Kupanda gari za magazeti,nimekoma

Kupanda gari za magazeti,nimekoma

Ndege haiwezekani sababu karibu mikoa na vituo vyote wanapita kuacha magazeti
...Eti wewe mleta mada, huyo dereva alikuwa anaacha magazeti njiani au mlivyotoka DSM aliweka jiwe kwenye accelerator mpaka A town?
 
Salam sana ndugu zangu.Ni matumaini yangu kwamba week-end inakwenda vizuri sana!

Juzi siku ya Alhamisi January 19, 2017 niliingia "mkenge" kwa kupanda gari ya magazeti ya MWANANCHI kutoka Dsm to Arusha. Nilipanda hilo gari kwa sababu nilipata wito muhimu sana wa kuonana na mtu muhimu sana kesho yake Ijmaa saa 3 kamili asuubuhi.

Na nilifanikiwa kukaa seat ya mbele,hivyo nikawa naona namna dereva anavyocheza na usukani wake barabarani.

Speed 100 km /hr n ya kawaida sana kwa gari ya magazeti. Kuna muda anatembea speed mpk 160 km/hr.Dereva alikuwa amevaa shuka la kimasai na simu yake ya touch kwenye dushboard!

Ku-overtake malori hata kwenye kona, n kitu cha kawaida sana. Dereva anateendesha gari kuna wakati ananing'iniza mkono wake mmoja dirishani kwenye mlango wake, huku mkono mmoja ukiwa ndiyo unapapasa usikani!Balaaa.

Mbaya zaidi akawa anaongea na madereva wenzie ambao nao wameondoka Dsm na kuelekea mikoani.

Kuna vitu visivyoisha,dereva alianza kuvitafuna Dsm mpk tumeingia Arusha.

Tochi za kuwathibiti hawa madereva haziwanasi jamani?

Kwann trafic wasiwakamate hao madereva pindi wanapoona muda ambao wametumia n mfupi?Na kwann wasitumie usafiri wa ndege kutawanya hayo magazeti Au kwa nn wasiongeze vituo vya uchapishaji huko mikoani?
We mmbeya balaaa, ungekuwa Jirani ningekukodishia matarumbeta, duh! Ulilazimishwa kupanda kwanza wewe sio Gazeti, kama ulipewa msaada unaleta umbeya wa nini Jf? Mbavuuuuu
 
Hayo magari na speed zao huwa zinawachinjaga wenyewe....
Sema speed kwao ruksa Si unajua watu wanawahisha magazeti

OvA
 
Sioni kama kuna jambo la ajabu hapo!kutembea speed 160 mbona kawaida tu!

Nimeshangaa kidogo, yaani 160 ndo anashangaa, ndo tabu ya kuzoea kupanda mwendokasi, mi nilijua wanatembea zaidi ya 230 kph. Watu tunatembea na 180 afu tunaona kawaida tu.
 
Mtoa mada mpuuzi sana!kapata msaada alafu anaropoka ujinga wake wakati kawaishwa katika ishu yake muimu.
 
Acha kiherehere ningejua ningekushusha njiani tu.
Wewe si ulianiambia unataka kuwahi interview siku ya ijumaa. Ningejua ningekushusha wami.
Siku nyingine ukitaka kuwahi panda zile ndege za sizonje
🙄🙄🙄...Eti ndege za sizonje khaa!! Watu mna maneno hatar.
Cc mrisho mpoto.
 
Umenikumbusha mkuu, nilipata lift ya gari hilo pale Kituo cha Oryx Makambako la kuja dar, tulikuwa na mzee mmoja hivi. Tulipofika usawa wa Mafinga yule mzee alianza kusali, baadae alikaa kimya kama mgonjwa hivi. Tulipofika Ubungo alisema neno moja tu, MUNGU NAKUSHUKURU. Akakaa chini pale Oil com hana hamu.

Zile gari ni noma.
nakumbuka ht mm..kitonga tulishuka kwa dkk 6 yan dah mlima wote na kona zake zile hatare sana, ...nawale jamaa kuhusu usalama wao yan kwann hawaogop wanakwambia hatuogop lkn cku akidondoka tu bac ujue kwaeri dunian wanakwambia
 
Nenda ubungo sheli pale ndio wanapakiaga pale mida ya sa sita hiv ucku

Sawa mkuu asante kwa maelekezo, na yanayoenda mikoa mingine pia yanapakiliwa hapo shell??
 
Nimeshangaa kidogo, yaani 160 ndo anashangaa, ndo tabu ya kuzoea kupanda mwendokasi, mi nilijua wanatembea zaidi ya 230 kph. Watu tunatembea na 180 afu tunaona kawaida tu.
Hata Mimi nimemshangaa
 
Back
Top Bottom