Kupima Ngoma Inahitaji Ujasiri la Sivyo Utakimbia Majibu


J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,086
Likes
11
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,086 11 0
Jana nilienda kupima HIV pale Angaza Mnazi MMoja. Lengo ilikuwa nijijue hali yangu kiafya ili niadhimishe siku ya ukimwi duniani "while I'm informed".

Nimengia hapo angaza saa 2 asubuhi, nikakuta kundi la watu wa kutosha tu. Basi ndio tumewekewa video kwenye TV wakati tukisubiri vipimo (Video ilikuwa na mikwara mingi sana kuhusiana na mambo ya ukimwi). Baadaye kidogo, akaja dada mmoja, ni mrembo, katupa semina na watu wakauliza na kujibu maswali kadha wa kadha.

Angaza sio mchezo! Nilikuwa mtu wa kati katika mfuatano wa kwenda kupima. Waliotangulia, kuna watu walitoka wanacheka, wengine walitoka na nyuso zimebadilika, wengine wanalia, n.k.!

Muda huo, wakati wengine tukisubiria kwenda kupima, wenye roho nyepesi walitoka na kusepa kimojaa. Ukitoka, ilikuwa ni lazima utoke na macho ya watu wote waliokuwepo hapo! Watu wakisikia purukushani kama za mtu kutaka kutoka, hasa kama alikuwa amekaa viti vya nyuma, walikuwa wakigeuka kimyakimya bila kusema chochote na kukupiga macho paa!

Mie nilitoka kwenda kupokea simu nje, walinikata macho, halafu nikasikia wadada fulani wawili wakisema amejibeep huyo! Dah, watu tulikuwa hatuaminiani kabisa! Niliwajibu, kwa taarifa yenu narudi!

Ikafika zamu yangu kwenda kuchukuliwa damu. Maongezi yangu na Dada mtoa damu yakawa hivi:

Dada: Karibu, kaa kwenye kiti (sikusalimia, maana hapo unasahau mengi), jina lako, taja majina matatu
Mimi: Simplicity. XXXX YYYY
Dada: Umri wako
Mimi: XXX
Dada: Unaishi wapi?
Mimi: Dar, Nimehamia Mbezi Kimara hivi karibuni
Dada: Kiwango chako cha elimu?
Mimi: Nimemaliza chuo, VETA
Dada: Umeoa/una mke?
Mimi: Sijaoa/sina mke
Dada: Unaishi na mwanamke/wanawake?
Mimi: Hapana, naishi mwenyewe
Dada: Namaanisha una mahusiano ya kimapenzi na wanawake?
Mimi: Hapana, nina mahusiano tu ya kawaida
Dada: Una mchumba/girlfriend?
Mimi: Sina mchumba wala girlfriend
Dada: Mara ya mwisho kushiriki ngono ilikuwa lini?
Mimi: Sijawahi kushiriki ngono
Dada: Wewe kaka, acha masihara, umekuja kufanya mzaha eee! Tafadhali umeshiriki ngono lini, mara ya mwisho, na ulitumia condom au haukutumia?
Mimi: Labda zamani, wakati tunacheza michezo ya utotoni, na sidhani hata kama nilimfanya mdada fulani enzi hizo tunacheza michezo ya baba na mama, kondomu sidhani kama zilikwepo enzi hizo. Sikumbuki chochote
Dada: Wewe kaka, naona umekuja kunipotezea muda! Sasa kama hujashiriki ngono unapima nini?
Mimi: Kwani ngoma inaambukizwa kwa kujamiana tu!
Dada: (Kwa hasiri kidogo) Haya leta mkono nichukue damu, na ukutwe unayo sasa!
Mimi: (Nikasema huyu dada hana maana, asije akanibambikizia status, sikumjibu kitu, nikajisemea, la asije akafanya makusudi)
Dada: chukua hiki kikaratasi kina namba yako, subiri nje utaitwa

Nikawa nimetoka zangu nje, ila dah, moyo ukawa unaenda sana mbio, kama mnavyojua, angaza huwezi kujiamini.

Baada ya kama dk 7, nikaitwa kwenda kuchukua majibu.

Dada: Karibu (Dada akawa mpole sana, halafu ananiangalia kwa huruma)
Mimi: A- h sa nte (Maneno yananikwama kooni!)
Dada: Umesema hujawahi kufanya ngono?
Mimi: Samahani dada wewe nipe mie majibu niende zangu
Dada: Kwa hiyo ulikuwa unanitania?
Mimi: Utani gani! Sijawahi kufanya ngono, na kama nimefanya sikumbuki ni lini
Dada: Subiri (katoka nje akamwita dada kutoka chumba kingine, nikasema, dah, majibu sio! Anatafuta ushauri namna ya kunipakulia au? Karibu nisepe alivyotoa huo mwanya lakini nikapiga moyo konde na kuamua kusubiria, baada ya kama dakika 2, Dada akarudi). Wewe kaka umeamua kwa moyo mweupe kabisa kuja kupima?
Mimi: (Nikasema, haya maswali kulikoni, kuna nini?) Ndio
Dada: Uko tayari kupokea majibu?
Mimi: Ndio
Dada: Unatambua kukutwa na maambukizi ya ukimwi sio mwisho wa kuishi?
Mimi: Ndio (Nikasema dah, something detected!)
Dada: Umeshawahi kusikia/kupata ushauri nasaha jinsi ya kuishi na virusi vya ukimwi?
Mimi: Nilishawahi kusikia radioni (Karibu nimnyang'anye daftari ambalo lilikuwa na majibu, najiuliza huyu kwa nini hanipi majibu! Nikazidi kuwa mpole)
Dada: Una watu wowote wanaokutegemea?
Mimi: Dada tafadhali naomba majibu kama unanipa
Dada: Sasa wewe unataka kupewa bila kufuata utaratibu!?
Mimi: Bwana mie nimechoka na maswali hayaishi (Nikamjibu swali lake)
Dada: Iwapo umekutwa na maambukizi ya ukimwi utafanyaje?
Mimi: Hakuna kitu kama hicho (Alicheka wakati mie jasho linanitoka!)
Dada: Wewe kaka una vituko! Hakuna si usingekuja sasa?
Mimi: Siwezi kuwa na uhakika kihivyo, ndio maana nimekuja!
Dada: Nakupa majibu kama utahitaji ushauri au elimu yoyote kuhusiana na ukimwi ofisi zetu ziko wazi Jtatu - Jumamosi, kuanzia saa mbili - saa nane mchana. Tafadhali tumia kondomu wakati wa kukutana kimwili.
Mimi: Naomba majibu (Mood yangu hapo imebadilika kabisa)
Dada: Kwa sasa hivi hauna maambukizi yoyote ya ukimwi, rudi tena kupima baada ya miezi mitatu.

Alivyomaliza tu kuongea sikumwaga, nduki nje, hakuna cha kwa heri wala nini! Kumbe nyuma nimesahau simu. Kidogo mtu ananikimbilia wee kaka umesahu simu yako. Dah huku jasho likiwa linanitoka, watu pale walinipiga macho, na wanaweza kuamini tofauti!

Angaza sio sehemu ya kufanyia majaribio, nenda kama umeamua kweli na tegemea chochote!

Dah, pamoja na kwamba jasho lilinitoka, lakini baada ya kuambiwa sina maambukizi nilitoka mwepesi kama air force one, huku moyo mweupe! Nilienda sehemu nikanunua grand malt, nikawa nakunywa huku nikipumzika taratibu!

Dah, kutokujua status yako ni zigo la misumiri, lakini kupima nako inahitaji ujivue ufahamu!

Nenda kapime ujue uwe huru.

Starehe: Ferooz ft Proffesor Jay - Starehe - YouTube

CC: watu8 lara 1 Kongosho Kaunga charminglady mdida The Boss tinna cute Himidini mwe----- Washawasha nanjilinji MadameX madameA Madame B King'asti Dublin musubati Smile Sista sister Mshinga Mashaxizo Mtambuzi MziziMkavu gfsonwin HorsePower AshaDii mimi49 Heaven on Earth Lady doctor KOKUTONA Nyani Ngabu Eiyer Boflo SnowBall snowhite Mapi

na wana MMU wengine wote, hasa hasa moderators, pamoja na kusimamia JF ni vizuri mkajua status zenu.
 
Last edited by a moderator:
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,086
Likes
11
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,086 11 0
Dedication to all MMU members, attached.
 
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,086
Likes
11
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,086 11 0
miss chagga na PLL mnadhani kupima mbwembwe!
 
Last edited by a moderator:
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,717
Likes
3,390
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,717 3,390 280
Hahaha...ila kuna vimaswali umeviongezea

Mara nyingi maswali huwa machache, kubwa zaidi huwa ni kujua kama mtu anafahamu namna maambukizi ya HIV yalivyo, pia mpimaji huulizwa kama ana mpenzi na wakati wa ngono hutumia kinga.

Siku hizi kipimo si kama zamani kusubiria majibu muda mrefu bali ni kama dakika 5 hivi kwa kutumia Rapid HIV Test Kit...
 
Mkare_wenu

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2011
Messages
1,709
Likes
84
Points
145
Mkare_wenu

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2011
1,709 84 145
Mimi juzi nimeenda kupima,Ila kabla ya kufanya hvyo ilinibid nijidunge viroba vi3 vya konyagi,nimefika pale nazan hata dokta alibaki anashangaa jinsi nilivyokuwa na 'overconfidence' maana nilikuwa namjibu daktari bila wasi utazan nimeenda kupima uzito.Mi nilikuwa nimeenda kupima mara ya pili,Mara ya kwanza nilipima mwez wa 8,maswali niliyoulizwa that day kidogo nijiharishie,yaan hadi walipofikia hatua ya kunipa majibu nilikuwa hoi.Sikuhiyo ndo nikajifunza kupima h.I.v si sawa na kupima uzito hivyo ukiamua kwenda lazima ujiandae.Mara ya pili sikupata shida,kichwan nimeshapiga viroba,nimeenda kwa dokta natafuna bazoka kuondoa harufu
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
3,814
Likes
36
Points
145
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
3,814 36 145
hao angaza kama wanafanya hivyo ni kosa....kuna namna ya kuongea na mtu....na kila mtu ana namna yake ya kuongea nae....wanaonekana kama kuna questionnaire wanaifuata....alafu siku hizi kupima wala sio issue watu wanapima tu
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,717
Likes
3,390
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,717 3,390 280
Nadhani kaweka maneno mawili matatu ya kunogesha kijiwe...

Kawaida huwa ni watu wa nasaha sana na hufanya pre and post test counselling kwa uzuri sana...

hao angaza kama wanafanya hivyo ni kosa....kuna namna ya kuongea na mtu....na kila mtu ana namna yake ya kuongea nae....wanaonekana kama kuna questionnaire wanaifuata....alafu siku hizi kupima wala sio issue watu wanapima tu
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,717
Likes
3,390
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,717 3,390 280
..... ila kwa me napima wala siogopi.... though kutokujua ni safe zaidi kuliko kujua ndivyo navyo amini mimi...
Kama huogopi kupima mbona waamini kutojua usalama wa afya ni ahueni zaidi!!!

Hata hivyo ni vyema kupima kuliko kutopima...kujua usalama wa damu yako au uathirika kunakufanya uchukue hatua ambazo wakati wote ni positive.
 
Mkare_wenu

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2011
Messages
1,709
Likes
84
Points
145
Mkare_wenu

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2011
1,709 84 145
siyo sifa kama unakitembeza sana..... ila kwa me napima wala siogopi....mmh unaonekana ujiamini.. though kutokujua ni safe zaidi kuliko kujua ndivyo navyo amini mimi...
Usitudanganye hapa,hakuna asiyeogopa kupima.labda usiwe binadam wa kawaida
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
3,814
Likes
36
Points
145
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
3,814 36 145
Nadhani kaweka maneno mawili matatu ya kunogesha kijiwe...

Kawaida huwa ni watu wa nasaha sana na hufanya pre and post test counselling kwa uzuri sana...
....sijui lakini naona pre and post counselling zao kama wamekremu....saa nyingine kama wanawatisha wagonjwa.....wakati mwingine hwaangali mazingira, privacy, aina ya mtu........mimi nimeshaenda kupima angaza mara nyingi nawaona...
 
Mashaxizo

Mashaxizo

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Messages
6,723
Likes
109
Points
145
Mashaxizo

Mashaxizo

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2013
6,723 109 145
Khaa!
Jameni kila siku ukimwi tu! Lol!
Kifua changu kidogo mie!!!!!!
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Mkuu umenikumbusha na mimi nitakwenda kupima tena mwaka jana nilipima ukimwi na afya yangu kwa ujumla nikakuta nipo Negative na wiki hii nitakwenda kupima tena kwa sababu Happybirthday yangu inakuja tarehe 6 mwezi huu hahahhahah pole sana upo Negative wewe mkuu.@Simplicity.hongera sana.
 
HUNIJUI

HUNIJUI

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Messages
1,440
Likes
12
Points
135
HUNIJUI

HUNIJUI

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2012
1,440 12 135
haa haa Simplicity tena bora uende pekee yako, kuliko uwe na patna wako halafu hukuwahi kupima before.
ah cku hizi kila mtu anapima kivyake then mkienda ujue marudio
 
Last edited by a moderator:
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2008
Messages
2,720
Likes
34
Points
145
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2008
2,720 34 145
Yaani hizi story za watu kupima HIV kwa mara ya kwanza ama mara yeyote...mara nyingi zina misisimuko ya aina yake.
 

Forum statistics

Threads 1,250,616
Members 481,419
Posts 29,738,807