Kupigania Katiba Mpya ni kama kumkamua maziwa ng'ombe mwenye kichaa

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Nikiwa mdogo kijijini kwetu ngulugulu huko wilaya ya ileje Babu yangu alinifundisha namna nzuri ya kumkamua ng'ombe maziwa, nilipewa mbinu kwamba kuna ng'ombe wastaarabu, hauhitaji kumfunga kamba miguu ili umkamue, na kuna ng'ombe lazima umfunge kamba ndipo umkamue, kwa kuwa anaweza kukupiga teke muda wowote.

Lakini pia Kuna ng'ombe mwenye kichaa huyu hafungwi tu kamba Bali mnashirikiana kumuangusha chini mkiwa mmefunga kamba na kumbana mbavu kisawa sawa ndipo mtafaulu kumkamua. Suala la katiba mpya mpaka sasa limekula pesa nyingi sana bila dalili za mafanikio, rasimu ya warioba nikama mzimu uliotafuna pesa nyingi zaidi na unatutesa usiku na mchana, inaonekana wanaotaka katiba mpya zaidi ni wapinzani ambalo ni kundi dogo.

Nastyle wanayotumia kudai katiba mpya ni kurusha mateke kwa Kila anaejaribu kuwasogelea hata mwenye Nia njema, vyama vingine vipo kimya na mamlaka ambayo ndiyo imekalia dola inaonekana kuwa kama ng'ombe mwenye kichaa; haiingiliki, inarusha mateke yasiyo na idadi inategemea ameamkaje leo analeta matumaini kesho anabadilika.

Nawaambieni katiba mpya ni ndoto kuipata. Labda tushirikiane kumuangusha huyu ng'ombe na kumbana mbavu, kinyume chake tutaenda mpaka 2050 na katiba hii hii, hizi zingine ni faraja za kisiasa tu. Mbowe na lissu peke yao hawataweza.
 
Ni suala tu la muda Wananchi tutaipata Katiba yetu tuliyo ipendekeza mwaka 2012, na hivyo kuondokana na hii takataka ya sasa iliyo tengenezwa kwa nia moja tu ovu ya kuilinda CCM na vigogo wake wa juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom