Kuonesha au kuonyesha?

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Kwa mara nyingi sasa nimekuwa nikiona watu wanaandika neno hili 'kuonesha'. Wakati mimi nasoma, na nimekuwa nikiandika pia kwa muda mrefu kwa lugha ya Kiswahili, nimekuwa nikitumia ' kuonyesha'. Nataka kuuliza hivi kuliandika neno hilo bila y ni kwa sababu ya lafudhi (dialect) tu, au limekubalika katika jamii? Ninavyoelewa mimi ni kuwa ukuandika, au kutanka 'kuonesha', unatumia lafudhi ya Zanzibar au Pemba. Sasa hili neno nalo limesambaa mpaka bara?
 
Samahani kama nitakuwa nimekosea kwasababu lugha siyo taaluma
yangu lakini ninavyo fahamu ni kuwa:

Onyesha inatokana na mzizi wa neno 'ONYA' yaani tahadhari kwahiyo
matumizi sahihi ya hili neno lazima yaendane na tahadhari. Vivyo
hivyo "onesha" inatokana na mzizi wa neno 'ONA' yaani tazama, angalia
n.k. Mtumiaji wa hili neno nilazima amaanishe uangalizi wa kitu fulani.
 
Neno onya linabakia hapo hapo. Huwezi kusema kuonyesha, ukimaanisha kutoa onyo. Ila linaweza kubadilika tu na kuwa 'onyo'.
 
Tofauti zote mbili zinakubalika na msingi wa tofauti uko kwenye lahaja tu. Kwa atumiaye "onyesha" na atumiaye "onesha" wote wako sawa! Na hata kamusi za TUKI zina neno "onyesha".

Mfano mwingine wa tofauti za lahaja ni neno "sifuri" ambapo "sufuri" pia inakubalika.

Hata kwenye Kiingereza pia kuna tofauti za lahaja. Kwa mfano, neno "skeptic". Wamarekani wanalitamka hivyo hivyo linavyoandikwa lakini Waingereza wanaliandika "sceptic" na kulitamka tofauti na walitamkavyo Wamarekani. Waingereza wao wanalitamka 'septic'
 
Back
Top Bottom