kupewa vyakula na mke wa mtu

Mpe mwezi ahame nyumbani kwako hata kama hana hela ya kodi kama unauwezo mlipie miezi sita aanze maisha. Hivi kama ukisikia mke wako anampelekea dogo chakula kwanza ungechuliaje hio hali..na hatua gani ungemchukulia huyo Dogo??? Vaa viatu vyake ili uone jinsi huo msala ulivyo
 
vyakula vipo nyumbani anakula na kusaza na hakuna matatizo kama ugomvi nk ni shwari na ndo maana anabeba kuleta nyumbani coz vinamzidi ale chakula cha home na mke wa mtu nazani vinamzidi
 
Hivi wew jail unakaa na mbaba mzima, alafu unamuwita dogo?? sasa kama na wew una mke ngoja akuoneshe madogo aliyo nayo kwake
 
Mtaftie huyo dogo ule uzi unaosema Mambo ambayo inabidi ufanye kabla haujafikisha miaka 30...Inakuwaje unakaa na mtu mzima hivi nyumbani?huenda anayafanya hayo yote kwakuwa hana shughuri yakufanya.Mtafutie shughuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
nina mke mtoto housegirl sijui ana maana gani kuleta nyumbani mke wangu namuuliza anasema huyu ni mtu mzima kwani hajui kuwa ni kosa

Na ukisharuhusu hotpot la jirani kuingia ndani kwako, chalii anakula mwenyewe ama na wanao pia?
Acheni uswahili bwana, hata kama anadoea mke wa jirani hana sababu ya kupewa misosi. Akale huko huko. Kwanza tabia mbaya kula kwa watu.
 
vyakula vipo nyumbani anakula na kusaza na hakuna matatizo kama ugomvi nk ni shwari na ndo maana anabeba kuleta nyumbani coz vinamzidi ale chakula cha home na mke wa mtu nazani vinamzidi

Kama ni mdogo wako kweli, mwite muonye kwamba hiyo tabia sio nzuri na hupendi kuiendekeza nyumbani kwako. Pili inaonekana dogo hana issue za kumkeep busy.....najua changamoto za kazi siku hizi, wapo wanaokushauri labda ahamie sehemu nyingine ni wazo zuri ila inawezekana huna uwezo au hana uwezo wa kuhamia kwengine. kama hatafata ushauri basi waite wote wawili maadam ni majirani na waambie umeandaa hati ya mashtaka tayari unamkabidhi mwenye mke kabla ya mwaka mpya!:faint2::shocked:
 
Na ukisharuhusu hotpot la jirani kuingia ndani kwako, chalii anakula mwenyewe ama na wanao pia?
Acheni uswahili bwana, hata kama anadoea mke wa jirani hana sababu ya kupewa misosi. Akale huko huko. Kwanza tabia mbaya kula kwa watu.

Kwa mfano, sisi tumekatazwa kula kwa watu au sio King'asti
 
Last edited by a moderator:
habari wa ndugu
nina mdogo wangu nyumbani ni wa kiume (30yrs) kuna tabia ya tofauti nimeiona nayo ni kupewa vyakula na mazawadi na mke wa jirani yangu wakati mwingine anaenda huko na kuongea yani hii tabia inanitia wasi wasi haswa hili swala la kupewa chakula nakuta mahot pot maziwa nk nyumbani kwangu jana nimemuuliza kwa nini unapokea vyakula toka kwa mke wa mtu alinijibu kama naletewa nifanyaje? nikatae?nikajaribu kumwelewesha sio vizuri badaye nikatafuta rafiki yake na kumuuliza huyu dogo ana mahusiano gani na huyo mke wa jirani yangu yule dogo akaniambia yani mpaka mapilau matunda nk anagewa na huwa anaingia mara kwa mara kwa huyo mke wa mtu sijui anafanyaga nini da hebu naombeni mawazo yenu wadau namna ya kumsaidia huyu dogo yeye anakataa hana ishu naye but mimi siamini kama vyakula anagewa tu ushahidi sina ila nataka kumsaidia dogo asije akafa kijinga.asanteni
Nionavyo mimi watu tunakariri tu kuwa hakuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume,zaid Mke wa mtu.
Lakini,Ikitokea kuwa Dogo ni Mlafi hashibi kwako tunajuaje? Na kama hata huyo Mume wa huyo mwanamke anatambua kuwa dogo huwa anapewa Chakula na huyo mke wake na pengine ni marafiki na Dogo pia inakuwaje?
Tusihukumu bila ya utafiti wa kutosha,
Ingawa wasiwasi ndio ujanja.

Uwiii mume mtu asiwe MCHAGA tu...!
 
Kama ni mdogo wako kweli, mwite muonye kwamba hiyo tabia sio nzuri na hupendi kuiendekeza nyumbani kwako. Pili inaonekana dogo hana issue za kumkeep busy.....najua changamoto za kazi siku hizi, wapo wanaokushauri labda ahamie sehemu nyingine ni wazo zuri ila inawezekana huna uwezo au hana uwezo wa kuhamia kwengine. kama hatafata ushauri basi waite wote wawili maadam ni majirani na waambie umeandaa hati ya mashtaka tayari unamkabidhi mwenye mke kabla ya mwaka mpya!:faint2::shocked:

asante kwa ushauri
 
Nionavyo mimi watu tunakariri tu kuwa hakuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume,zaid Mke wa mtu.
Lakini,Ikitokea kuwa Dogo ni Mlafi hashibi kwako tunajuaje? Na kama hata huyo Mume wa huyo mwanamke anatambua kuwa dogo huwa anapewa Chakula na huyo mke wake na pengine ni marafiki na Dogo pia inakuwaje?
Tusihukumu bila ya utafiti wa kutosha,
Ingawa wasiwasi ndio ujanja.

ni kweli but vitu vinavyohusisha garama vinaweza athiri uaminifu hata makazini zawadi zinapozidi huleta wasiwasi
 
Yeleuwiii! Yaani ukinuswa mdomo unanukia dagaa wakati home kuna maharagwe utabana ngenge.
Afu kaka, wifi AshaDii kaniudhiii. Ntakuja kumsemelezea

yani acha kinachokera vyakula vinamzidi anaweka frijini hamalizi mpaka mke wangu anashangaa mavyakula kibao da
 
Last edited by a moderator:
Mwambie huyo dogo wako kuwa unakusudia kumweleza mwenye mke hayo yanayoendelea umsikie atasemaje.
 
habari wa ndugu
nina mdogo wangu nyumbani ni wa kiume (30yrs) kuna tabia ya tofauti nimeiona nayo ni kupewa vyakula na mazawadi na mke wa jirani yangu wakati mwingine anaenda huko na kuongea yani hii tabia inanitia wasi wasi haswa hili swala la kupewa chakula nakuta mahot pot maziwa nk nyumbani kwangu jana nimemuuliza kwa nini unapokea vyakula toka kwa mke wa mtu alinijibu kama naletewa nifanyaje? nikatae?nikajaribu kumwelewesha sio vizuri badaye nikatafuta rafiki yake na kumuuliza huyu dogo ana mahusiano gani na huyo mke wa jirani yangu yule dogo akaniambia yani mpaka mapilau matunda nk anagewa na huwa anaingia mara kwa mara kwa huyo mke wa mtu sijui anafanyaga nini da hebu naombeni mawazo yenu wadau namna ya kumsaidia huyu dogo yeye anakataa hana ishu naye but mimi siamini kama vyakula anagewa tu ushahidi sina ila nataka kumsaidia dogo asije akafa kijinga.asanteni

.....mwambie dogo hata "kuku boi hupewa misosi ya nguvu," ili anone na hatma yake ni kisu tu!
 
Kwani mpaka age hiyo bado tuu unamlea asokwenda kutafuta maisha mbele,Hana majukumu ndio mana anaishikiza kwa mke wa jirani lakini siku likija bumburukaa ataomba ardhi ipasuke,huyu kijana anajitafutia balaa sasa bora ya nusu Shari mrudishe kwa wazee....
 
Back
Top Bottom