Nauli za daladala na uelewa wa wananchi katika jiji la Dar es Salaam

Msurunje

JF-Expert Member
Oct 21, 2019
219
342
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa wote tulio na afya njema na poleni kwa wote wenye changamoto za kiafya kwa umoja wetu tunawaombea ili muwe na afya njema mrejee katika majukumu yenu ya kimaisha.

Wakuu kuna hili suala la wafanyakazi wa daladala za jiji la Dar es Salaam kuchukua nauli kwa abiria zaidi ya kiwango kilichowekwa na SUMATRA kwa sasa LATRA. Tabia hii kwa sasa imekuwa sugu mpaka kondakta anatoa lugha isiyokuwa ya kiungwana kwa abiria ambae yeye anamchukulia kama ametoa nauli pungufu. Lakini cha ajabu zaidi sio abiria anaedaiwa kutoa nauli pungufu au abiria wengine waliomo ndani ya gari atasema kuwa konda anatoza nauli zaidi ya kiwango kilichowekwa na mamlaka husika kulingana na umbali. Tena mbaya zaidi kuna abiria anadiriki kusema kiwango sahihi ni kile kinachosemwa na konda kwa sababu tu ya mazoea.

Hapa natoa mfano wa ruti ambazo wafanyakazi wa daladala wanatoza nauli kimakosa either kwa kutokujua au kwa kuwaibia abiria kwa maksudi kwa kuwa abiria hawaelewi mpangilio wa ulipaji wa nauli. Mfano ukipanda gari la kutoka gongo la mboto kwenda mbagala na kama upandia banana na unashuka tazara au sokoni konda anakwambia nauli ya 400 mwisho tazara kabla ya kukunja kona na gari likishakunja kona nauli ni 500, hivyo hivyo ukiwa unaenda makumbusho wanakwambia nauli ya 400 inaishia buguruni hata km umepandia wapi, ukipanda magari ya temeke kupitia buza wanakwambia nauli ya 400 mwisho ni jeti na ukipanda magari ya temeke kwenda makumbusho wanakwambia nauli ya 400 inaishia ilala boma.

Sasa ndg zangu kwa kuwa mimi nimekuwa nikikelwa na hiki kitu naomba kitoe elimu kupitia hili jukwaa ili kwa wale asiokuwa na uelewa ili wanapokuwa wanatoa nauli wajue kiwango halali kinachotakiwa kutolewa kulingana na umbali anaokwenda na hata kama ikitoa akatozwa nauli zaidi basi iwe ni kwa kutaka kwake lkn uelewa anakuwa nao.

Ndg zangu tangu mwaka 2013 yalipo tangazwa mabadiliko ya nauli za daladala kutoka 300 kwenda 400 mpaka leo mamlaka haijatangaza tena mabadiliko ya nauli za daladala kwa hiyo tunaendelea na nauli za tangu 2013 na hakuna mfanyakazi wa daladala anaruhusiwa kutoza nauli zaidi ya iliyowekwa na mamlaka kwa maana hiyo mamlaka ndio inapanga viwango vya nauli. Badala ya kueleza kila umbali na kiwango kinachotakiwa kutozwa naambatanisha jedwali kutoka Sumatra/Latra linaloonyesha umbali na kiasi kinachotakiwa kulipwa pamoja na mfano wa ruti. Kitu muhimu cha kuelewa ni kwamba umbali unahesabika toka pale ulipopandia daladala mpaka utakaposhuka na siyo pale gari linapoanzia safari na kuishia.

20210906_093220.jpg
 
sheria haijafafanua kituo hadi kituo nauli iwe shingapi.

mfano hapo unaona minmum ni 400,vipi ukivuka vituo vitatu??
 
Hao Latra nauli mpaka wanapanga wanaangalia vitu vingi sana,kwanza wanaangalia kilometa kisha na hali ya barabara,miundombinu kwa ujumla,mfano mdogo tu kutoka kinyerezi hadi kivukoni nauli yao ni 500,ila kutoka segerea hadi mnazi mmoja nauli ni 450,kaa kwa kutulia Latra wapo makini sana katika kupanga bei za nauli
 
Back
Top Bottom