Kuondoka kwa Mbunge wa Monduli CHADEMA ni dalili ya Lowassa kuachana na siasa?

Umeandika vizuri.
Ila Hapo mwisho ulipomuweka Dr. slaa umeharibu kila kitu. Masuala ya Asset na liability hayakua na maana hiyo.
Masuala ya asset na liability wewe uliyaelewaje? Ni wazi hukuelewa Dr. Slaa alimaanisha nini.
 
Chadema bado wako imara Sana Sana, ccm wakitaka kujua uimara wa upinzani waache kutumia Vyombo vya dola
 
Hizi filamu zipo Tanzania tu !
Hata huko Marekani kwenye uchu wa maendeleo hili hakuna..
Watu hujiunga na vyama kabla ya uchaguzi ili kuomba nafasi ya kuwakilisha wananchi. Awamu hii wanajiunga baada ya kuchaguliwa ili uchaguzi urudiwe tena..
Unahama kwako ili ukaunge mkono kiongozi wa CCM, kwanini hili hukuliona kabla ya kuchaguliwa ukaenda huko mapema ili kuepuka gharama ?
Je huko CCM hakuna watu wa kutosha kumuunga mkono huyo jamaa ?
Unajiunga na CCM ili aliyeko CCM atumbuliwe na nafasi yake upewe wewe..
Kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni takriban Tshs milioni 600. Na kwa uchaguzi wa mbunge mmoja ni bilioni moja na point kodi za Watanzania..
Huku kuwazihaki Watanzania ambao CCM huwaita vilaza, mafala..
Je kiongozi wa CCM hawezi kuwaunganisha Watanzania wakiwa katika vyama tofauti kwa sababu tu ya tofauti za kiitikadi ?
Je siku watanzania wote wakihamia CCM je ataweza kuwaunganisha wakiwa kwenye makabila tofauti na dini zenye itikadi tofauti ?
Tayari kuna malalamiko ya udini na ukabila..
Watanzania wengi sasa hivi ukiacha wale ccm wanaoishi kwa kodi zetu, wanaishi maisha magumu..
Movie liendelee !
 
Kisa cha Lowasa na Chadema ni kisa cha Samsoni na Wafilisti pale alipoomba nguvu mara moja tu ila aliwaua siku hiyo ni wengi kuliko wengine wote
 
Geez Lowassa kaivunjilia mbali cdm na alipoondoka CCM aliiacha vipandevipande. Kweli jamaa ni divisive figure. Lowassa ni liability Chadema. DK Slaa was absolutely right.
 
Katika geography, niliwahi kusoma vitu vinaitwa "SWASH and BACKWASH!"... nafikiri wakati tunafurahia mafuriko kupita tulisahau yakirudi itakuwa Backwash!
 
Masuala ya asset na liability wewe uliyaelewaje? Ni wazi hukuelewa Dr. Slaa alimaanisha nini.

Dr. slaa aliposema mambo ya Asset na liability aliwalenga watu alioamini sio wasafi wakiwa CCM HAWAPASWI Kukaribishwa CDM. Na aliwatolea mifano. Akawaita ni liability sio assets. Wakina Msindai, Mgeja nk.

Dr. slaa ambaye hata yeye amejiunga CCM na alikua na Kadi yake ya CCM, AMBAYO ALIKATAA KUICHANA WALA KUIRUDISHA alipokua CDM. KADI HII ilishawahi kuibua sintofahamu kipindi kile. Hii ina leta picha kua hata yeye ni liability kwasababu alijua ipo siku atatakiwa kurudi CCM ALIKOKULIA.

Ukweli ni kua Dola ina mkono 100% katika hamahama hii. Hakuna cha Lowasa wala unaabii wa Dr. slaa.
Ushahidi wa Madiwani kununuliwa ulishawahi kupelekwa hadi mahakamani ilibaki kidogo ukatize uhai wa Mbunge Nassari.

Mnyeti alishasema kuwa ni kweli wanawanunua wapinzani. Kwa sababu HAWAWATAKI na hawataki kushirikiana nao.
Kheri james pia. Nk.

Bwana mkubwa naye hajawahi kutaka kukaa Meza moja na wapinzani kuongea nao.

Kwa miaka yote 3. Tundu lisu hali yake si nzuri na hapati msaada wowote kutoka serikalini. Na Dr.Slaa amekataa kumpa Pole Tundu Lisu.
 
Last edited:
Magufuli hakuwa kabisa chaguo la wanaCCM na yeye analijua hilo. Na kwa kuwa ni mtu wa visasi na kuhold grudges ANAWASOMESHA namba kwelikweli. Anatengeneza CHAMA CHAKE TU NDANI YA CHAMA ( KUNDI LAKE TUKUFU LA KUMWIMBIA NA KUMWAMBUDU ).

WanaCCM wengine watakuja kushtuka KUSHAPAMBAZUKA. Kilele cha yote haya ni KURA YA MAONI 2019 hapo ndio kutakuwa na CCM PURE PRO- MAGUFULI atakaowaambia inama wanainama, inuka wanainuka siyo hii ya sasa kuna wanafiki VUGUVUGU kina NAPE na BASHE.
 
Mbowe alitumika kuua upinzani nchini bila kujielewa, tamaa yake mda mfupi inaathiri upinzani kwa miaka mingi ijayo.
Mbowe kajenga upinzani kwa shida alafu amekuja kuubomoa mwenyewe! CCM wana take advantage tu.

Anachofanya Mbowe ni sawa na wanaapolo wanaochimba Tanzanite miaka 15 bila kupata chochote alafu mgodi ukitema fedha inafujwa miezi mitatu anaanza mizinga ya kumrudisha Mererani tena ....
 
Dr. slaa aliposema mambo ya Asset na liability aliwalenga watu alioamini sio wasafi wakiwa CCM HAWAPASWI Kukaribishwa CDM. Na aliwatolea mifano. Akawaita ni liability sio assets. Wakina Msindai, Mgeja nk.

Dr. slaa ambaye hata yeye amejiunga CCM na alikua na Kadi yake ya CCM, AMBAYO ALIKATAA KUICHANA WALA KUIRUDISHA alipokua CDM. KADI HII ilishawahi kuibua sintofahamu kipindi kile. Hii ina leta picha kua hata yeye ni liability kwasababu alijua ipo siku atatakiwa kurudi CCM ALIKOKULIA.

Ukweli ni kua Dola ina mkono 100% katika hamahama hii. Hakuna cha Lowasa wala unaabii wa Dr. slaa.
Ushahidi wa Madiwani kununuliwa ulishawahi kupelekwa hadi mahakamani ilibaki kidogo ukatize uhai wa Mbunge Nassari.

Mnyeti alishasema kuwa ni kweli wanawanunua wapinzani. Kwa sababu HAWAWATAKI na hawataki kushirikiana nao.
Kheri james pia. Nk.

Bwana mkubwa naye hajawahi kutaka kukaa Meza moja na wapinzani kuongea nao.

Kwa miaka yote 3. Tundu lisu hali yake si nzuri na hapati msaada wowote kutoka serikalini. Na Dr.Slaa amekataa kumpa Pole Tundu Lisu.
Tafsiri feki! Alafu haisaidii mzee ...hiyo kauli ni kama jinamizi huko Chadema ....makamanda wanakufa kiume tu ....
 
Back
Top Bottom