kupewa vyakula na mke wa mtu

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
475
250
habari wa ndugu
nina mdogo wangu nyumbani ni wa kiume (30yrs) kuna tabia ya tofauti nimeiona nayo ni kupewa vyakula na mazawadi na mke wa jirani yangu wakati mwingine anaenda huko na kuongea yani hii tabia inanitia wasi wasi haswa hili swala la kupewa chakula nakuta mahot pot maziwa nk nyumbani kwangu jana nimemuuliza kwa nini unapokea vyakula toka kwa mke wa mtu alinijibu kama naletewa nifanyaje? nikatae?nikajaribu kumwelewesha sio vizuri badaye nikatafuta rafiki yake na kumuuliza huyu dogo ana mahusiano gani na huyo mke wa jirani yangu yule dogo akaniambia yani mpaka mapilau matunda nk anagewa na huwa anaingia mara kwa mara kwa huyo mke wa mtu sijui anafanyaga nini da hebu naombeni mawazo yenu wadau namna ya kumsaidia huyu dogo yeye anakataa hana ishu naye but mimi siamini kama vyakula anagewa tu ushahidi sina ila nataka kumsaidia dogo asije akafa kijinga.asanteni
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
kama unampenda na kumjali na kama unauwezo heri ahame huo mtaa kabla hajafanywa mbaya.
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
halaf kwanini anavileta nyumban? Nyie wote ma bachela?
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
910
500
sidhani kama mtu anaweza kuletachakula bila sababu ya maana.hapo lazima kunaishu inaendelea ..kama huyo mdogo wako hana kazi mtafutie ishu ya kufanya mbali na hapo nyumban itakayo muweka bize mdawote.pia jalibu kumkanya asije mwagiwa tindikali bule.
 

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
475
250
sidhani kama mtu anaweza kuletachakula bila sababu ya maana.hapo lazima kunaishu inaendelea ..kama huyo mdogo wako hana kazi mtafutie ishu ya kufanya mbali na hapo nyumban itakayo muweka bize mdawote.pia jalibu kumkanya asije mwagiwa tindikali bule.

kuna kazi anafanya hapo ofisini ndo yanatokea hayo chakula kingine analeta home ni maeneo ya nyumbani na nilimwita kufanya kazi sio kukaa kazi anafanya na vituko juu huyo mke wa mtu wamezoeana hapo hapo
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,500
2,000
Umri wote huo anaishi kwako, mpe miezi kadhaa ahame asikuletee tabu maana wakati mwingine huwa tunakaa na wadogo zetu kwa kudhani tunawasaidia maisha kumbe tunawaharibu bila kujijua, umri huo ni kuwa na kwake na kama anapokea misosi toka kwa mke wa mtu hata kama asingekuwa mke wa mtu basi huyo mdogo wako hana kifua cha utafutaji au kwa maana nyingine ameanza kuonyesha kuwa na zile tabia za kulelewa. Mjengee mazingira ya kurudi nyumbani kwa baba na mama maana akiwa kule atapata nafasi ya kujipanga kwa vitendo kwani kuna watu huwa wakikaa kwa ndugu zao hujisahau kama pale sio kwao hivyo anatakiwa a-struggle ili atoke
 

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
475
250
halaf kwanini anavileta nyumban? Nyie wote ma bachela?

nina mke mtoto housegirl sijui ana maana gani kuleta nyumbani mke wangu namuuliza anasema huyu ni mtu mzima kwani hajui kuwa ni kosa
 

Kingmairo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
4,939
2,000
Hapo sio tu yeye ameshajitaftia matatizo bali hata wewe unaingia kwenye tatizo. Haraka sana mpe mwezi mmoja akapangishe hata uwanja wa fisi geto mbona bei chee tu kule?
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,523
2,000
Napata wakati mgumu kuelewa kwamba hutambui kinachoendelea hapo...
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
910
500
basi nenda kampige stop huyo mdada akikuzingua bola umwambie mume wake iliajue tabia ya mkewake.bola nusu shali kuliko shali kamili...
 

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,136
2,000
Nawe pia unamlea!
Alete vyakula nyumbani kwako hasa,anapitishia mlango gani?
Wavizie siku moja uwape makavu wote wawili na uwaambie wakitaka kuendelea kujitoa fahamu basi wakatafute pa kufanyia balaa lao si nyumbani kwako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom