Kupaka rangi za ruti: UDA na SUMATRA nani mbabe?

Kupaka rangi za ruti: UDA na SUMATRA nani mbabe?

Pilimi

Member
Joined
Mar 23, 2009
Posts
67
Reaction score
14
Wana JF,naomba kuuliza kati ya SUMATRA na UDA nani anasimamia sheria za usafiri nchi hii? Maana ni matamko mengi sana yaetolewa na SUMATRA kuhusu kupaka rangi za route zao katika hizo UDA lakini hadi leo hakuna kitu.Cha ajabu zaidi leo nimepanda UDA kutoka Gongo la Mboto-Ubungo konda anatoa tiketi hazijaandikwa wala bei hata route hakuna.Wakati huo huo trafiki wengi njia yote.hawafanywi chochote.Sasa SUMATRA wameshindwa kwa huyo UDA?

Na attach tiketi.
 

Attachments

  • UDA.jpg
    UDA.jpg
    17.3 KB · Views: 347
Hio tiketi ya kwenda mkoani?
Mabosi wa sumatra ndio hao hao wa uda usitegemee mabadiliko.
Kuna route ya kutoka mnazi mmoja adi kivukoni hii ni kuwaumiza wananchi tu uroho wa pesa
Na gari za uda na madereva wake wanaringa sana
 
Hio tiketi ya kwenda mkoani?
Mabosi wa sumatra ndio hao hao wa uda usitegemee mabadiliko.
Kuna route ya kutoka mnazi mmoja adi kivukoni hii ni kuwaumiza wananchi tu uroho wa pesa
Na gari za uda na madereva wake wanaringa sana

Hapana,ni tiketi ya usafiri Dar es salaam.
 
Usitegemee mahali penye vigogo kama yule mwana mfalme haki ikapatikana,zitakamatwa tu vidaladala vyetu vya kajamba nani....
 
Sumtra hii ni tofauti na enzi za David Mwaibula. Hawa ni toothless kabisa. Hilo tangazo la kuwataka UDA wapake rangi za route lipo karibia mwezi sasa, ila hakuna kilichofanyika.
 
UDA lazima iogopwe,nani hajipendi aanze kuhangaika na kampuni ambayo hata mmiliki wake hajulikani na inazidi kupeta! Bunge na baraza la mawaziri limenywea sembuse sumatra,tuvumilie tu siku wakipenda wataweka na wasipo penda ndo hivo tena!
 
UDA haijadililiki hata Bungeni kama ulikuwa haujui basi tumekujuza!!
 
Huyu Kisena ana nguvu kuliko serikali msimchukulie poa, anaweza hata kuangusha serikali.
 
da hiyo mi naona sumatra ndio kila kitu aise mana wote ni sawa na mtoto kumtuma baba yake
 
Serikali ya tz kila kitu ni miradi ya vigogo tu fulani fulani hakuna kingine na wala hawajali wananchi wake watakua ktk hali gani
 
Leo hii kwa wakazi wa kigamboni lazima wapande mabasi mawili au watembee kwa miguu hadi mnazi mmoja ndio wachukuwe usafiri mwengine kuelekea wanakotataka kwenda
 
Hili la uda ni tatizo;
Wanafanya ruti wanayoona haina folen;
Ukiuliza wanasema ni mabasi ya wakubwa;

Ni heri kabisa UDA isiwepo kama wameshindwa
kuweka rangi za roti.
 
Hili la uda ni tatizo;
Wanafanya ruti wanayoona haina folen;
Ukiuliza wanasema ni mabasi ya wakubwa;

Ni heri kabisa UDA isiwepo kama wameshindwa
kuweka rangi za roti.

CEO wa zamani SUMATRA Mr.Sekilasa alijifanya kukomaa na sheria hata mali za wakubwa mwishowe alishia kipindi kimoja tu, hakuongezewa kipingi kingine cha miaka mitano
 
nchi zetu hizi twendage tu bwanah maana ni shd kidgoo aiseee kila mtu anatumia meza kushbisha tumboo
 
Namkumbuka sana Mwaibula.., hii Sumatra ya sasa hivi ni urojo sana..
 
yana mwisho haya.. na nitaushuhudia mwisho wake.. as long as God lives
 
Back
Top Bottom