Kupendwa na mgeni wa rafiki yako

Kupendwa na mgeni wa rafiki yako

Pombe,pombe,pombe,pombe hakuna njia utakayotumia kumfanya aache pombe zaidi ya yeye mwenyewe kuamua na mpaka pale atakapo pata relief ya kile kinachomfanya ame na urahibu wa pombe,mimi pia nilikuwa mtumiaji wa kupitiliza wa pombe na nilikuwa sijali chochote zaidi ya pombe nilikuwa ni mtu wa kuhit and run, ma gf wangu wengi walikuwa wanalalamika kitu kile kile mpaka pale nilipoamua kupunguza na kuepukana na tabia hiyo ya unywaji pombe kupitiliza

mchunguze uone ana tatizo gani linalomsababisha awe mlevi kiasi icho na jaribu kumliwaza aone ilo tatizo ni sehemu tu ya maisha na inatakiwa awe anajari sana muda na management of money,na vitu kama hivo i know you girls are good at that.
 
Habari zenu waungwana..

Mimi nina rafiki yangu wa kiume ambaye ana classmet wake waliosoma pamoja alikuja kumtembelea huyo rafiki.. Jamaa akanimezea mate akamuuliza jamaa huyo binti ana mtu?? Jamaa akamwambia hana..

Sasa huyo rafiki mgeni anataka kuwa na mimi kwenye mahusiano na ni mgeni hapa mjini alikuwa anafanya kazi mkoani akaacha kasema kaja huku kuangalia fursa za biashara afungue biashara.

Sasa tatizo linakuja hapa jamaa anakunywa pombe kama alizaliwa na pombe hajali kama pesa zitaisha na ana miezi mitatu tu kesha tumia zaidi ya milion sita ...hajali mahali popote giza litakapomkuta hapohapo ndo anatafuta lodge ya kulala ..ni mkweli mpaka kupitiliza ...huyo mgeni kasema aliachwa na mpenzi wake baada ya kumhoji kwanini unakunywa pombe hivo??

Sasa waungwana naombeni mnishauri nimfanyeje jamaa aache pombe...ili tuwe na malengo yenye mafanikio...
 
Fursa hiyo bint wa kirombo mpende hivyo zikiisha ataacha mwenyewe
 
Hahaha. Dah we kweli mchaga. Yaani jamaa "kukumezea mate" tu, ushakagua mahesabu. Classment aangalie matumizi bana.


My big brother Paulo Sergio De Souz umenichekesha kupitiliza. That is a super one!

Daah! Ila mtani wangu binti wa kirombo ameonyesha umakini wa kutosha na kile kipaji chetu cha asili kwenye mambo ya mahela. Halafu yaani dada yangu ndio kwanza amekutana na jamaa hata hajamjua kwa undani ashaanza kuota ndoto za ndoa!!!!

Haya bana Binti wa Kirombo kila la kher ila kuwa macho maana ushaonywa tayari na classmet kuwa kilichovunja penzi lake liliopita ni ishu ya kufuatilia mambo yake ya pombe.
 
Niko Arusha ila hayo maziwa sasa sina. We tumia njia yoyote upate hapo kwa jirani,ondoa woga hawezi kukuhisi vibaya
Daah yaani mimi nina bahati ya mtende sababu mimi pia niko Arusha nakaa Bondeni..MUNGU SI ASUMANI.
 
Ananywea pombe mafao?? Kwa matumizi hayo hiyo biashara itadumu kweli?? Kuacha pombe kwa mtu ambaye yuko addicted ni kazi sana..hata kupunguza itabidi ujipinde na uwe mvumilivu haswaaa.....umeshaona unywaji wake sio wa kawaida unafikiri utaweza kuishi nae kwa hali hiyo??
 
Back
Top Bottom