeonekana kwa kutuhabarisha juu ya hatua aliyofikia Rev Mtikila kwa mujibu wa gazetila IPP MEDIA Nipashe Jumatatu, Novemba, 22, 2010.

Kwa wanaJF wenye memory wanaweza kukumbuka miaka ya zamani sana katika jimbo moja la uchagu, kama sikosei, Korogwe?, ambapo wapigakura 2, kitu kama hicho, waligangamala mahakamani mpaka mbuge aliyekwisha dumu bungeni kwa muda mrefu kuvulivuliwa na mahakama ubunge!

Hili ni somo kwetu kwamba kama watakuwepo wapigakura wenye uchungu ambao hawatakuwa tayari kuona na kunyamazia serikali ya sisiemu ikinyang'anya kidhuluma wapigakura halali katika majimbo ya uchaguzi 19 haki yao ya kikatiba!!!. Hiki ni kitendo cha kinyama.

Kwa nchi inayopigia debe kuendesha utawala wa kisheria; na hata kuwa na Tume ya Haki za Binadamu.

Mimi naungana na wanaJF ambao wametupeleka katika hatua za kufungua kesi mahakamani kwa hoja za msingi bila kujali kwamba mahakama zitachakachuliwa au la. Hatuwezi kujua; Mungu anaweza kutuinulia majaji mfano wa marehemu Mwalusanya, na wengineo waliotoa maisha yao kuona haki inlindwa kwa gharama zote. Itakuwa ni kosa la kujutia kama tutaishia tu kwa hisia za mahakama kutotenda haki. Lalamiko la namna hii lije pale ambapo kesi imechakachuliwa, au haki imecheleweshwa!!.Aidha tusiogope gharama. Penye nia pana njia!

Pia naungana na wanaJF walioleta wazo la kuhamashisha vyama, hasa CDM ambao ni victim mkubwa- na pia taasisi zote za Haki ya Bindamu, pamoja na ile ya serikali-ile ya Jaji Manento!!!!!!!! Seriousness katika uhamasishaji itaipa jambo hili kuvuta hisia za watu wengi na taasisi nyingi na kulifanya jambo hili kuonekana kupata uzito kitaifa na hata kimataifa ili kupata msukumo wa kufanya wabunge husika kujutia tendo hilo.

MwanaJF Mwanakijiji naomba ukubali jukumu la kutuongoza katika mipango ya kufungua kesi, na uhamasishaji!
 
Last edited by a moderator:
wana Jf,

wote ni mashuhuda wa kilichotokea mwaka jana wakati wa uchaguzi. Mambo mengi yenye kufisha demokrasia nchini yalifanyika huku yakikingiwa kifua na baadhi ya sheria za uchaguzi zilizosimamiwa na tume ya uchaguzi ikishirikiana na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Mojawapo lilikuwa ni hili la kupita bila kupingwa kwa baadhi ya wabunge na madiwani. Baadhi ya wagombea walifikia hatua ya kuwafanyia wagombea wenza fitina ili waenguliwe na wao watangazwe kuwa wamepita bila kupigwa. Mfano mzuri ni kilichojiri mwanza kwenye jimbo la Nyamagana wakati Bw. Lawrence Masha alipotangazwa mshindi wa ubunge kwa kupita bila kupingwa huku mpinzani wake Wenje akiwa amewekewa pingamizi. Lengo hapa si kumnyooshea kidole bwana Lawrence masha, lakini madhaifu yote haya yanatokana na sheria iliyopo.

Dhana ya demokrasia ni pana sana na inakinzana na mantiki iliyokusudiwa na kifungu hiki cha sheria kilichoruhusu baadhi ya viongozi kupita bila kupingwa. Haiingiii akilini mtu kupita bila kupingwa pasi kupigiwa hata kura ya Ndiyo au Hapana. Embu tujiulize, Kwa hiyo nikiwa ni mgombea pekee niliyejitokeza kugombea baada ya kuwatisha wenzangu kwamba nitawaua endapo wataingia kwenye kinyang'anyiro; Je, ni haki mimi kupita bila kupingwa??? Je, mimi nitakuwa ni chaguo la hao watu ninaotaka kuwaongoza??? Jibu ni hapana hapana. Lakini je tutaendelea na hii sheria mpaka lini???

Nimeandika haya leo ili yafanyiwe kazi mapema iwezekanavyo, na lengo ni kubadili vifungu kama hivi mapema ili kunusuru hali iliyojitokeza kwenye chaguzi za mwaka jana na hivyo kuendelea kuimarisha demokrasia ambayo ni haki ya msingi ya kila mwananchi. Nasema hivo kwa sababu lolote linaweza tokea ndani ya hii miaka mitano, kwa mfano vifo au kuachia ngazi kwa hiari kwa wale walio chaguliwa na hivi kulazimisha chaguzi ndogo zifanyike.

Nawasilisha.
 
Kumbe kweli watu tunajifunza kutokana na vihoja. Yale ya Lau Marsha yadhibitiwe kabisa yasijejitokeza tena.
 
Hilo nalo neno ndugu yangu.

Kwa mtazamo wangu ni vyema ku-kawa na mchakato mpya na huru baada tu ya kugundua kuwa kuna mgombea kabaki peke yake katika jimbo husika.

Pia sheria ipitishwe kuvibana vyama, kusimamisha wagombea katika kila jimbo... hii nikiwa na maanisha vile vinavyokuwa havina pesa vishurtishwe kuunga mkono chama kingine kwa maandishi ili kuonyesha ushiriki wao katika uchaguzi.

Hii pia naiona inatengenezwa na Chama tawala kwa kuwa sina uhakika kama kuna sehemu alipita mgombea wa upinzani bila ya kupingwa... so hoja yangu hapa ni kuwa VIGEZO vinavyotumika katika kumuengua mtu viweze kuwa na nguvu kuliko "MAKANDOKANDO" yanayotumika kama hoja ya kumuengua mtu.

KWa hoja hii... sheria ia itunge KUWABANA wagombea wanaojitoa kugombea wakati wakiwa tayari wameteuliwa na vyama vyao kwa gharama amabazo kwa sasa huwa zinaonekana zinapotea, kwa kuwa naamini hata pesa zinazotumika katika kura za maoni ndani ya vyama ni za walipa kodi kwa kuwa vyama vinapokea ruzuku ambazo ni pesa zetu... ni vyema iwepo sheria kuwawajibisha ikiwa ni pamoja kuanagalia mianya ya rushwa

Mtazamo wangu
 
Katika uchaguzi mkuu uliopita kuna wabunge wapatao takribani 20 hivi, wote kutoka CCM waliopitishwa kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa ibara ya 66 ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania tunao wabunge wa aina tano; ikiwa ni pamoja na wale waliochaguliwa kuwakilisha majimbo, wabunge wa viti maalumu, wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la wawakilishi, wabunge kumi wa kuteuliwa na rais, na mwana sheria mkuu wa serikali.

Hao wabunge wa kupita bila kupingwa hawapo; kitu kilichotakiwa ni kwamba kama mgombea hakupata mpinzani alitakiwa apigiwe kura ya hapana au ndio, ndipo akubalike kuwa mbunge anayewakilisha jimbo na si vinginevyo.
 
Byendangwero

Hivi katika hili yule anayejiita mchungaji mtikila hajatuuza??????? Huyu bila shaka atakuwa kapewa donge nono kumzima nywiiii!!!!!!!! Yule ni mtu dili kwa kila jambo!!!!!!! Kama siyo kweli basi ajitokeze. Vingine tutawataka Pipooooooooooooooooooooos pawaaaaaaaaa watuambie jibu la hili.!

Tz ni nchi ya utawala wa sheria bwana-tusimruhusu pinda na makinda wapindishe taratibu za nchi na kufanya watakavyo.
 
Last edited by a moderator:
Let me refresh your memory katiba hairuhusu hata kidogo kwani kuna aina tano tu za wabunge chini ya katiba soma ibara 66 (1) (a) mpaka (e). Sheria ya uchaguzi inaleta chini ya kifungu 44 aina nyingine ya wabunge ambao katiba haijawagusia kabisa. Zaidi ya hiyo sheria imenyang'anya haki ya msingi ya raia kuchagua wabunge, Kwa hiyo pamoja na kukosa wapinzani ilitakiwa wapigiwe kura na wakubaliwe au wakataliwe na raia.

Sasa wewe huoni kama vifungu vya katiba vimepingana?!
 
Watu tunakumbushia tu kuwa hakuna jipya linalotokea sasa ambalo halikujadaliwa kwa kina hapa. Linapojirudia sisi wengine hata kulalamiki hatulalamiki watu wajue kwanini.
 
Kama mtu anaweza kuangushwa na konyagi alafu akatangazia dunia ameangushwa na wasiojulikana bila shaka hawezi kushindwa kutunga orodha feki ya watu kupita bila kupingwa.
 
Back
Top Bottom