Kupewa nguo na mtu kunaniletea madhara

Kupewa nguo na mtu kunaniletea madhara

Wapendwa habari zenu

Mwaka 2013 nikiwa chuo nimewahi kupewa nguo na mwananchuo mwenzangu ambae sikuwa hata na urafiki nae. kwa kweli siku ile nimepokea tu nguo niliugua ghafla mara kuumwa kichwa kesho yake nilipoamka nikajikuta nimenyolewa nywele. Ila kutokana na kuumwa kichwa muda mrefu ilinibidi nirudie semister kutokana na hali niliyokuwa nayo tena baada ya kuhangaika sana ndo nikapona.

Sasa jana tena kuna huyo dada mfanyakzi mwenzangu sina ukaribu nae hata kidogo zaidi ya salaam tu amenipa nguo tena ikiwa ni mara ya pili mara ya kwanza sikuivaa ile nguo nilimpa rafiki yangu..

Mimi ni mhanga wa kupewa nguo mwisho wa siku zinaniletea madhara..

Jamani nimpigeje stop huyu dada kwa staili gani asiniletee tena hizo nguo?? Maana nimemuuliza mbona unaniletea nguo mimi tuuu na sijakuomba anajibu nimekuletea tu kwasababu ati mim napenda magauni marefu... Nilibaki nikiguna.. nguo nimeiacha ofisini namrudishia.. Siamini katika kupewa tena zawadi ya nguo na mtu.

Nimeteseka sana na kupewa nguo jaman sitaki kuteseka tena...ushauri wenu nimfanyaje huyu dada?
Kua assertive, onyeshanmsimamo kataa waziwazi,
.akichukia na achukie.
 
Co lazima uivae.. Na ww ichukue tafuta mwenye shida /omba omba/maskin umpatie..
Hapana aisee kama nguo ina mikosi ni bora kuichoma kuliko kumpelekea mtu mwingine matatizo.Kuzichoma naona ni bora kuliko kuhamisha tatizo kwa mtu mwingine
 
Maana yangu ni hivii.. Mara nyingi mambo ya uchawi humdhuru yule aliyenuiwa.. Ndio maana mie nishakula sana nazi na mikate ya kumimina inayotupwa njia panda..

Co sidhan kama itamdhuru maskini aliyepewa..
Pia katika kabila letu sisi ni uchuro kuchoma nguo
 
Wapendwa habari zenu

Mwaka 2013 nikiwa chuo nimewahi kupewa nguo na mwananchuo mwenzangu ambae sikuwa hata na urafiki nae. kwa kweli siku ile nimepokea tu nguo niliugua ghafla mara kuumwa kichwa kesho yake nilipoamka nikajikuta nimenyolewa nywele. Ila kutokana na kuumwa kichwa muda mrefu ilinibidi nirudie semister kutokana na hali niliyokuwa nayo tena baada ya kuhangaika sana ndo nikapona.

Sasa jana tena kuna huyo dada mfanyakzi mwenzangu sina ukaribu nae hata kidogo zaidi ya salaam tu amenipa nguo tena ikiwa ni mara ya pili mara ya kwanza sikuivaa ile nguo nilimpa rafiki yangu..

Mimi ni mhanga wa kupewa nguo mwisho wa siku zinaniletea madhara..

Jamani nimpigeje stop huyu dada kwa staili gani asiniletee tena hizo nguo?? Maana nimemuuliza mbona unaniletea nguo mimi tuuu na sijakuomba anajibu nimekuletea tu kwasababu ati mim napenda magauni marefu... Nilibaki nikiguna.. nguo nimeiacha ofisini namrudishia.. Siamini katika kupewa tena zawadi ya nguo na mtu.

Nimeteseka sana na kupewa nguo jaman sitaki kuteseka tena...ushauri wenu nimfanyaje huyu dada?

Mpendwa Binti wa Kirombo ..... Kwanza pole na mikasa iliyokupata.... Kumbuka sio kila anayekuchekea anakuwazia mema. Uchawi/Ulozi upo kataa au ukubali. Pia kumbuka hujalazimishwa kuchukua hizo zawadi za nguo.... Mwambie kuwa wewe unazo za kutosha... Mshauri kuwa kama ana nguo anazotaka kugawa apeleke kwenye vituo vya watoto yatima wenye uhitaji .....

Ni vema ukawa na muda wa maombi ..... pia nakushauri uwe na siku za kufunga na kuomba kuhusiana na mambo yako mbalimbali yanayokuhusu wewe pamoja na familia yako.
 
Sijawahi kuisikia hii kabla. Mi naijua tu ya kuombwa nguo. Anyway, jaribu ku-develop taste ya kipekee na ya gharama kidogo, ili wasifikirie hata kujaribu.
 
Hiyo mbaya mkuu c wanajua lazima utaivaa tena MTU anachagua nguo nzurinzuri mm imenitokea pia ukishavaa ndo umevaa mabalaa yote ya dunia
 
Mpendwa Binti wa Kirombo ..... Kwanza pole na mikasa iliyokupata.... Kumbuka sio kila anayekuchekea anakuwazia mema. Uchawi/Ulozi upo kataa au ukubali. Pia kumbuka hujalazimishwa kuchukua hizo zawadi za nguo.... Mwambie kuwa wewe unazo za kutosha... Mshauri kuwa kama ana nguo anazotaka kugawa apeleke kwenye vituo vya watoto yatima wenye uhitaji .....

Ni vema ukawa na muda wa maombi ..... pia nakushauri uwe na siku za kufunga na kuomba kuhusiana na mambo yako mbalimbali yanayokuhusu wewe pamoja na familia yako.

asante dear narudisha
 
dada inapaswa udumu katika maombi, kunakitabu fulani cha mchungaji Kenneth Onyeme kinaitwa MAOMBI YA KILA SIKU YAKULETEAYO MIUJIZA KWA KILA HITAJI, Ni pm nikuandikie baadhi ya maombi ,hata ukizivaa hazitakudhuru ilimradi usali tu kwa imani

NAOMBA NITUMIE MPENDWA ..NAOMBA
 
Mimi pia mhanga wa kupewa nguo, Nina WiFi yangu huyo alikuwa anapendaga kunipa nguo tena anaomba uivae muda huohuo et aone Kama imekutoa, baada ya siku tatu nikafukuzwa Kazi bila sababu za msingi mambo yakaharibika Sana kila kitu kikawa hakiend mikosi mtindo mmoja ila baada ya kujihangaikia ndo Mwaka huu nimerudi kwenye msitari sasa naogopa hata kwenda kwake maana sijui nitakataaje hizo nguo, mm nakushauri zikatae kwa nguvu zako zote ikibidi punguza ukaribu nae najua watu wanapinga ushirikina lakn upo na hiyo ni njia moja ya ushirikina

POLE MPENDWA SINA HATA UKARIBU NAE ZAIDI YA SALAM TU....ATASHHINDWA KATIKA JINA LA YESU KWA KILA BAYA NA OVU ANALOLIPANGA JUU YANGU DAMU YA YESU IMENIFUNIKA..
 
Zamani mimi nikitaka kukumaliza, nakupa nguo au viatu..
Hii nilikuwa nafanya kwa wabaya wangu tu.. Hasa chuoni..

Siku hizi nimeacha. Ipo siku nitaeleza the science behind it.. Na haiihitaji uwe mchawi/kingunge kufanikisha..

Hata hivyo naweza kukuelekeza namna ya kuzitumia bila madhara.. Ni kamtego kadogo tu ambako hakagharimu hata kilo moja ya sukari..
 
Duh......tueleze ili nasi tujue namna ya kujikinga.!
 
Back
Top Bottom