Kupenda kunaisha lini?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Leo nimekutana na boyfrendi wangu wa zamani. Tuliachana tukiwa form six mwaka 98. Nilipopeana nae mkono kwa ajili ya kumsalimia nikajikuta kama nimepigwa shoti ya umeme. Nikayakumbuka mapenzi yetu ya zamani. Yeye ameoa tayari na mimi nina mchumba, lakini nakiri kuwa bado nampenda, sijui ni lini atanitoka moyoni mwangu.
 
Akikuomba penzi utamnyima? Je wewe ni muaminifu kiasi gani kwa mpenzio? Nasjaz naomba jibu tafadhali.
 
ameoa uyo.
kaza moyo msahau lasivyo unaelekea KUIBAKA NDOA YAKO TARAJIWA.
 
mapenzi hayaishi na hudumu milele ila uasherati, uzinzi, umalaya nk vinaisha unapompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako
 
Leo nimekutana na boyfrendi wangu wa zamani. Tuliachana tukiwa form six mwaka 98. Nilipopeana nae mkono kwa ajili ya kumsalimia nikajikuta kama nimepigwa shoti ya umeme. Nikayakumbuka mapenzi yetu ya zamani. Yeye ameoa tayari na mimi nina mchumba, lakini nakiri kuwa bado nampenda, sijui ni lini atanitoka moyoni mwangu.
Ndio maana siamini na wala siwezi kuamini kama mapenzi yanayositishwa kwa amani huisha..... Tafadhali Nazjaz, huwa tunaamini kuwa wahenga walisema uhamapo usinyee kambi......, lakini kambi ya mapenzi hupaswa kunyewa na kuchomwa moto, vinginevyo utarudi tu...... And, because of these kind of feelings, that I can't trust anyone along her/his ex....., unless the relationship has broken because of a big conflict, and the conflict is never get resolved.....!
 
Samahani kwa kuvamia jukwaa ambalo halinihusu, ila huyu bado ana ugonjwa wa facebook. maana juzi alikuPM waziri na leo unataka kupigwa mpini na boyfriend wa zamani, kwa kifupi jina lako halisi wewe ni Malaya au kahaba.
 
Kwa kweli mapenzi hayaishi moja moja kwa moja, ndo maana baadhi ya wapenzi wanagombana na kuachana lakini baada ya muda muda mrefu usishangae kusikia wamerudiana. Unapopata mwenzi wako wa ndoa manawekeana ahadi kemkem ndo maana unatakiwa kusahau habari ya wapenzi wako wa zamani.
 
Samahani kwa kuvamia jukwaa ambalo halinihusu, ila huyu bado ana ugonjwa wa facebook. maana juzi alikuPM waziri na leo unataka kupigwa mpini na boyfriend wa zamani, kwa kifupi jina lako halisi wewe ni Malaya au kahaba.

SAIGON MKUU, Kwanza samahani ikiwa nimevamia ugomvi usionihusu na wala sitaki niwe Hakimu wa Ibilisi (Devil's Judge) kati yako na na huyu binti, lakini yale ya juzi yalishaisha na sioni sababu ya kuendelea kumnanga hasa kwa lugha ya kashfa hasa kwakutilia maanani kuwa hapa ni MMU ndani ya JF.
 
inategemea mliachana vipi.na kama una feelings nae,ina maana huyo uliokuwa nae kuna kitu hakikuridhish au kuna kitu ex wako alikukuna vilivyo,hicho kitu ex wako,hajakuridhisha.jaribu kurekebisha mapungufu yako na mchumba wako,ukifanya hivyo,huyo ex wako utamuona wa kawaida tu
 
Leo nimekutana na boyfrendi wangu wa zamani. Tuliachana tukiwa form six mwaka 98. Nilipopeana nae mkono kwa ajili ya kumsalimia nikajikuta kama nimepigwa shoti ya umeme. Nikayakumbuka mapenzi yetu ya zamani. Yeye ameoa tayari na mimi nina mchumba, lakini nakiri kuwa bado nampenda, sijui ni lini atanitoka moyoni mwangu.

Ikkiwa unaelewe neno kinyume ya mapenzi, mwisho wa mapenzi ni pale panapoingia hilo neno.
 
Samahani kwa kuvamia jukwaa ambalo halinihusu, ila huyu bado ana ugonjwa wa facebook. maana juzi alikuPM waziri na leo unataka kupigwa mpini na boyfriend wa zamani, kwa kifupi jina lako halisi wewe ni Malaya au kahaba.

Hajakuomba umtathmini bali kauliza swali apewe jibu na siyo matusi.Kwani kama umekerwa na swali lake, kuliko kumvunjia heshima yake si ungenyamza ingetosha?
 
Mlikuwa wapenzi mkaachana ilikuwaje je upendo uliyeyuka?
Yule ni mume wa mtu na wewe unamchumba mbona hueleweki
kuwa mwaminifu kwa mchumba wako acha papara

au ndio yule bwana wa kisukuma?
 
Mkimbie, wala usi entatain ya kuwa nae karibu, kumbuka wewe una mchumba, usijemkosa mwana na maji ya moto. Kama ulimsahau miaka yote hiii na umesavaivu waweza endelea kuishi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom