Kupandishwa Daraja kazini inakuaje wadau?

Kupandishwa Daraja kazini inakuaje wadau?

Syosaamenye

Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
79
Reaction score
7
Eti wadau kwa mtumishi wa umma kupandishwa daraja kazini inakuaje? maana kuna dada mmoja analalamiaka sana anasema hajapandishwa daraja wakati muda wa kupandishwa daraja ulipita tangu mwaka jana, je anaweza kumshtaki mwajili kwa maana hakuna barua ya kalipio lolote aliyowahi kuandikiwa wala kufanya misconduct yoyote katika kipindi cha utumishi wakae. naomba mnijuze ili nimsaidie....
 
Kupandishwa kazi kunategemea yafuatayo: kwanza,ELIMU-namaanisha awe ameongeza elimu. Pili,ana mahusiano gani na bosi wake-PROMOTION.Kama ana mahusiano mazuri na bosi wake basi aweza kuwa promoted,kama hana mahusiano mazuri na boss wake hilo asahau kabisa.Tatu,UZOEFU KAZINI.kama ana uzoefu wa muda mrefu aweza pia kupandishwa daraja.SABABU ZOTE ZINAWEZEKANA KUTEGEMEA NA UPATIKANAJI WA NAFASI PAMOJA NA ELIMU YA BOSI WAKE MBNA HAIWEZEKANI BOSS AKAWA NA ELIMU NDOGO THEN AKUPANDISHE DARAJA ILI UWE BOSS WAKE??
 
Sijajua anafanya kz ktk kada gani kwa kawaida kama ni serikalini kupandishwa daraja hakutegemei elimu ya muhusika kada nyingi unapandishwa daraja kila baada ya miaka mitatu lakini siyo lazima itategemea na uwezo wa muajiri katk bajeti yake kwa hiyo suala la kupandishwa daraja huwezi mpeleka muajiri mahakamani maana inategemea na bajeti yake muhimu waone maafisa utumishi wakuweke kwenye mpango wa bajeti ili mwaka ujao wa fedha upandishwe daraja
 
Natumai wote wazima naombeni msaada wa hali na mali nimemaliza kidato cha sita mwaka jana naomba msaada niweze kwenda chuo 0762612213 mungu awajalie mtakaoguswa
 
Sijui kama unaelewa maana ya kupandishwa daraja...Naona umepiga siasa tu hapo. Nitarudi baadaye kidogo kukuelekeza maana ya kupanda daraja
 
Sijajua anafanya kz ktk kada gani kwa kawaida kama ni serikalini kupandishwa daraja hakutegemei elimu ya muhusika kada nyingi unapandishwa daraja kila baada ya miaka mitatu lakini siyo lazima itategemea na uwezo wa muajiri katk bajeti yake kwa hiyo suala la kupandishwa daraja huwezi mpeleka muajiri mahakamani maana inategemea na bajeti yake muhimu waone maafisa utumishi wakuweke kwenye mpango wa bajeti ili mwaka ujao wa fedha upandishwe daraja
Wewe ndio unajua japo hujaeleza kila kitu
 
natumai wote wazima naombeni msaada wa hali na mali nimemaliza kidato cha sita mwaka jana naomba msaada niweze kwenda chuo 0762612213 mungu awajalie mtakaoguswa

hata form four wamemaliza, kumaliza sio deal ni umefaulou kwa kiwango gani
 
kupandishwa daraja kazini kunategemeana na utendaji wako wa kazi, hilo litategemeana na ujazaji wako wa fomu ya wazi ya mapitio ya kazi -OPRAS, pili utumikie cheo chako kwa muda wa miaka mitatu lakini ujazaji wa opras ni lazima ili ikifika miaka mitatu uwe considered

so muulize huyo dada kama amejaza OPRAS na cheo alicho nacho sasa amekitumia kwa miaka mitatu
 
Hili swala bana limekuwa ni utata sana siku hizi, OPRAS imeleta majanga!!! Mie nimefanyakazi kwenye taasisi fulani serikalini ni mwaka wa nane sasa sijui daraja linavyopanda!!! Naona tu wakiajiriwa watoto wa vigogo mwaka huu mwaka kesho yake wana mishahara mikubwa kupita maelezo. Nimewazidi elimu, nimewazidi uzoefu kazini, nawafundisha kazi mwenyewe cha ajabu mishahara yao inanizidi na kichwani mwao ndo empty kabisaaa!!! Wakiharibu kazi ukapishana nao lugha tu utashangaa simu zinatoka hata usikokujua na vimemo vya vitisho!!!

Nimehangaika kupandishwa daraja mpaka imefikia tunatukanana matusi ya nguoni na mabosi ikabidi nitulie tu mana wengine hatuna wajomba vibosile!!!

Dawa yao ni kutumia fursa zilizopo kujishindilia shule mpaka wakishtuka uko mbali, uvumilivu muhimu sana!!!
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Serikalini ni duration ya miaka3 unatakiwa kupanda daraja ila ndo hvyo ishu inaanzia kwa afisa utumishi wa kitengo
 
Natumai wote wazima naombeni msaada wa hali na mali nimemaliza kidato cha sita mwaka jana naomba msaada niweze kwenda chuo 0762612213 mungu awajalie mtakaoguswa
aaaah job!si ungeanzisha na wewe thread nyingine upate huo msaada unaohitaji!!sasa ona umeandika haraka haraka umeshindwa hata kusema unataka msaada wa nini!!
 
Natumai wote wazima naombeni msaada wa hali na mali nimemaliza kidato cha sita mwaka jana naomba msaada niweze kwenda chuo 0762612213 mungu awajalie mtakaoguswa

post juu ya post kwa nini unedandia gari tena kwa mbele
endelea kusubirii tena subiri sana huo msaada wa kwenda chuo
 
Unatakiwa kupandishwa daraja ndani ya miaka 3
Kwakuwa mwajiriwa ana sifa za msingi za kuajiriwa,kuongeza Elimu ni suala la kawaida ila si kigezo cha mtu kupanda daraja.

Suala la Boss laweza kuwa jingine kabisa
pia anatakiwa kumkumbusha Boss wake
Mfano mzuri ni kwa Walimu huwa wanakwenda
Halmashauri kudai barua za kupanda daraja
kwa Afisa Utumishi.

Labda kama mwajiriwa awe na makosa ya
utendaji hiyo pia yaweza kuwa ni sababu
 
Back
Top Bottom