Kwa kadiri ya mawazo yangu....
Ni ujinga kuwaza kuwa kukopa na kuongeza kodi kwa watanzania ama katika huduma z a kijamii na kibiashara ndiyo njia pekee ya kuendesha shughuli za kimaendeleo nchini huku nchi ikiruhusu kupokea 4% ya mapato ya madini yake kwa wawekezaji wa nje. 50% peke yake ya makanikia tuliyokamata ilitosha kuinua uwekezaji wa ndani na nje ya nchi kusababisha ukuaji kiuchumi na kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana kwa kuwawezesha katika kilimo na usindikaji wa mazao. Fedha zilizowekezwa katika miradi ya kifisadi kama kule Chato na Dar es salaam zingewekezwa pia kuinua kilimo na viwanda leo hii tungeshuhudia kuimarika kwa shilingi ya Tanzania hadi kuwa $1 = Sh 1800 badala ya ilivyo sasa kuwa ni sh 2250! Vipaumbele vibovu na ufisadi wa uwekezaji kwenye mirdi isyozalisha haraka kama hii ya flyovers, pangaboi na treni ya mwendokasi ndivyo visababishi vikubwa kwa vichaa kuona njia pekee ya kupata pesa ni kuongeza kodi na gharama za huduma za jamii nchini
Niwie radhi na mimi nitoe maoni yangu kwa mawazo yangu! Kama kumbukumbu zetu zitakuwa sahihi, kulikuwa na mjadala mpana bungeni na nje ya bunge juu ya athari za kiuchumi zilizokuwa zinaisibu nchi kutokana na msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam. Mabilioni ya shilingi yamekuwa yakipotea kwa wafanyakazi na wadau wengineo wa maendeleo kupoteza muda mwingi kwenye foleni. Hivyo kuwekeza kwenye barabara za juu
(flyovers) kama mmoja ya mbinu za kukabiliana na changamoto hiyo (ambayo pia naamini imetoa ajira kwa vijana) haijawa ni mipango ya kifisadi kama utaona umuhimu wake. Uharibifu wa barabara kutokana na magari ya mizigo, nadhani ni sababu tosha ya kujenga reli mpya (ambayo pia imetoa ajira kwa vijana). Tunaweza tusione matokeo chanya sasa hivi, lakini naamini kitambo si kirefu, tutaona manufaa yake!
Kuhusu uwanja wa ndege Chato, kama tutakuwa na uelewa wa jiografia ya Ziwa Magharibi, na kuelewa makusudio ya kimkakati, naamini tutaondokana na tuhuma zisizokuwa na msingi za kuuona mradi huu kama wa kifisadi.
Aidha ni ukweli usiopingika kwamba ukopaji na nyongeza ya kodi sio njia pekee ya pato la taifa. Lakini pia si sahihi kuiona kodi kama balaa (sio kwa tafsiri yako). Tunapaswa kuchukulia ulipaji kodi kama mmoja wa wajibu wa kila anayestahiki kulipa kodi. Nchi zingine ni wakali zaidi kwenye masuala ya ukwepaji kodi. Ni vyema basi nasi tukajenga utamaduni wa kulipa kodi pasi shuruti.
Kuhusu mrabaha wa madini, ni kweli serikali (kupitia mikataba mibovu) iliingia kwenye mfumo wa utandawazi na uwekezaji kwenye madini bila kuandaa sera na sheria za ukusanyaji wa mapato kutokana na madini. Haiwezekani kutumia sheria ya madini juu ya mrabaha kwa kutumia kiwango kile kile ujichokuwa unawatoza wachimbaji wadogo wadogo ambao pia ulikuwa unakusanya / unanunua dhahabu yao (STAMICO) na kuweka akiba Benki Kuu na huyu mwekezaji mkuu anakulipa 3% na anakwenda na dhahabu yote kwao. Haiwezekani kuwapa likizo ya kodi (Holiday Tax) wakati wachimbaji wadogo wadogo / wachimbaji wazawa wanaminywa kodi! Haiwezekani!
Kwa kuwa tuko kwenye kipindi cha mabadiliko
(transition period), na kwa kuwa kila enzi na kitabu chake, ni vyema tukavuta subira na kuishauri serikali (kupitia majukwaa mbali mbali) juu ya njia mwafaka na yenye mtizamo chanya ya kutupeleka mbele. Tuikosoe kirafiki na kuipongeza pale inapofanya vizuri!
Tujitafakari!