Kuondoka kwa Mbunge wa Monduli CHADEMA ni dalili ya Lowassa kuachana na siasa?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Ni muda mrefu kwa sasa kumekuwa na mvutano ndani ya familia ya Lowassa kuhusu hatma yake kisiasa.

Mke wa Lowassa na watoto wake wanataka Mzee aachane na siasa kwa sababu ya umri, afya na mazingira ya kisiasa kwa sasa lakini wapambe wa Lowassa kama kina Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania wanamshinikiza asiachane na siasa kwa sababu bado ana ''uwezekano mkubwa'' wa kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Mgeja na Sheikh Katimba wanajua kama Lowassa ataachana na siasa basi hata pesa wanazopata kama wapiga debe wa Lowassa zitakatika.

Tukio la Mbunge wa Monduli kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM limeanza kutoa picha halisi kuhusu hatma ya Lowassa ndani ya CHADEMA na katika siasa nchini.

Katika watu ambao walikuwa karibu sana na Edward Lowassa kisiasa wakati akiwa CCM na CHADEMA mmojawapo ni Julius Kalanga Laizer ambaye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia CHADEMA.

Julius Kalanga Laizer alikuwa ni mmoja wa watu ambao kama utataka kuonana na Lowassa wakati akiwa Mbunge lazima upitie kwake. Kwa maneno mengine alikuwa ni gatekeeper au kiunganishi cha Lowassa.

Mtu yeyote aliyetaka kugombea udiwani katika Jimbo la Monduli ilikuwa lazima kwanza akubaliwe na Julius Laizer akishirikiana na Isack Joseph na pia Paulo Kiteleki. Ikumbukwe kuwa bila ridhaa ya Lowassa kama unataka uongozi katika Jimbo la Monduli utakuwa unapoteza muda wako.

Lowassa baada ya kuachia Jimbo la Monduli aliamua kumkabidhi kijana wake Julius Kalanga Laizer ambaye alihama naye kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Kwa sasa Julius Laizer ameamua kurudi CCM na kwa maana hii kuna uwezekano mkubwa Lowassa ameishawaeleza vijana wake kama Laizer kuhusu hatma yake kisiasa ndani ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa madiwani zaidi ya 7 kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli wamejivua uanachama na kuhamia CCM.

Yajayo ndani ya CHADEMA yanafurahisha na kufikirisha!

Hii ndio faida ya mafuriko ya Edward Lowassa ambayo yako mbioni ‘’kuisomba’’ tena CHADEMA!

Swali la Dkt. Slaa bado VALID! Lowassa is an asset or a liability to the opposition party?
 
Last edited:
JPM na Lowassa nani mwenye mvuto wa kisiasa zaidi? Siasa is not abt age au rafiki ako iko wapi Trump is 75 bado anaushawishi....swali nzuri kuuliza je Jpm ni mzigo kwa chama chake au ni slow poisoning wa chama?
 
Hakuna mvuto kwenye siasa.

Wananchi wanaojua maana ya siasa hawamchagui mwanasiasa kwa sababu anamvuto.

Swali la mvuto majibu yake yako chumbani!
 
Swali la Dkt. Slaa wamelikataa wengi ndani ya CHADEMA lakini ni swali ambalo linatoa picha halisi kwa sasa.

Ukiukataa ukweli haina maana kuwa utabadilika kuwa uwongo!

Jiwe ndiye Strongman aliyebaki hivi sasa anayeangamiza upinzani na wapinzani.

Na Sio Udhaifu wa CDM bali ni Nguvu ya Serikali na vyombo vyake. Imeonekana kua Afya ya CCM n Serikali yake inategemea zaidi uwepo wa CDM dhaifu na upinzani dhaifu

Manake hata uko CuF hali ni hiyohiyo. Huwezi sema kuna ombwe la Lipumba.

Wabunge wa upinzani wanajisalimisha tu. Kwasababu hakuna namna; hata Maendeleo huwezi kupeleka tena ukiwa Upinzani.
Na watendaji wa Serikali wanasema haya waziwazi kwenye mikutano hawafichi. Ilani inayotekelezwa ni ya CCM TU.
 
Last edited:
JPM na Lowassa nani mwenye mvuto wa kisiasa zaidi? Siasa is not abt age au rafiki ako iko wapi Trump is 75 bado anaushawishi....swali nzuri kuuliza je Jpm ni mzigo kwa chama chake au ni slow poisoning wa chama?
Swali zuri sana!
 
Suala la Lowassa kurudi CCM halihitaji kuwa Sheikh Yahya...very soon atarudi alikotoka ili mambo yake binafsi na kifamilia yaende vizuri
 
Ni muda mrefu kwa sasa kumekuwa na mvutano ndani ya familia ya Lowassa kuhusu hatma yake kisiasa.

Mke wa Lowassa na watoto wake wanataka Mzee aachane na siasa kwa sababu ya umri, afya na mazingira ya kisiasa kwa sasa lakini wapambe wa Lowassa kama kina Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania wanamshinikiza asiachane na siasa kwa sababu bado ana ''uwezekano mkubwa'' wa kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Mgeja na Sheikh Katimba wanajua kama Lowassa ataachana na siasa basi hata pesa wanazopata kama wapiga debe wa Lowassa zitakatika.

Tukio la Mbunge wa Monduli kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM limeanza kutoa picha halisi kuhusu hatma ya Lowassa ndani ya CHADEMA na katika siasa nchini.

Katika watu ambao walikuwa karibu sana na Edward Lowassa kisiasa wakati akiwa CCM na CHADEMA mmojawapo ni Julius Kalanga Laizer ambaye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia CHADEMA.

Julius Kalanga Laizer alikuwa ni mmoja wa watu ambao kama utataka kuonana na Lowassa wakati akiwa Mbunge lazima upitie kwake. Kwa maneno mengine alikuwa ni gatekeeper au kiunganishi cha Lowassa.

Mtu yeyote aliyetaka kugombea udiwani katika Jimbo la Monduli ilikuwa lazima kwanza akubaliwe na Julius Laizer akishirikiana na Isack Joseph na pia Paulo Kiteleki. Ikumbukwe kuwa bila ridhaa ya Lowassa kama unataka uongozi katika Jimbo la Monduli utakuwa unapoteza muda wako.

Lowassa baada ya kuachia Jimbo la Monduli aliamua kumkabidhi kijana wake Julius Kalanga Laizer ambaye alihama naye kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Kwa sasa Julius Laizer ameamua kurudi CCM na kwa maana hii kuna uwezekano mkubwa Lowassa ameishawaeleza vijana wake kama Laizer kuhusu hatma yake kisiasa ndani ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa madiwani zaidi ya 7 kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli wamejivua uanachama na kuhamia CCM.

Yajayo ndani ya CHADEMA yanafurahisha na kufikirisha!

Hii ndio faida ya mafuriko ya Edward Lowassa ambayo yako mbioni ‘’kuisomba’’ tena CHADEMA!

Swali la Dkt. Slaa bado VALID! Lowassa is an asset or a liability to the opposition party?

Wewe ndo yule mtoto wa Lowassa aitwaye Freddy?
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom