Bungeni: Wabunge wanapokuwa wanasema wanashikilia au kuondoa shilingi wanakuwa na maana gani?

Mchezo wa kuigiza ndiyo sera yao mpya Magamba. Huwaoni akina Kinana na Nape wanavyowapa kielelezo Viongozi wengine wa Chama chao, kwa kuigiza kula kwa mama nitilie; kula mahindi ya kuchoma, mitaani; ufundi uashi, kusukuma vitoroli vya watoto vijijini, kupanda bajaji, na kupanda treni ya TAZARA!!!!??????

Wanatekeleza ilani ya chama:

kinana na maigizo.jpg

magamba malaya.jpg
 
Nasikia kuna wale mawaziri wanaoongoza kwa sura mbaya bungeni ''wanawatumia'' sana wabunge hasa wa viti maalum
 
Pamoja na hayo maigizo ya kuondoa shilingi yanayofanywa na wabunge wa CCM, bajeti za ovyo na ambazo haziwanufaishi wananchi zimeendelea kupitishwa kila kukicha.

bajeti--serikali+wananchi.jpg
 
Haka kamsemo huwa nakasikia sana bungeni kakizungumzwa na baadhi ya wabunge kuwa nashikilia shilingi au sitoi shilingi, sasa bado nimeshindwa elewa kuwa maana yake ni nini...

Naombeni kwa mnaojua tuambizane kama linatumika badala ya neno fulani kwann lisisemwe hilo neno ili kuondoa ugumu kwani naamin wengi hawajui maana ya kushika shilingi.

Japokuwa linaleta radha fulani lakini huwa silielewi kabisa a hili neno... Hebu sasa tujuzane huwa lina maanisha nn

Mm naachia shilingi mjadala uanze sasa...

Karibuni
===============
Wenu

Kalenga kidamali
 
Shillingi inaweza kua inahusika na mshahara wa Waziri. Ngoja wajuzi wa mambo waje
 
Wana maana ya credit mkuu mfano,kama kuna wizara flan imetoa mapendekezo ya kuomba kiasi flan cha pesa wabunge wote lazima wachangie ndo weingine wanazuia shilingi au kumpa shilingi waziri husika
 
Bunge linapokaa kama kamati kupitisha vifungu/vote vilivyoainishwa kwenye bajeti, inapofika vote inayohusu mshahara wa waziri mbunge anaamua kushikilia shilingi kifungu kile kisipitishwe kwa kutoa hoja ijadiliwe hadi pale atakaporidhika. Bunge lilkikubali kupitisha hoja iliyotolewa na mbunge ya kuzuia mshahara wa waziri (ambapo haijawahi kutokea kwa wabunge kukubali ) basi waziri huyo hatarini kung'atuka
 
Soma hapa jaridahuru.blogspot.co.ke/2014/05/bungeni-je-unafahamu-maana-ya-kuondoa.html?m=1
 
Daaah sisi wauswahilini tunawaelewa vibaya...........................mwanaume akisema ameondoa shilingi anatuchanganya sana sisi wa uswahilini
 
Kila ukisikiliza bunge Haya mambo matatu yanatamkwa kwa kujirudia rudia sana lakini sijui na naamini watu wengi pia hawajui maana yake au tija yake kwenye mijadala na maamuzi ya bunge.

1. KUSHIKA SHILINGI
Huwa ina maana gani mbunge kushika shilingi katika mshahara wa waziri? Asipoichilia hiyo shilingi nini kitakwama?
Faida gani inapatikakana kwa shilingi kushikwa?

Katika historia ya bunge kuna mbunge aliwahi kushika shilingi mpaka mwisho bila kuiachia au huwa ni kutishia tu?

2. KUZUNGUMZA NA KITI
Huwa ina maana gani Spika au naibu spika ambaye huwa ndio namsikia mara nyingi sana akiwaambia wabunge wanazungumza na KITI sio watu wengine? Mbunge anapochangia si anailekeza hoja yaka kwa bunge zima na wote wanaomsikiliza au ni vinginevyo?

3. TAARIFA
Mara nyingi tumeona mijadala mizuri ya mbunge mmoja ikiharibiwa na kitu kinaitwa taarifa kutoka kwa upande mwingine.

Kwanini mchangiaji huwa anaulizwa kama anaikubali au anaikataa taarifa wakati hakuna hata akiikataa hawezi fanywa chochote? Kwa nini taarifa isitolewe baada ya mchangiaji kumaliza kabisa kutoa hoja yake na kuepusha malumbano ya muda?
 
Hao hakuna wanachosaidiaga maana serikali ikipanga bajeti kelele zao huwa ni sawa na kelele za mlango hazimtishi mwenye nyumba.
 
Natazama Bunge hapa la 12 mkutano wa Saba 7 kikao Cha 29 hoja inayozungumziwa hapa ni ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Mbunge wa Kigamboni ndugu yetu Ndugulile alichangia na kuunga mkono hoja Hukua akiwa mawazo amelelalamika sana kuwa wananchi wa Kigamboni wanatezeka sana na vivuko Ni vibovu na tozo za daraja nazo pia ni mzigo pamoja na kwamba tozo hizo zimepunguzwa kdg na kutaka tozo hizo zifutwe na vivuko vibinafzishwe kwa watu binafsi kuongeza ufanisi.

Sasa wakati anahitimisha alisema kama Wizara au Serikali hawatafanyia kazi maombi ya wananchi ya Kigamboni yeye atashika shilingi ya Waziri.

Pia Mbuge wa Sumbawanga Mjini bwana Aishi amesema pia kuwa yeye pia atashika shilingi ya Waziri.

Je, wabunge hawa wanamaanisha nn kusema kuwa watashika shilingi za mawaziri je Ni kuzuia mishahara yao au kutounga hoja mkono.
 
Ameuliza swala ni la Msingi Sana. Badala ya kujibu mnaleta tabia za Facebook hapa! ebo

Kushika shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kanuni ambayo bunge limejiwekea. Itokeapo mbunge hakubaliani na mpango wa waziri hasa anapowasilisha bajeti huweka pinganizi ambapo waziri aidha atoe ufafanuzi utakaomridhisha mshika shilingi ama bajeti hiyo haitapita mpka waziri mpanga bajeti hiyo amridhishe mbunge huyo.

Ni utaratibu tu ambao wewe unaweza ukauona wa ajabu lkn una function kibunge. Na hii ni maslahi mapana ya wananchi wa eneo la mbunge huyo. Si Kwa maslahi zake mwenyewe, kama wanavyo jitwalia ma Hela baada ya kustaafu bila kodi
 
Ameuliza swala ni la Msingi Sana. Badala ya kujibu mnaleta tabia za Facebook hapa! ebo

Kushika shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kanuni ambayo bunge limejiwekea. Itokeapo mbunge hakubaliani na mpango wa waziri hasa anapowasilisha bajeti huweka pinganizi ambapo waziri aidha atoe ufafanuzi utakaomridhisha mshika shilingi ama bajeti hiyo haitapita mpka waziri mpanga bajeti hiyo amridhishe mbunge huyo.

Ni utaratibu tu ambao wewe unaweza ukauona wa ajabu lkn una function kibunge. Na hii ni maslahi mapana ya wananchi wa eneo la mbunge huyo. Si Kwa maslahi zake mwenyewe, kama wanavyo jitwalia ma Hela baada ya kustaafu bila kodi

Kama mbunge akiamua kukaza shingo anaweza kukwamisha bajeti ya waziri husika?
 
Back
Top Bottom