Kuondoa shilingi ni mchezo wa kuigiza!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,215
2,000
Katika hili bunge la bajeti linaloendelea sasa hivi, pamoja na kwamba limekosa mvuto kutoka kwa jamii ya watanzania, kuna mambo matatu nimeyagundua. Kwanza, huu utaratibu wa kuondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kama mchezo wa kuigiza kwa kuwa wabunge wanaoshika hizo shilingi hatimaye huziachia na vifungu vya ovyo vya bajeti hupitishwa.

Pili, kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge hili nimeshuhudia wabunge wa CCM wakiondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri wa chama chao. Nadhani ni muendelezo ule ule wa kuleta mzaha na kuwakoga wananchi wanaowatazama ili waone kwamba wana uchungu na maendeleo yao wakati si kweli. Lakini pia wanafanya hivyo ili kufuata mkumbo wa wabunge wa UKAWA ambao tangu mwanzo walitahadharisha kushika shilingi za mishahara ya mawaziri ambao wameshindwa kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Kinachowaponza wabunge wa UKAWA ni uchache wao kwani hata kama wakishika shilingi, mwisho wa siku wabunge wa CCM watapiga kura za Ndiyooooooooooooooo ili kuwaokoa mawaziri wao wa CCM.

Tatu, nimegundua kwamba mle bungeni kuna wabunge wa CCM ambao wao kazi yao kubwa wanayoijua ni kusema NDIYOOOOOOOOOOO kwa sauti kubwa ili vifungu vya bajeti, hata vile vibovu, vipite bila kupingwa. Kundi hili huwa halichangii chochote bungeni. Wakishaingia bungeni wakasaini kwenye kitabu cha posho, hukaa mezani na kusubiri kugonga meza. Hili ni suala la kustaajabisha sana kwani wabunge hawa wametumwa na wananchi waende kuwawakilisha lakini wamegeuka kuwa wachumia tumbo na watetezi wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wananchi. Na kwa kuwa moja ya kazi ya wabunge ni kuibana serikali iwahudumie wananchi, wabunge hawa wa CCM ni wasaliti wa wapiga kura wao na hawafai kurejeshwa bungeni tena msimu ujao. Inasikitisha sana kuona kwamba wabunge hawa wa CCM wapo bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wananchi badala ya kuwatetea!

cc:[MENTION]lusungo[/MENTION] Lizaboni Nyani Ngabu Ritz FaizaFoxy mwa Mchambuzi MSALANI sokwe[MENTION]siafu dume[/MENTION]

:yield:
 
Last edited by a moderator:

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Kuondoa shillingi ni simply kutaka hoja hiyo ijadiliwe zaidi, mwisho wa siku ikiwa mbunge kapata majibu ya kuridhisha kwanini aendelee kushika hiyo shillingi? na akiendelea kushika hiyo shillingi maana yake inapigwa kura. Hapo inategemea na waliokuunga au kutokukuunga mkono hoja yako, mara nyingi upinzani hushindwa hapo kwa uchache wao bungeni.

Hilo la kusema kwa mara ya kwanza wewe unayaona, hiyo ni kuonesha kuwa kwa mara ya kwanza wewe unafatilia mambo ya bungeni. Hata ilipokuwa chama kimoja bungeni walikuwa wanazuwiliana shilingi, tuulize tuliokuwepo enzi hizo.
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
Wabunge wengi hasa wa ccm wanawakilisha chama badala ya wananchi waliowachagua, wabunge wa upinzani ingawa sio wote wameonyesha kutoa uwakilishi uliotukuka kwa umma wa watanzania pamoja na uchache wao! Wito wangu kwa watanzania wenzangu mwaka 2015 tuwaongeze wabunge wa upinzani kwa kuwaondoa wagonga meza wengi waliopo upande wa ccm!
 
Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,944
1,500
...time will come ambapo yanayompata mama banda yatawapata ccm,wameshindwa kuonyesha wao ni watu makini na wanastahili kushika dola...
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,698
2,000
Katika hili bunge la bajeti linaloendelea sasa hivi, pamoja na kwamba limekosa mvuto kutoka kwa jamii ya watanzania, kuna mambo matatu nimeyagundua. Kwanza, huu utaratibu wa kuondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kama mchezo wa kuigiza kwa kuwa wabunge wanaoshika hizo shilingi hatimaye huziachia na vifungu vya ovyo vya bajeti hupitishwa.

Pili, kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge hili nimeshuhudia wabunge wa CCM wakiondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri wa chama chao. Nadhani ni muendelezo ule ule wa kuleta mzaha na kuwakoga wananchi wanaowatazama ili waone kwamba wana uchungu na maendeleo yao wakati si kweli. Lakini pia wanafanya hivyo ili kufuata mkumbo wa wabunge wa UKAWA ambao tangu mwanzo walitahadharisha kushika shilingi za mishahara ya mawaziri ambao wameshindwa kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Kinachowaponza wabunge wa UKAWA ni uchache wao kwani hata kama wakishika shilingi, mwisho wa siku wabunge wa CCM watapiga kura za Ndiyooooooooooooooo ili kuwaokoa mawaziri wao wa CCM.

Tatu, nimegundua kwamba mle bungeni kuna wabunge wa CCM ambao wao kazi yao kubwa wanayoijua ni kusema NDIYOOOOOOOOOOO kwa sauti kubwa ili vifungu vya bajeti, hata vile vibovu, vipite bila kupingwa. Kundi hili huwa halichangii chochote bungeni. Wakishaingia bungeni wakasaini kwenye kitabu cha posho, hukaa mezani na kusubiri kugonga meza. Hili ni suala la kustaajabisha sana kwani wabunge hawa wametumwa na wananchi waende kuwawakilisha lakini wamegeuka kuwa wachumia tumbo na watetezi wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wananchi. Na kwa kuwa moja ya kazi ya wabunge ni kuibana serikali iwahudumie wananchi, wabunge hawa wa CCM ni wasaliti wa wapiga kura wao na hawafai kurejeshwa bungeni tena msimu ujao. Inasikitisha sana kuona kwamba wabunge hawa wa CCM wapo bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wananchi badala ya kuwatetea!

cc:[MENTION]lusungo[/MENTION] Lizaboni Nyani Ngabu Ritz FaizaFoxy mwa Mchambuzi MSALANI sokwe[MENTION]siafu dume[/MENTION]

:yield:
masahihisho kidogo, si wabunge wote waliotumwa na wananchi, wabunge wa viti maalum ni nafasi za viburudisho vya magamba fc na kwenye katiba mpya futilia mbali vitu maalum.
 
Last edited by a moderator:

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
masahihisho kidogo, si wabunge wote waliotumwa na wananchi, wabunge wa viti maalum ni nafasi za viburudisho vya magamba fc na kwenye katiba mpya futilia mbali vitu maalum.
uko sahihi mkuu, katika viti maalumu hata wa upinzani wapo ambao nao ni mizigo mfano letisia nyerere, ingawa upande wa ccm ndo wengi zaidi...
 
Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,766
2,000
Bunge limekuwa chanzo cha vimisemo vya ajabu ajabu tu.

Bunge limegeuka kuwa ni mbadala wa kikao cha CCM kilichoalika watazamaji(wao huwaita wapiga kelele) wachache,kwani mwisho wa siku hutumia wingi wao kupitisha matakwa yao.

Bunge limegeuka kuwa ni sehemu ya kuwadanganyia watanzani kuwa serikali yao imefanikisha na inaendelea kuimarisha miradi mingi ya maendeleo,na kuwa kipindi kifupi kijacho tutakuwa na mafanikio makubwa ili hali miradi mingi ya maendeleo imetegeshwa kuja kuzinduliwa pale uchaguzi mkuu wa 2015 utakapokaribia.

Bunge limegeuka kuwa ni sehemu ya wachache(Lukuvi na wenzake) kujifunzia busara ili hali wananchi tunawajua kuwa ni mambumbu na vinara wa siasa nyepesi na zisizo na tija.

Watanzania tuko sawa kihali,maisha hata vipaumbele...wachache walituibia kupitia baba zao,na wao wanaendelea kupokezana kijiti kana kwamba wao ni wateulekwa nafasi hizo.

Tubadilike #changeTanzania
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
597
250
Siku hizi mpaka hakuna mvuto kila mbunge anatishia kutoa shilingi. Enzi za kina Mudhihiri walikuwa wanatikisa bunge kwa hoja zao. Lakini hawa wa siku hizi jambo la kawaida utasikia natoa shilingi.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Ni utaratibu mzuri kwa wenye dhati moja ya kusukuma gurudumu ila kwa nchi hii hamna kitu sawa na rasilimali zilizopo!!!!!
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Katika historia ya Bunge la JMT, mbunge ambaye aliwahi KUSHIKIRIA SHILINGI YA WAZIRI akiwa na dhamira kweli ya kuishikiria na ali manusura bunge livunjike. Rais kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya, alikuwa JENERALI TWAHA ULIMWENGU 1990(?). Nakumbuka bunge liliahirishwa zaidi ya mara 2 kumshawishi Jenerali Ulimwengu kurudisha shilingi ya waziri. Jenerali Ulimwengu wakati huo akiwa na back up ya G55. Nakumbuka hadi TISS waliingilia kati kumshawishi Ulimwengu kurudisha shilingi ya Waziri. Wakati huo vikao vya bunge la JMT vikafanyika pale Karimjee!
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,215
2,000
Huu mchezo wa kuigiza ipo siku utafikia tamati. Haiwezekani kuwalaghai wananchi kwa bajeti hewa huku miradi ya maendeleo ikishindwa kutekelezwa na wananchi wakizidi kutopea kwenye umasikini. Hata punda akibebeshwa mizigo kwa muda mrefu sana ipo siku hughairi na kumpiga mateke, na hata kumuua mtu anayembebesha hiyo mizigo. Ijapokuwa maigizo haya yameanza siku nyingi sana, tamati yake haipo mbali sana kuanzia sasa.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,215
2,000
uko sahihi mkuu, katika viti maalumu hata wa upinzani wapo ambao nao ni mizigo mfano letisia nyerere, ingawa upande wa ccm ndo wengi zaidi...

MASAHIHISHO: Leticia Nyerere ni mbunge wa CCM, sio wa UKAWA. Wabunge wengi wa UKAWA wako makini kuliko wa magamba.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
MASAHIHISHO: Leticia Nyerere ni mbunge wa CCM, sio wa UKAWA. Wabunge wengi wa UKAWA wako makini kuliko wa magamba.

Nimetemblea website ya bunge la JMT, kujiridhisha usahihi wa takwimu zako na kukuta kwamba Leticia Nyerere ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA.
 
Escardo-bird

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
622
195
Wabunge wengi hasa wa ccm wanawakilisha chama badala ya wananchi waliowachagua, wabunge wa upinzani ingawa sio wote wameonyesha kutoa uwakilishi uliotukuka kwa umma wa watanzania pamoja na uchache wao! Wito wangu kwa watanzania wenzangu mwaka 2015 tuwaongeze wabunge wa upinzani kwa kuwaondoa wagonga meza wengi waliopo upande wa ccm!

Yaan me roho inaniumaga nikiona nchi yetu na utajiri wake wanao nufaika ni wachache na familia zao kwa cost ya watanzania walala hoi upinzani maskini wanajitahidi lakn wameshikilia makali mpini wamekamata tawala.
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
17,788
2,000
Ivi shilingi bado inathamani kiasi icho!?
Ivi inanunua nini kwa sasa?!
Kwanini wasiseme natoa milioni 7 kwenye mshahara wa waziri!
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Mchezo wa kuigiza ndiyo sera yao mpya Magamba. Huwaoni akina Kinana na Nape wanavyowapa kielelezo Viongozi wengine wa Chama chao, kwa kuigiza kula kwa mama nitilie; kula mahindi ya kuchoma, mitaani; ufundi uashi, kusukuma vitoroli vya watoto vijijini, kupanda bajaji, na kupanda treni ya TAZARA!!!!??????
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom