Kuongeza kodi ni kuongeza umasikini...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Tangu serikali hii ya tano iingie umekuwepo na msisitizo wa kukusanya kodi mkubwa
lakini hata hivyo imekuwepo na tabia za kupandisha kodi maeneo mbalimbali kiholela

na hata hii bajeti ya sasa inaonesha wazi serikali hii ya awamu ya tano wanachotaka
wao ni kodi tu hata kama kodi hiyo 'itaua' baadhi ya biashara za watu....

Ukweli ni kwamba wanachokifanya ni 'kumkamua maradufu ng'ombe maziwa' huku ng'ombe mwenyewe
hana afya ya kutosha na chakula chake kinazidi kupungua......

Kwa mwendo huu umasikini utaongezeka......biashara zitakufa na hayo mapato yatapungua

Ilikuwa busara zaidi ng'ombe akaongezewa kwanza chakula na matunzo na hata kupunguza
kumkamua kwanza ili anawiri ndo ukamuaji ufuatie......

Mentality kuwa watanzania wengi wana pesa na hawalipi kodi ni hatari sana...
Ukweli ni kuwa watanzania wengi ni masikni na wanaishi kwa kubangaiza zaidi
biashara rasmi ni chache sana na gharama za umeme,kodi na nyinginezo ni kuubwa sana...

Serikali ilipaswa kutumia nguvu kubwa kwenye 'new economy' na Utalii...ambako hakuna
mafanikio ya kuridhisha......kuliko kukazania kuongeza kodi kwa mwananchi....

kodi zinavyo zidi na umasikini unazidi

.
 
Mkuu, tuliahidi kutoa ajira ndo maana twakaba kodi kila kona na hata kuiobgeza ili kutoa ajira zaidi!
 
Kwa nidhamu yetu ya woga,
Hapa Lumumba hawawezi kukubaliana napo,

Nimesikitika leo aliyekuwa kampeni meneja (Bulemboo)
Akisema bajeti hii ni chereko chereko kwa wamaskini....kweeeeli jamani?

Kweli shule ni muhimu mana huyu ni darasa la 7,
Ila kwa sisiem hata uwe nayo bado haitatumika.
 
Tangu serikali hii ya tano iingie umekuwepo na msisitizo wa kukusanya kodi mkubwa
lakini hata hivyo imekuwepo na tabia za kupandisha kodi maeneo mbalimbali kiholela

na hata hii bajeti ya sasa inaonesha wazi serikali hii ya awamu ya tano wanachotaka
wao ni kodi tu hata kama kodi hiyo 'itaua' baadhi ya biashara za watu....

Ukweli ni kwamba wanachokifanya ni 'kumkamua maradufu ng'ombe maziwa' huku ng'ombe mwenyewe
hana afya ya kutosha na chakula chake kinazidi kupungua......

Kwa mwendo huu umasikini utaongezeka......biashara zitakufa na hayo mapato yatapungua

Ilikuwa busara zaidi ng'ombe akaongezewa kwanza chakula na matunzo na hata kupunguza
kumkamua kwanza ili anawiri ndo ukamuaji ufuatie......

Mentality kuwa watanzania wengi wana pesa na hawalipi kodi ni hatari sana...
Ukweli ni kuwa watanzania wengi ni masikni na wanaishi kwa kubangaiza zaidi
biashara rasmi ni chache sana na gharama za umeme,kodi na nyinginezo ni kuubwa sana...

Serikali ilipaswa kutumia nguvu kubwa kwenye 'new economy' na Utalii...ambako hakuna
mafanikio ya kuridhisha......kuliko kukazania kuongeza kodi kwa mwananchi....

kodi zinavyo zidi na umasikini unazidi

.
Hebu orodhesha maeneo ambayo yameongezwa kodi kwa wananchi!...Nilitegemea uorodheshe hayo maeneo kwa mifano ili sote tuchambue...
 
Hebu orodhesha maeneo ambayo yameongezwa kodi kwa wananchi!...Nilitegemea uorodheshe hayo maeneo kwa mifano ili sote tuchambue...
Kwenye biashara zote dogo dogo kodi imeongezwa karibu Mara 3 yke mfano mm nina stationery mwaka juzi nmelipa laki 3 kwa mwaka lkn mwaka huu kodi milion moja kwa mwaka capital yngu yenyewe Mil 3 wapi na wapi Nchi hii ipo kwa ajiri ya wenye nacho nakuona mtu wa chini unazidi kurudi chini
b41ac912ef5ad6c795e1bdf6d3e41c39.jpg
 
Serikali ya awamu ya tano inadhani inawakomoa wafanyabiashara kumbe hasira zote zinarudi kwa wananchi wa hali ya chini.
Kama unaongeza makato kwenye transactions za ATM basi benki wataongeza riba ambayo wananchi wa kawaida wataumia tu.
Mfanyabiashara hakubali kuingia hasara hata siku moja.
 
Kariakoo na kwingineko biashara zimenuna, wanunuzi hakuna. Na hapohapo unataka alipe kodi. Ataitoa wapi?
Bandarini mizigo imeshuka, hata ile kidogo kidogo waliokuwa wanaipata hawaipati tena. Fedha itatoka wapi?
 
Kwenye biashara zote dogo dogo kodi imeongezwa karibu Mara 3 yke mfano mm nina stationery mwaka juzi nmelipa laki 3 kwa mwaka lkn mwaka huu kodi milion moja kwa mwaka capital yngu yenyewe Mil 3 wapi na wapi Nchi hii ipo kwa ajiri ya wenye nacho nakuona mtu wa chini unazidi kurudi chini
b41ac912ef5ad6c795e1bdf6d3e41c39.jpg
Sasa hapo mbona unafanya shughuli nyingi zaidi ya za stationary?
 
Nakubaliana nawe.

Ikumbukwe sekta binafsi ndizo zinazoajiri Watanzania wengi kuliko serikali ambao wanakadiriwa kuwa 500,000 sawa na asilimia 10% tu ya Watanzania karibia 50,000,000.

Kwa mantiki hiyo, iwapo taasisi za watu binafsi zitabanwa sana na kunyimwa fursa za kujiendesha biashara zao au taasisi hizo zitakufa na matokeo yake watu wengi watapoteza ajira na serikali itakosa mapato.

Kwa mfano tazama mfano hapa chini unao akisi bajeti ya 2016/2017:

1.Zabuni zote za matangazo,vyakula,usafiri,promotion n.k,zipewe kipaumbele kwa taasisi za serikali pekee.

2.Mikutano,makongamano,semina,zote zifanyikie kwenye kumbi za serikali.

Ni dhahiri kwamba kwa wafanya biashara waliokopa fedha kutoka katika mabenki wataathirika katika urejeshaji kutokana na mdororo wa biashara. Benki pia wataathirika.Serikali itaathirika.Walalahoi wataathirika zaidi....
 
Kazi tunayo... Shida ni serikali kutaka kuachieve 10 years success in one year.... They need to take it one step at a time

Tuna shida kubwa ya mifumo na efficiencies... Hata wakikusanya ngapi, bado matumizi yatatusumbua; vilevile if the government tightens everything sasa basi wanaweza kukausha kabisa vyanzo vya mapato na kutufanya tuanze upya

I hope kutakua na revision ya hizi hasty decisions
 
Back
Top Bottom