Kupata kazi yenye mshahara mnono kunachangia kujituma

Gotze Giyani

Senior Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
143
Reaction score
212
Wadau poleni na majukumu

Mimi ninahoja kama 3 naomba tujadili kidogo.Hivi wadau kwa aliyewai kufanya kazi akapa mshahara mnono na package nono alifanyaje ilikuwa ni bahati au connection nauliza hivyo sababu mimi sijawai kupata hiyo bahati ila kazi uwa napata hilo namshukuru Mungu kingine hivi pia hili la Veta limekaaje au ndio viongozi wetu wanatuchukulia poa sana.

Wadau karibuni na experience zenu za kupata kazi sehemu nzuri nataka nipate uzoefu wenu nitafurai na pia je alikuwa anajituma kazini??
 
Vyote bahati au connection vinaweza pelekea kupata kazi yenye mshahara mnono ( kubali kuanzia chini zipo kazi za mshahara wa kawaida lakini vipo viposho vinono ndani yake) kuhusu veta Ni kawaida kwa msomi kujiongezea taaluma. Wengi tumesoma driving pale. Chagua fani si haba ukipata maarifa kedekede.
 
Hueleweki ,,,, unataka mshahara mnono ? Una kaz mshahara wa kawaida ? Ama ni jobless umeambiwa uende Veta ! Jiweke sehemu moja ili tukushauri vyema ! Vijana mnataka mabadiliko ya haraka haraka, ukianza kazi Leo kesho uwe promoted!
 
Kujituma kazini inategemea na work ethic yako. Kizazi chenu hiki kipya hiki ni legelege ajabu. Hata kipewe mshahara mnono ni madoido tu na kuiba. Ndiyo maana watu makini wanaogopa sana kuweka Mbongo kwenye vyeo vya juu katika makampuni yao. Wanapendelea Wahindi na hata Wakenya. Kidogo wana integrity na work ethic nzuri.

Wabunge wana mishahara minono na package nzuri sana, unaona kama wanajituma?

Kupata kazi zenye mishahara minono unahitaji bahati, experience yako na sana sana connection.

Kuhusu Veta Blessings kasema anapeleka boom. Utakwenda? 😂

1247523385.jpg
 
Niko kazini japo ninajiendeleza sana kazi nimefanya miaka 7 sio nataka mabadiliko ya haraka mimi nimvumilivu sana sema nataka changamoto sehemu nyingine nzurii
 
Kujituma kazini inategemea na work ethic yako. Kizazi chenu hiki kipya hiki ni legelege ajabu. Hata kipewe mshahara mnono ni madoido tu na kuiba. Ndiyo maana watu makini wanaogopa sana kuweka Mbongo kwenye vyeo vya juu katika makampuni yao. Wanapendelea Wahindi na hata Wakenya. Kidogo wana integrity na work ethic nzuri.

Wabunge wana mishahara minono na package nzuri sana, unaona kama wanajituma?

Kupata kazi zenye mishahara minono unahitaji bahati, experience yako na sana sana connection.

Kuhusu Veta Blessings kasema anapeleka boom. Utakwenda? 😂

View attachment 3277650
Veta ninakubali kabisa ila broo ajira kwangu sio tatizo wala sipendi mambo marahisi nimekaa kazini miaka 7 na zaidi ila sema nimeulizia sehemu nzuri kama zenye posho na promotion nzuri
 
Kujituma ni hulka ,kazi ni kawaida ila kama unakutana na client moja kwa moja basi pambana ...Miaka ya nilikuwa nalipwa less amount compare ya sasa ,kwa sababu nilikuwa makao mkuu nakutana na clients moja kwa moja ,unatakiwa kuwa mtu wa haraka ,ukifungua emails unaweza kuzikuta 20+ unread, huku wengine wamekuja ana kwa ana ni changamoto sana .

Ila ukiwa vituo vya mkoani kama sasa kazi ni nyepesi ,kawaida sana ila mshahara mzuri unaleta hamasa kwa kweli...Just imagine unaanza na mil kadhaa .
 
Kujituma kazini inategemea na work ethic yako. Kizazi chenu hiki kipya hiki ni legelege ajabu. Hata kipewe mshahara mnono ni madoido tu na kuiba. Ndiyo maana watu makini wanaogopa sana kuweka Mbongo kwenye vyeo vya juu katika makampuni yao. Wanapendelea Wahindi na hata Wakenya. Kidogo wana integrity na work ethic nzuri.

Wabunge wana mishahara minono na package nzuri sana, unaona kama wanajituma?

Kupata kazi zenye mishahara minono unahitaji bahati, experience yako na sana sana connection.

Kuhusu Veta Blessings kasema anapeleka boom. Utakwenda? 😂

View attachment 3277650
Surely, Wabongo walio wengi ni waangushiaji...maneno mengiiiii...kazi kiduchu! Hii ni indicator ya umaskini
 
Veta ninakubali kabisa ila broo ajira kwangu sio tatizo wala sipendi mambo marahisi nimekaa kazini miaka 7 na zaidi ila sema nimeulizia sehemu nzuri kama zenye posho na promotion nzuri
Creativity is most important thing in your work!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom