binti wa kirombo
JF-Expert Member
- May 17, 2016
- 847
- 968
Wapendwa habari zenu
Mwaka 2013 nikiwa chuo nimewahi kupewa nguo na mwananchuo mwenzangu ambae sikuwa hata na urafiki nae. kwa kweli siku ile nimepokea tu nguo niliugua ghafla mara kuumwa kichwa kesho yake nilipoamka nikajikuta nimenyolewa nywele. Ila kutokana na kuumwa kichwa muda mrefu ilinibidi nirudie semister kutokana na hali niliyokuwa nayo tena baada ya kuhangaika sana ndo nikapona.
Sasa jana tena kuna huyo dada mfanyakzi mwenzangu sina ukaribu nae hata kidogo zaidi ya salaam tu amenipa nguo tena ikiwa ni mara ya pili mara ya kwanza sikuivaa ile nguo nilimpa rafiki yangu..
Mimi ni mhanga wa kupewa nguo mwisho wa siku zinaniletea madhara..
Jamani nimpigeje stop huyu dada kwa staili gani asiniletee tena hizo nguo?? Maana nimemuuliza mbona unaniletea nguo mimi tuuu na sijakuomba anajibu nimekuletea tu kwasababu ati mim napenda magauni marefu... Nilibaki nikiguna.. nguo nimeiacha ofisini namrudishia.. Siamini katika kupewa tena zawadi ya nguo na mtu.
Nimeteseka sana na kupewa nguo jaman sitaki kuteseka tena...ushauri wenu nimfanyaje huyu dada?