Kuona vitu vilivyopotea na mwizi aliechukua

Hii TV ya asili wangezitangaza tu tukawa tunazinunua pale Mlimani City kwa bei nzuri tu maana importation cost na other charges hakuna.

Wajua haya ma-samsung yao na LG wanatugonga sana bei.
ha ha haa, namna hii lazima usahau machungu ya siasa.
 
Tuliibiwa vitu mbalimbali pale Mlimani City, rafiki wa Mr, akampeleka kwa mganga mwenye Tv asili.
Huko akapakwa dawa usoni ili aweze mwona mwiziwe kwenye tv.
Aliporudi home, alirudi sura imevimba, macho yamekuwa mekundu na akiwa kama kapumbazwa. Hali hiyo alikaa nayo kwa siku tatu.
Nenda!!!!!!!
Ha ha haaaaaa duh, leo ni full kicheko.
 
ni imani tu, mie niliwai kuibiwa, cha kwanza nilienda polisi kutowa ripoti na siku ya pili yake nikaelekezwa kwa mzee mmoja magomeni mapipa, akaniuliza siku ngapi zimepita toka uibiwe, nikamwambia ni jana tu, akasema vitu vyako utavipata, ajanipa dawa wala nini,siku ya iliyofuata polisi wananipigia simu kwamba mwizi ameenda polisi kujisalimisha na vitu vyangu vyote. sasa sijui mkwala wa huyo dingi ama nini,

yapili niliwai kuibiwa spea dukani kwangu, mwizi aliiba turbo, nikasema ngoja niende tena kwa huyo mdingi, kilichofuata siku ya pili tumeikuta turbo imewekwa nje ya duka, mdingi ajanipa dawa yoyote ninywe wala chochote sijui nifanye nini.

Duh, hii kali.
 
kama umewaza kwenda huko umeshapata wazo baya sana na ndio mwanzo wa kuwa mtumwa wa shetani.hata kama vitu vilivyo ibiwa vina thamani kiasi gani kamwe usimwasi MUNGU wako na uende kwa sangoma.kwa taarifa yako hao waliokuibia mpaka leo roho zinawasuta na hawana amani na mbaya zaidi umasikini wao upo palepale.mwachiu MUNGU yeye atakupa nguvu na ujasiri wa kutafuta fedha na punde utapata mara dufu ya ulivyoibiwa.
 
Back
Top Bottom