Kupima Ngoma Inahitaji Ujasiri la Sivyo Utakimbia Majibu

^^
Ha ha Simplicity Umenipa furaha namna ulivyowasilisha tukio lako! Ni ujumbe murua unaofaa yeyote anayejijali na kuwajali wengine.
Nami ntaenda tena kupima
^^
 
Last edited by a moderator:
Jana nilienda kupima HIV pale Angaza Mnazi MMoja. Lengo ilikuwa nijijue hali yangu kiafya ili niadhimishe siku ya ukimwi duniani "while I'm informed".

Nimengia hapo angaza saa 2 asubuhi, nikakuta kundi la watu wa kutosha tu. Basi ndio tumewekewa video kwenye TV wakati tukisubiri vipimo (Video ilikuwa na mikwara mingi sana kuhusiana na mambo ya ukimwi). Baadaye kidogo, akaja dada mmoja, ni mrembo, katupa semina na watu wakauliza na kujibu maswali kadha wa kadha.

Angaza sio mchezo! Nilikuwa mtu wa kati katika mfuatano wa kwenda kupima. Waliotangulia, kuna watu walitoka wanacheka, wengine walitoka na nyuso zimebadilika, wengine wanalia, n.k.!

Muda huo, wakati wengine tukisubiria kwenda kupima, wenye roho nyepesi walitoka na kusepa kimojaa. Ukitoka, ilikuwa ni lazima utoke na macho ya watu wote waliokuwepo hapo! Watu wakisikia purukushani kama za mtu kutaka kutoka, hasa kama alikuwa amekaa viti vya nyuma, walikuwa wakigeuka kimyakimya bila kusema chochote na kukupiga macho paa!

Mie nilitoka kwenda kupokea simu nje, walinikata macho, halafu nikasikia wadada fulani wawili wakisema amejibeep huyo! Dah, watu tulikuwa hatuaminiani kabisa! Niliwajibu, kwa taarifa yenu narudi!

Ikafika zamu yangu kwenda kuchukuliwa damu. Maongezi yangu na Dada mtoa damu yakawa hivi:

Dada: Karibu, kaa kwenye kiti (sikusalimia, maana hapo unasahau mengi), jina lako, taja majina matatu
Mimi: Simplicity. XXXX YYYY
Dada: Umri wako
Mimi: XXX
Dada: Unaishi wapi?
Mimi: Dar, Nimehamia Mbezi Kimara hivi karibuni
Dada: Kiwango chako cha elimu?
Mimi: Nimemaliza chuo, VETA
Dada: Umeoa/una mke?
Mimi: Sijaoa/sina mke
Dada: Unaishi na mwanamke/wanawake?
Mimi: Hapana, naishi mwenyewe
Dada: Namaanisha una mahusiano ya kimapenzi na wanawake?
Mimi: Hapana, nina mahusiano tu ya kawaida
Dada: Una mchumba/girlfriend?
Mimi: Sina mchumba wala girlfriend
Dada: Mara ya mwisho kushiriki ngono ilikuwa lini?
Mimi: Sijawahi kushiriki ngono
Dada: Wewe kaka, acha masihara, umekuja kufanya mzaha eee! Tafadhali umeshiriki ngono lini, mara ya mwisho, na ulitumia condom au haukutumia?
Mimi: Labda zamani, wakati tunacheza michezo ya utotoni, na sidhani hata kama nilimfanya mdada fulani enzi hizo tunacheza michezo ya baba na mama, kondomu sidhani kama zilikwepo enzi hizo. Sikumbuki chochote
Dada: Wewe kaka, naona umekuja kunipotezea muda! Sasa kama hujashiriki ngono unapima nini?
Mimi: Kwani ngoma inaambukizwa kwa kujamiana tu!
Dada: (Kwa hasiri kidogo) Haya leta mkono nichukue damu, na ukutwe unayo sasa!
Mimi: (Nikasema huyu dada hana maana, asije akanibambikizia status, sikumjibu kitu, nikajisemea, la asije akafanya makusudi)
Dada: chukua hiki kikaratasi kina namba yako, subiri nje utaitwa

Nikawa nimetoka zangu nje, ila dah, moyo ukawa unaenda sana mbio, kama mnavyojua, angaza huwezi kujiamini.

Baada ya kama dk 7, nikaitwa kwenda kuchukua majibu.

Dada: Karibu (Dada akawa mpole sana, halafu ananiangalia kwa huruma)
Mimi: A- h sa nte (Maneno yananikwama kooni!)
Dada: Umesema hujawahi kufanya ngono?
Mimi: Samahani dada wewe nipe mie majibu niende zangu
Dada: Kwa hiyo ulikuwa unanitania?
Mimi: Utani gani! Sijawahi kufanya ngono, na kama nimefanya sikumbuki ni lini
Dada: Subiri (katoka nje akamwita dada kutoka chumba kingine, nikasema, dah, majibu sio! Anatafuta ushauri namna ya kunipakulia au? Karibu nisepe alivyotoa huo mwanya lakini nikapiga moyo konde na kuamua kusubiria, baada ya kama dakika 2, Dada akarudi). Wewe kaka umeamua kwa moyo mweupe kabisa kuja kupima?
Mimi: (Nikasema, haya maswali kulikoni, kuna nini?) Ndio
Dada: Uko tayari kupokea majibu?
Mimi: Ndio
Dada: Unatambua kukutwa na maambukizi ya ukimwi sio mwisho wa kuishi?
Mimi: Ndio (Nikasema dah, something detected!)
Dada: Umeshawahi kusikia/kupata ushauri nasaha jinsi ya kuishi na virusi vya ukimwi?
Mimi: Nilishawahi kusikia radioni (Karibu nimnyang'anye daftari ambalo lilikuwa na majibu, najiuliza huyu kwa nini hanipi majibu! Nikazidi kuwa mpole)
Dada: Una watu wowote wanaokutegemea?
Mimi: Dada tafadhali naomba majibu kama unanipa
Dada: Sasa wewe unataka kupewa bila kufuata utaratibu!?
Mimi: Bwana mie nimechoka na maswali hayaishi (Nikamjibu swali lake)
Dada: Iwapo umekutwa na maambukizi ya ukimwi utafanyaje?
Mimi: Hakuna kitu kama hicho (Alicheka wakati mie jasho linanitoka!)
Dada: Wewe kaka una vituko! Hakuna si usingekuja sasa?
Mimi: Siwezi kuwa na uhakika kihivyo, ndio maana nimekuja!
Dada: Nakupa majibu kama utahitaji ushauri au elimu yoyote kuhusiana na ukimwi ofisi zetu ziko wazi Jtatu - Jumamosi, kuanzia saa mbili - saa nane mchana. Tafadhali tumia kondomu wakati wa kukutana kimwili.
Mimi: Naomba majibu (Mood yangu hapo imebadilika kabisa)
Dada: Kwa sasa hivi hauna maambukizi yoyote ya ukimwi, rudi tena kupima baada ya miezi mitatu.

Alivyomaliza tu kuongea sikumwaga, nduki nje, hakuna cha kwa heri wala nini! Kumbe nyuma nimesahau simu. Kidogo mtu ananikimbilia wee kaka umesahu simu yako. Dah huku jasho likiwa linanitoka, watu pale walinipiga macho, na wanaweza kuamini tofauti!

Angaza sio sehemu ya kufanyia majaribio, nenda kama umeamua kweli na tegemea chochote!

Dah, pamoja na kwamba jasho lilinitoka, lakini baada ya kuambiwa sina maambukizi nilitoka mwepesi kama air force one, huku moyo mweupe! Nilienda sehemu nikanunua grand malt, nikawa nakunywa huku nikipumzika taratibu!

Dah, kutokujua status yako ni zigo la misumiri, lakini kupima nako inahitaji ujivue ufahamu!

Nenda kapime ujue uwe huru.

Starehe: Ferooz ft Proffesor Jay - Starehe - YouTube

CC: watu8 lara 1 Kongosho Kaunga charminglady mdida The Boss tinna cute Himidini mwe----- Washawasha nanjilinji MadameX madameA Madame B King'asti Dublin musubati Smile Sista sister Mshinga Mashaxizo Mtambuzi MziziMkavu gfsonwin HorsePower AshaDii mimi49 Heaven on Earth Lady doctor KOKUTONA Nyani Ngabu Eiyer Boflo SnowBall snowhite Mapi

na wana MMU wengine wote, hasa hasa moderators, pamoja na kusimamia JF ni vizuri mkajua status zenu.

Umesomeka MKUU,
Hongera kwa kujua HIV status yako.
 
kuna kaka mmoja kazini kwao huwa wanapimwa.siku alivyoenda kupima na wafanyakazi wake,walikuwa kama 20 na wengine ni watu wazima,9 walikuwa positive.huu ugonjwa wacha tu.kuna sekta nyengine kazini lazima mpimwe.
 
Mkuu umenikumbusha na mimi nitakwenda kupima tena mwaka jana nilipima ukimwi na afya yangu kwa ujumla nikakuta nipo Negative na wiki hii nitakwenda kupima tena kwa sababu Happybirthday yangu inakuja tarehe 6 mwezi huu hahahhahah pole sana upo Negative wewe mkuu.@Simplicity.hongera sana.

Negative mkuu.
 
Eiyer acha kabisa, ngoma ipo kwenye angle nyingi!
kisukari hiyo ofisi yenu kiboko, maana kama 50% hivi
PLL huwezi jua umeambukizwaje, labda kwa kiss, kapime tu
Ngalikihinja issue sio macho, ni majibu hasa yakiwa big result, mbona waweza kutwa umezirai
 
Last edited by a moderator:
Eiyer acha kabisa, ngoma ipo kwenye angle nyingi!
kisukari hiyo ofisi yenu kiboko, maana kama 50% hivi
PLL huwezi jua umeambukizwaje, labda kwa kiss, kapime tu
Ngalikihinja issue sio macho, ni majibu hasa yakiwa big result, mbona waweza kutwa umezirai
Halafu na maporsija yao yale ndo yanatia presha tu.... Mara ukikutwa nao utafanyaje, mara ushauri nasaa mara sijui nini... fulu kutiana hofu na kisebusebu

 
Mkuu Mentor kujipima mwenyewe labda uchukue damu uiweke kwenye kipimo, halafu ulale kwanza, ukiamka unachungulia taratibu halafu kwa mbali, kuikabili damu yako inasoma big results utajilaumu sana. Utasema bora ningepimwa angaza labda nimekosea!
Ngalikihinja ndio maana wakati wa prosija zao watu kibao walisepa kwa kujibeep, mtu anajifanya anapokea simu, huyoo swiiiiiii.
ladyfurahia mie nimepima, nipo vizuri
 
Last edited by a moderator:
hahaha hii stori imenichekesha wallahi...................kupima ukimwi sio mchezo wallahi

Yaani, sijui watu wa angaza wanakabilianaje na watu ambao matokeo yao yanasoma big results! Pale kuna kujeruhi mtu kwa kisingizio cha kukubambikia status unajua!
 
kwann upate shida lkn??
siku hizi unatembea na KIPIMO mwenyewe, mfukoni kama vile mtu unavyotembea na MRDT
 
Mkuu Mentor kujipima mwenyewe labda uchukue damu uiweke kwenye kipimo, halafu ulale kwanza, ukiamka unachungulia taratibu halafu kwa mbali, kuikabili damu yako inasoma big results utajilaumu sana. Utasema bora ningepimwa angaza labda nimekosea!
Ngalikihinja ndio maana wakati wa prosija zao watu kibao walisepa kwa kujibeep, mtu anajifanya anapokea simu, huyoo swiiiiiii.
ladyfurahia mie nimepima, nipo vizuri
Ila kuna wakati huwa nashangaa sana... Yaani mtu fulu hofu kupima ukimwi, lakini maleria haogopi... Ukicheki unaweza ukakuta maleria inauwa sana kuliko ukimwi
 
Simplicity , kwa mujibu wa hii story yako napata picha kuwa hapo Angaza kuna baadhi ya wahudumu hawana weledi kabisa. Ni story ya kweli hii?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom