Kuna wakati watu waliuziwa vitu kabla havijaibiwa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Ulikuwa wizi wa ajabu sana lakini pia uliopitiliza viwango vya uoga na kutoogopa sheria.. Kulikuwa na tatizo kubwa mahali.. Tatizo ka kimfumo na kiutendaji katika kada nzima ya ulinzi na usalama wa raia na mali zako

Kilichotisha zaidi wizi huu ulikuwa wa kuanzia vitu vidogo mpaka vitu vya gharama kubwa.. Na sometimes mnunuzi alijua kabisa hicho kitu ni cha wizi na baadhi ya vikundi vya wizi vilimilikiwa ama kufadhiliwa na haohao wanunuzi

Unakatiza mitaani na raba yako kali.. Mtu anaulizwa unaitaka ile? Ukikubali mnapatana bei kabisa na kutoa advance.. Chini ya lisaa unaletewa mzigo wako na kumalizia pesa

Viatu, saa, nguo simu tv radio nknk viliuzwa kwa mtindo huo.. Kinapataniwa bei kikiwa chini ya umiliki wako.. Na watakichukua tu iwe
Kwa kuibiwa
Kwa kuporwa
Kutapeliwa ama hata kunyang'anywa kwa nguvu

Kuna wengine walifanyiwa hivyo mpaka kwenye vitu vikubwa kama magari, nyumba mashamba na viwanja! Na huna cha kuwafanya hata ukithubutu kwenda mbele ya sheria.. Mfumo uliingiliwa na dosari kubwa
Sasa ni kama haya mambo yanataka kurudi tena! Lakini sasa si kwenye mali bali kwenye uhai..
Yaani unapangiwa kudhulumiwa haki yako ya kuishi hivi hivi mchana kweupe na watu hawajali wala kuogopa!

Nimekuta mahali taarifa ya kifo imetolewa siku moja kabla mhusika umma haujatangaziwa kifo chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Damu ya mtu ni nzito...ipo siku yao.

Damu ya mtu hunuka

Unamau yako kwenye story za kitaa hapa embu fanya kuyapitiaa maana sio poaa..Kifo kinatangazwa mtu akiwa katika ya ibada na Mungu wakee😂😂😂
 
Nimekuta mahali taarifa ya kifo imetolewa siku moja kabla mhusika umma haujatangaziwa kifo chake
emoji3064.png
emoji3064.png
emoji3064.png
emoji1550.png
emoji1544.png
emoji1550.png
emoji1550.png
Hii nchi magumashi yametamalaki
 
Salam za rambirambi zimetayarishwa tarehe 3 ....muhusika karudisha namba tarehe 4
Only in Tz.
 
Back
Top Bottom