Kuondoka kwa Mbunge wa Monduli CHADEMA ni dalili ya Lowassa kuachana na siasa?

Nimeunusa uhusiano wa mbunge huyu kuliachia jimbo la Monduli na ile kesi ya mkwe wake Mamvi.

Huyu ni mtu mzuri sana wakati wa kampeni hakunitukana.
 
Mbowe alitumika kuua upinzani nchini bila kujielewa, tamaa yake mda mfupi inaathiri upinzani kwa miaka mingi ijayo.
Ni kweli kabisa, maana angalau nguvu ya CDM imekuwa ikileta changamoto kwa serikali ya CCM. Nguvu hiyo ikipotea litakuwa ni jambo baya kwa taifa na mustakabali wake.
 
Dr. slaa aliposema mambo ya Asset na liability aliwalenga watu alioamini sio wasafi wakiwa CCM HAWAPASWI Kukaribishwa CDM. Na aliwatolea mifano. Akawaita ni liability sio assets. Wakina Msindai, Mgeja nk.

Dr. slaa ambaye hata yeye amejiunga CCM na alikua na Kadi yake ya CCM, AMBAYO ALIKATAA KUICHANA WALA KUIRUDISHA alipokua CDM. KADI HII ilishawahi kuibua sintofahamu kipindi kile. Hii ina leta picha kua hata yeye ni liability kwasababu alijua ipo siku atatakiwa kurudi CCM ALIKOKULIA.

Ukweli ni kua Dola ina mkono 100% katika hamahama hii. Hakuna cha Lowasa wala unaabii wa Dr. slaa.
Ushahidi wa Madiwani kununuliwa ulishawahi kupelekwa hadi mahakamani ilibaki kidogo ukatize uhai wa Mbunge Nassari.

Mnyeti alishasema kuwa ni kweli wanawanunua wapinzani. Kwa sababu HAWAWATAKI na hawataki kushirikiana nao.
Kheri james pia. Nk.

Bwana mkubwa naye hajawahi kutaka kukaa Meza moja na wapinzani kuongea nao.

Kwa miaka yote 3. Tundu lisu hali yake si nzuri na hapati msaada wowote kutoka serikalini. Na Dr.Slaa amekataa kumpa Pole Tundu Lisu.
Hoja kuu ni Chadema kukiuka misingi yake ya Awali, kutoka kwenye kukemea ufisadi hadi kuwa watetezi wakuu wa mafisadi.

Wenye akili wote wakajiweka pembeni baada ya kuona chama hakieleweki kinasimamia nini na kinatetea nini.

Wakati ule watu walikipenda Chadema kwa sababu ya hoja zake za kitaifa.....

sasa hivi akiangalia kwa jicho la tatu watu wanaishabikia Chadema sababu ya chuki kwa Rais Magufuli.

Ila sio kwamba chadema wana hoja ama ushawishi wowote ule...

Sasa hivi Chadema hawana hoja zaidi ya Kukosoa bila kuonyesha mbadala ni nini...

Uamuzi wa kumleta Lowasa utaigharimu Tanzania miaka mingi ijayo kwenye siasa za Tanzania.
 
Ni muda mrefu kwa sasa kumekuwa na mvutano ndani ya familia ya Lowassa kuhusu hatma yake kisiasa.

Mke wa Lowassa na watoto wake wanataka Mzee aachane na siasa kwa sababu ya umri, afya na mazingira ya kisiasa kwa sasa lakini wapambe wa Lowassa kama kina Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania wanamshinikiza asiachane na siasa kwa sababu bado ana ''uwezekano mkubwa'' wa kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Mgeja na Sheikh Katimba wanajua kama Lowassa ataachana na siasa basi hata pesa wanazopata kama wapiga debe wa Lowassa zitakatika.

Tukio la Mbunge wa Monduli kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM limeanza kutoa picha halisi kuhusu hatma ya Lowassa ndani ya CHADEMA na katika siasa nchini.

Katika watu ambao walikuwa karibu sana na Edward Lowassa kisiasa wakati akiwa CCM na CHADEMA mmojawapo ni Julius Kalanga Laizer ambaye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia CHADEMA.

Julius Kalanga Laizer alikuwa ni mmoja wa watu ambao kama utataka kuonana na Lowassa wakati akiwa Mbunge lazima upitie kwake. Kwa maneno mengine alikuwa ni gatekeeper au kiunganishi cha Lowassa.

Mtu yeyote aliyetaka kugombea udiwani katika Jimbo la Monduli ilikuwa lazima kwanza akubaliwe na Julius Laizer akishirikiana na Isack Joseph na pia Paulo Kiteleki. Ikumbukwe kuwa bila ridhaa ya Lowassa kama unataka uongozi katika Jimbo la Monduli utakuwa unapoteza muda wako.

Lowassa baada ya kuachia Jimbo la Monduli aliamua kumkabidhi kijana wake Julius Kalanga Laizer ambaye alihama naye kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Kwa sasa Julius Laizer ameamua kurudi CCM na kwa maana hii kuna uwezekano mkubwa Lowassa ameishawaeleza vijana wake kama Laizer kuhusu hatma yake kisiasa ndani ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa madiwani zaidi ya 7 kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli wamejivua uanachama na kuhamia CCM.

Yajayo ndani ya CHADEMA yanafurahisha na kufikirisha!

Hii ndio faida ya mafuriko ya Edward Lowassa ambayo yako mbioni ‘’kuisomba’’ tena CHADEMA!

Swali la Dkt. Slaa bado VALID! Lowassa is an asset or a liability to the opposition party?
Mkuu kazi ya kupiga ramli waachie wenyewe.
 
Hizi dalili za awali kabisa za chama cha siasa ambacho kinaelekea kufa.

Bila shaka kuongoza vyama vya siasa kunahitaji "science" badala ya ujanja ujanja wa kupiga hela tu.
 
Mbowe kajenga upinzani kwa shida alafu amekuja kuubomoa mwenyewe! CCM wana take advantage tu.

Anachofanya Mbowe ni sawa na wanaapolo wanaochimba Tanzanite miaka 15 bila kupata chochote alafu mgodi ukitema fedha inafujwa miezi mitatu anaanza mizinga ya kumrudisha Mererani tena ....
Ni kweli wachache tulilaani na kupinga ujio wa Lowasa, ila wengi wakiongozwa na Mbowe walishangilia na bila kujua madhara ya baadaye.

Walitunanga zaidi baada ya kufanikiwa kuchukua halmashauriza majiji kadhaa, lakini wakasahau kuwa ushindi ule misingi yake ilitoka kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014.

Wakasahau kuwa ujio wa Lowasa sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga......

Ndio Dr.Slaa ilikuwa ngumu kuchukua nchi, lakini imani na heshima ya Chadema ingeendelea kuwa juu siku zote.....Chadema ingeelea kuzalisha vijana wengi waaminifu kwa chama hivyo kuwa na mtaji mkubwa wa wanachama na viongozi watarajiwa.
 
Siku akiondoka Lissu kwenda CCM ndivyo nami nitakapo kaa pembeni na Siasa.

Ila nyie wengine mwende tu.
Hizi kauli za kujifariji kwa sababu kuna wengine waliwahi kuapa kuwa kama Lowassa atajiunga CHADEMA watatembea uchi wiki nzima! Kilichoyanyika tunakujua na hao watu hawakuonekana tena.

Kwa kukusaidia, hakuna linaloshindikana kwa mwanasiasa.
 
Hakuna mvuto kwenye siasa.

Wananchi wanaojua maana ya siasa hawamchagui mwanasiasa kwa sababu anamvuto.

Swali la mvuto majibu yake yako chumbani!
Unajua huyu Wa kwenu kwa nini kula kitu anataka afanye yeye na anataka kionyeshwe live hata kama ni uzinduzi wa mabanda ya kuku?
Anataka kupata mvuto kwa nguvu
 
Kuondoka au kununuliwa,af kwa nini ununuzi huu unafanyika kipindi kukiwa na chaguzi ndogo?
 
Siku akiondoka TUNDU LISSU ndipo nami nitaachana na kufuatilia siasa.
 
Hizi kauli za kujifariji kwa sababu kuna wengine waliwahi kuapa kuwa kama Lowassa atajiunga CHADEMA watatembea uchi wiki nzima! Kilichoyanyika tunakujua na hao watu hawakuonekana tena.

Kwa kukusaidia, hakuna linaloshindikana kwa mwanasiasa.
Lissu si mwanasiasa, Lissu ni mwanaharakati
 
Siku akiondoka Lissu kwenda CCM ndivyo nami nitakapo kaa pembeni na Siasa.

Ila nyie wengine mwende tu.
Kama kuna watu sumu ni hawa wanaoweka imani yao kwa mtu badala ya chama. Mwanadamu tena mwanasiasa haaminiki ndugu, kama kuna mtu wa kumwamini ni wewe mwenyewe.
Nilitamani useme siku cdm ikibadilisha misingi yake ndio nitahama au siku cdm ikijiunga na ccm ndio na mimi nitajiunga.
 
Jiwe ndiye Strongman aliyebaki hivi sasa anayeangamiza upinzani na wapinzani.

Na Sio Udhaifu wa CDM bali ni Nguvu ya Serikali na vyombo vyake. Imeonekana kua Afya ya CCM n Serikali yake inategemea zaidi uwepo wa CDM dhaifu na upinzani dhaifu

Manake hata uko CuF hali ni hiyohiyo. Huwezi sema kuna ombwe la Lipumba.

Wabunge wa upinzani wanajisalimisha tu. Kwasababu hakuna namna; hata Maendeleo huwezi kupeleka tena ukiwa Upinzani.
Na watendaji wa Serikali wanasema haya waziwazi kwenye mikutano hawafichi. Ilani inayotekelezwa ni ya CCM TU.
Mkuu kumbuka siasa za Tanzania zina msingi unaochagizwa na maneno yanayosema, ''the winner takes it all AKA zero sum game''
 
Back
Top Bottom