Kuota Unakula Nyama

Kuota Unakula Nyama

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,494
Reaction score
12,466
nimeota nakula nyama mapande ya nguvu,ila sijui hata ni nyama gani,nashtuka nakuta tumbo limejaa,i mean nimeshiba.

Ile imani ya kwamba ndoto za aina hii zinakuaga na uhalisia yaweza kuwa kweli? mana naskia hadi kichefu chefu....K@$?#!6E....
 
Nawahi seat tu mkuu. Nangoja wajuvi wa mambo ya elimu dunia
 
Ndoto ya kula nyama inaweza kuwa na maana nyingi.
Kubwa,nyama na damu ndiyo vitu pekee vinavyotumika kuingiza watu ktk mikataba ya giza means uchawi.Kwa kula nyama umeingizwa ktk mkataba mchafu ili uutumikie.At all si ndoto nzuri.Ni ndoto inayoenda na utoaji wa kafara ktk giza.Hata hivyo waweza kuona kafa mtu ktk ukoo wako na mkala nyama kama mlivyokula ukiwa ktk usingizi.
Umelishwa mikataba michafu ktk ulimwengu wa giza.
Solution to this is to cancel through prayer and repent ,try to see your church leaders for more advise.
Worry not nothing cant be terminated to God through faith.
 
nimeota nakula nyama mapande ya nguvu,ila sijui hata ni nyama gani,nashtuka nakuta tumbo limejaa,i mean nimeshiba.

Ile imani ya kwamba ndoto za aina hii zinakuaga na uhalisia yaweza kuwa kweli? mana naskia hadi kichefu chefu....K@$?#!6E....
Una muda gani hujala nyama? isije ikawa njaa zako tu!
 
NDOTO HATARI AMBAZO UKIOTA UNAPASWA KUINGIA MAOMBI YA VITA.

[emoji637] Kuota Unakunywa maji machafu(Ni ishara ya kupewa sumu katika ulimwengu wa roho na kuondoa moto wa Roho Mtakatifu)

[emoji638] Kuota unakoroma na unalia kwa uchungu(Ni Ishara kuwa adui anapanda mateso juu yako)

[emoji639] Kuota kuna Vipingamizi vya kuzia usiendelee mbele( Ni Ishara adui anaweza Uzio kwenye Mafanikio yako)

[emoji640] Kuota unakula vyakula usiku (Ni Ishara kuwa umeunganishwa na mtandao wa kiuchawi)

[emoji641] Kuota unaoanda mlima kwa taabu sana( Ni Ishara kuwa adui anakufanya uhangaike sana kabla ya kupata riziki)

[emoji642] Kuota uko kwenye Mataa ya Barabarani( Ni Ishara kuwa pana Vikwazo vya kuendelea Mbele)

[emoji643] Kuota umetumbukia shimoni (Ni Ishara kuwa adui ameshakuweka kwenye shimo fulani)

[emoji644] Kuota Upepo Mkali (Ni ishara Mungu qnakwambia Mbele kuna Vita)

[emoji645] Kuota unanyonyesha Mtoto wakati hauna mtoto(Ni Ishara kuwa kuna maadui wananufaika na wewe bila wewe kujijua)

[emoji637][emoji646] Kuibiwa nguo kwenye ndoto(Ni Ishara kuwa adui anapanga kukuondolea Heshima na utukufi wako)

[emoji637][emoji637] Kuota umebeba mzigo mzito (Ni Ishara adui amekubebesha mizigo mizito)

[emoji637][emoji638] Kuota kofia yako imechukuliwa na upepo ( Ni Ishara ya kuaibishwa)

[emoji637][emoji639] Kuota upo katikati ya giza nene( Ni Ishara ya Upofu wa Kiroho unakuvamia)

[emoji637][emoji640] Kuota moto mkali unateketeza (Ni ishara ya mashambulizi ya Majanga kutokea)

[emoji637][emoji641] Kuota unafanya mitihani ila hujamaliza karatasi zikakusanywa (Ni Ishara kuwa Roho ya Kufeli inakuandama)

[emoji637][emoji642] Kuota Unasafiri ila hufiki unakokwenda(Ni Ishara adui anarefusha Mafanikio yako yasikufikie haraka)

[emoji637][emoji643] Kuota umepigwa risasi ( Ni Ishara kuwa adui anakurushia mashambulizi)

[emoji637][emoji644] Kuota umevaa nguo zilizochanika ( Ni Ishara ya roho ya Umaskini)

[emoji637][emoji645] Kuota uko kwenye mazingira Yamezungukwa na Vinyesi ( Ni Ishara ya Kuwa Ibilisi anafanya kila awezalo kukuzia Usiende Mbinguni)

[emoji638][emoji646] Kuota uko Uchi Ndotoni ( Ni Ishara ya kuaibishwa na kufedheheshwa)

[emoji638][emoji637] Kuota umepoteza pete ya ndoa au gauni ya harusi ( Ni Ishara kuna Mpango wa Mashambulizi dhidi ya ndoa yenu)

[emoji638][emoji638] Kuota mmevamiwa na kuibiwa ( Ni Ishara kuwa adui anapanga kuwaletea roho ya Umaskini au Ufakara na kupungukiwa)

[emoji638][emoji639] Kuota umeumwa na Mbwa ( Ni Ishara kuwa roho za Uzinzi na Uasherati zinakutesa)

[emoji638][emoji640] Kuota umeshambuliwa na Paka ( Ni Ishara ya Mashambulizi ya roho za Kichawi)

[emoji638][emoji641] Kuota unashambuliwa na Nyoka (Ujue adui anakutegea Sumu)

[emoji638][emoji642] Kuota umepoteza Fedha (Ni Ishara ya shambulio juu ya uchumi(

[emoji638][emoji643] Kuota kuna mtu anakulaani. (NI ishara kuwa bado kuna misingi ya laana haijavunjwa juu yako)

[emoji638][emoji644] Kuota unatokwa Damu puani na sehemu zingine za Mwili (Ni Ishara kuwa Kuna Mashambulizi juu ya Afya yako)

[emoji638][emoji645] Kuota uko sokoni unazunguka na hauna kiti cha kufanya ( Ni Ishara kuwa roho za Ukichaa zinakunyemelea)

[emoji639][emoji646] Kuota unafanya mapenzi Kwenye ndoto ( Ni Ishara kuwa unasumbuliwa na Roho ya Mahaba au Uzinzi)

[emoji639][emoji637] Kuota umevaa nguo za Msingi wakati wewe ni mtu mzima sasa ( Ni shara ya Kudumaa kimafanikio)

[emoji639][emoji638] Kuota Unakufa ( Ujue roho ya mauti ya Kiuchumi,kimwili kiafya inakuandama(

[emoji639][emoji639] Kuota majeneza au Makaburi ( Ni Ishara ya roho ya mauti inafanyakazi)

[emoji639][emoji640] Kuota unafukuzwa na Wanyama ( Ni ishara kuwa kuna Mashambulizi yalishaachiliwa juu yako katika ulimwengu wa roho)

[emoji639][emoji641] Kuota Ndege Bundi au Popo ( Ni ishara kuwa unasumbuliwa na roho ya unafiki na masengenyo)

[emoji639][emoji640] Kuota kuna Utando umekuzonga ( Ni ishara ya roho ya kukataliwa)

[emoji639][emoji641] Kuota umepoteza Vyeti vya Shule ( Ni ishara adui anakuzuia usipate kazi)

[emoji639][emoji642] Kuota umevaa Wigi Kwenye ndoto ( Ni Ishara ya utukufu Bandia juu yako)

[emoji639][emoji643] Kuota makufuli ( Ni ishara kuna maeneo fulani juu ya maisha yako yamefungwa)

[emoji639][emoji644] Kuota unalia ( Ishara ya roho ya huzuni)

[emoji639][emoji645] Kuota Umeangusha Biblia au Umeshindwa kusoma Neno ( Ni Ishara kuwa adui anataka kuliondoa Neno juu yako)

[emoji640][emoji646] Kuota unaogelea Kwenye Maji ( Ni Ishara roho za Majini zinakuandama)

[emoji640][emoji637] Kuota unatembea peku( Ni ishara ya roho ya umaskini na kwa wanandoa ni ishara ya Kuachana na mwenzi wako)

[emoji640][emoji638] Kuota umevaa manguo Meusi au Kofia nyeusi ( Ni Ishara bado kuna utawala wa Giza na Mapepo ndani yako)

Ukiota ndoto za namna hiyo hapo Juu yakupasa kuchukua Hatua za Kuomba Maombi ya Vita.

Mshirikishe Mwenzio tujifunze pamoja

MBARIKIWE NA MUNGU
 
nimeota nakula nyama mapande ya nguvu,ila sijui hata ni nyama gani,nashtuka nakuta tumbo limejaa,i mean nimeshiba.

Ile imani ya kwamba ndoto za aina hii zinakuaga na uhalisia yaweza kuwa kweli? mana naskia hadi kichefu chefu....K@$?#!6E....
Tarajia mafanikio makubwa yatayokutosha wewe na ukoo wako.
Hakuna uchawi hapo.
Kuota unaka nyama haina maana ni wachawi...
Sikia ndoto hutokana na source 3
Mungu....kusema na wewe.
Shetani...kukuonesha mipango yake mibaya juu yako...na hiii inatokea pale ambapo Anakuwa amebanwa na walinzi wa Mwanadamu...hivyo shetani hulazimishwa akioneshe mipango yake mibaya ili wewe uweze kuiepuka..

3.Mawazo yako mabaya au mazuri huleta ndoto.

Narudia ...Anza kusali sana...na omba Sasa hizo baraka za kishibishwa vinono zikiujilie upesi...

Utaanza kuwa na utosherevu wa kuyosha
Yani wewe
Uyakuja siku moja unishukuru
Usiikemee hyo ndoto
Sio ndoto mbaya.

Sema wanadamu wamekalili tafsiri walizosoma kwrnye Vitabu vya kina Mwingira na Gwajima...
 
Belo umefafanua vizuri sana hapo juu [emoji115]
 
Hii ndoto hata kama inahusishwa na ushirikina, mimi siamini!

Binafsi nishatandika sana minyama ya kuku nikiwa ndotoni na bado nadunda!

Mara nyingi kama sio zote, ndoto za aina hii unikuta kama nimelala bila kula!

So, nikiwa usingizini na minjaa njaa yangu, mara nyingi huota ndoto nikiwa nagonga menu!

Na kv even in a real world siwezi kutamani ugali kwa maharage, there's no way naweza kuota ndoto eti nakula ugali kwa maharage!

Kwahiyo hapo mwendo ni mijipaja ya kuku na maminofu ya nyama!
 
Ni ndoto ya kawaida. Kuepuka hilo kumbuka kunywa maji ya kutosha kabla ya kulala.
 
Tarajia mafanikio makubwa yatayokutosha wewe na ukoo wako.
Hakuna uchawi hapo.
Kuota unaka nyama haina maana ni wachawi...
Sikia ndoto hutokana na source 3
Mungu....kusema na wewe.
Shetani...kukuonesha mipango yake mibaya juu yako...na hiii inatokea pale ambapo Anakuwa amebanwa na walinzi wa Mwanadamu...hivyo shetani hulazimishwa akioneshe mipango yake mibaya ili wewe uweze kuiepuka..

3.Mawazo yako mabaya au mazuri huleta ndoto.

Narudia ...Anza kusali sana...na omba Sasa hizo baraka za kishibishwa vinono zikiujilie upesi...

Utaanza kuwa na utosherevu wa kuyosha
Yani wewe
Uyakuja siku moja unishukuru
Usiikemee hyo ndoto
Sio ndoto mbaya.

Sema wanadamu wamekalili tafsiri walizosoma kwrnye Vitabu vya kina Mwingira na Gwajima...
Ndugu hatugombani ila ukweli utabaki kuwa ukweli.Mungu anapomuonesha mtu kuwa mbele yako kuna neema zipo ishara za vitu ambavyo humuonesha ktk ndoto kama ifuatavyo.

1.kuna kuona mazao yamestawi yaani kijani kibichi.

2.kuna kuona unafungulia bomba maji.

3.kuna kuona unakunywa maziwa.

4.kuna kuona unapanda ngazi au ghorofa.

5.na ishara nyinginezo.
Nakataa kabisa kuwa kula nyama ndotoni ni neema haipo kabisa tena sahau.Soma vizuri biblia utajua vema nini maana ya damu na nyama.
Muda wa kufanikiwa ukifika Mungu atamwambia lakn kwa sasa anachoambiwa ni kinyume na usemacho wewe.
 
Ndugu hatugombani ila ukweli utabaki kuwa ukweli.Mungu anapomuonesha mtu kuwa mbele yako kuna neema zipo ishara za vitu ambavyo humuonesha ktk ndoto kama ifuatavyo.

1.kuna kuona mazao yamestawi yaani kijani kibichi.

2.kuna kuona unafungulia bomba maji.

3.kuna kuona unakunywa maziwa.

4.kuna kuona unapanda ngazi au ghorofa.

5.na ishara nyinginezo.
Nakataa kabisa kuwa kula nyama ndotoni ni neema haipo kabisa tena sahau.Soma vizuri biblia utajua vema nini maana ya damu na nyama.
Muda wa kufanikiwa ukifika Mungu atamwambia lakn kwa sasa anachoambiwa ni kinyume na usemacho wewe.
Mimi nimeota ninakulamahindi ya kuchoma.
Je, nitasubiri milele?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom