Kupanda gari za magazeti,nimekoma

Kupanda gari za magazeti,nimekoma

Mbona 160 ni speed ya kawaida, mim mwenyewe siyo driver by professional lakini natembea mpaka 180 km per hour kama naenda Arusha sasa hao kila siku wako barabarani unashangaa 160!!!
 
Kaka hiyo Gari nilipanda aisee toka Makambako kuja Dar..nakumbuka Dereva alikuwa anazungumza na wenzake kwamba anataka kuwahi kuchek gem ya UEFA Dar..makambako tulitoka saa 7..ila tuliwa mech mapema sana...

Kikubwa sio kulaumu kwanza hao jamaa ni special case hawasimamishwi na Traffic..

Nimeskia hutafutwa madereva maalum kwa kazi hizo na sio madereva waoga waoga

Umenikumbusha mkuu, nilipata lift ya gari hilo pale Kituo cha Oryx Makambako la kuja dar, tulikuwa na mzee mmoja hivi. Tulipofika usawa wa Mafinga yule mzee alianza kusali, baadae alikaa kimya kama mgonjwa hivi. Tulipofika Ubungo alisema neno moja tu, MUNGU NAKUSHUKURU. Akakaa chini pale Oil com hana hamu.

Zile gari ni noma.
 
Wakati nasoma ARUSHA nilikuwa nalipanda sana like coaster.
 
Tumezika kijana mdogo sana December alipata ajari Same....gari hizo hizo zisizojari muda
 
Mkuu huo ni unafiki we mwenyewe hukupanda bus ukaona upande gari la magazeti ili uwahi ishu yako umesolve basi ushaanza kuomba wakamatwe. Dah kweli wema mtendee MBUZI utakunywa hata Mchuzi
 
Salam sana ndugu zangu.Ni matumaini yangu kwamba week-end inakwenda vizuri sana!

Juzi siku ya Alhamisi January 19, 2017 niliingia "mkenge" kwa kupanda gari ya magazeti ya MWANANCHI kutoka Dsm to Arusha. Nilipanda hilo gari kwa sababu nilipata wito muhimu sana wa kuonana na mtu muhimu sana kesho yake Ijmaa saa 3 kamili asuubuhi.

Na nilifanikiwa kukaa seat ya mbele,hivyo nikawa naona namna dereva anavyocheza na usukani wake barabarani.

Speed 100 km /hr n ya kawaida sana kwa gari ya magazeti. Kuna muda anatembea speed mpk 160 km/hr.Dereva alikuwa amevaa shuka la kimasai na simu yake ya touch kwenye dushboard!

Ku-overtake malori hata kwenye kona, n kitu cha kawaida sana. Dereva anateendesha gari kuna wakati ananing'iniza mkono wake mmoja dirishani kwenye mlango wake, huku mkono mmoja ukiwa ndiyo unapapasa usikani!Balaaa.

Mbaya zaidi akawa anaongea na madereva wenzie ambao nao wameondoka Dsm na kuelekea mikoani.

Kuna vitu visivyoisha,dereva alianza kuvitafuna Dsm mpk tumeingia Arusha.

Tochi za kuwathibiti hawa madereva haziwanasi jamani?

Kwann trafic wasiwakamate hao madereva pindi wanapoona muda ambao wametumia n mfupi?Na kwann wasitumie usafiri wa ndege kutawanya hayo magazeti Au kwa nn wasiongeze vituo vya uchapishaji huko mikoani?
Acha kuwachomea wewe.....aliyekutuma kupanda hizo gari ni nani? Umetatuliwa shida yako unaanza kulaumu, ulikuwa hujui kwamba hzo gar huo mwendo ni wa kawaida sana kwao??
 
Back
Top Bottom