Kuona vitu vilivyopotea na mwizi aliechukua

Hawa Waganga! Kuna jamaa yangu aliambiwa apeleke beberu wakati dadake aliyekuwa anasumbuliwa na maradhi ya akili akitibiwa pale. Jamaa alipotoka usiku kwenda kujisaidia akamkuta mganga anauza ile nyama kwa mzani na amezungukwa na wateja waliokuwa wamamsifia kwa kuwauziaga nyama nzuri tofauti na za mabuchani pale kwao!
 
Pole sn ndg,jitahid kuondokana na iman hizo coz ztakugombanisha bure na ndg or jamaa!!
 
magomeni maeneo gani?
ni imani tu, mie niliwai kuibiwa, cha kwanza nilienda polisi kutowa ripoti na siku ya pili yake nikaelekezwa kwa mzee mmoja magomeni mapipa, akaniuliza siku ngapi zimepita toka uibiwe, nikamwambia ni jana tu, akasema vitu vyako utavipata, ajanipa dawa wala nini,siku ya iliyofuata polisi wananipigia simu kwamba mwizi ameenda polisi kujisalimisha na vitu vyangu vyote. sasa sijui mkwala wa huyo dingi ama nini,

yapili niliwai kuibiwa spea dukani kwangu, mwizi aliiba turbo, nikasema ngoja niende tena kwa huyo mdingi, kilichofuata siku ya pili tumeikuta turbo imewekwa nje ya duka, mdingi ajanipa dawa yoyote ninywe wala chochote sijui nifanye nini.
 
kama unakata hile barabara ya kondoa ukitokea wilayani, nyumba ya mwanzo kulia kona, ina duka la mafriji, anaitwa bwaoja, wengine wanaoamini wanasema ata kama ndugu yako chizi hapo mwisho, kama nilivyosema ni imani isije ikawa haikuwa ukaniambia nimekuingiza siko

magomeni maeneo gani?
 
He he he eheeee, pole sana, bila huruma mkaibiwa tena! ama kweli safari moja huanzisha nyingine.
Kwa kweli sikupi pole, hata nikisema uliibiwa mara ya pili nitakose, hii uliamua kuchangia unga wa mganga...
Tena mwizi wa pili wanmuona na hawamfanyi chochote!
 
Ndugu polesana,kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mkristo hivyo napenda kukushauri kuwa achana na huo mpango wa kwenda kwa waovu kufanya yaliyo machukizo mbele ya MUNGU wetu.unazo option nyingine ikiwemo ya kusamehe maana itakuondolea uwezekano wa kumtenda MUNGU dhambi.
Nasema hivyo maana hadi sasa inaonesha bado uko na uchungu mwingi kiasi kwamba unaona ni sawa tu kwenda kwa wapiga bao.ukisoma kwenye biblia kumbukumbu la torati MUNGU alikataa vikali kwenda kwa hao jamaa na kuwa yeyote afanyae hayo hufanya machukizo kwa MUNGU.

Wewe samehe muombe Mungu akupe amani,ukishikilia uchungu na visasi bro huo ni mtaji wa shetani atatumia hivyo ili uendelee kumkosa MUNGU wakati wewe unaona unasolve.

Pia kama wewe ni mkristo hebu fanya bidii ujifunze principal za mafanikio kikristo maana usipozijua basi hata mali zako zinakosa devine protection na kuwa exposed kwa shetani so any time akitaka kukuharibia atafanya tu na kufanikiwa
Jamani mimi ni muhanga wa kuibiwa kwa kweli ni karibu mwaka sasa umepita kuna mwizi alivunja gari na kuondoka na vitu muhimu sana sasa kila mahali na kila ninayemuhadithia anasema ni kwamba ni mchoro uliochorwa na mtu aliye karibu na mimi sasa bila kuzunguka maneno nasiikia kuna waganga wana tv ya asili ambayo inaonyesha tukio zima lilivyofanyika naomba mtu anejua sehemu nzuri ya kupata huduma hii na yenye uhakika anijuze na pia kama kuna madhara ya kuangalia iyo tv niambie najua humu kuna watu washa experience kuibiwa vitu muhimu
 
Ngoja niconfess. Nikiwa form one boarding skuli, nikaumwa bwana. Akaja couain wake mshua kunichukua anipeleke hospitali. Nikaandikiwa sindano za masaa ikabidi nilale town wiki. Kumbe hapo alipopanga kuna mganga wa kienyeji. Dah, tulikuwa tunakula kuku za chienyeji balaa. Manake mganga nahisi alikuwa hana friji. So tunashinda na hgelo, ukiskia hodi ujue vyuku. Mgonjwa nilikulaje michemsho? Yaani ulozi ni wizi mtupu!
King'asti wee! hapo chacha
 
Last edited by a moderator:
kama unakata hile barabara ya kondoa ukitokea wilayani, nyumba ya mwanzo kulia kona, ina duka la mafriji, anaitwa bwaoja, wengine wanaoamini wanasema ata kama ndugu yako chizi hapo mwisho, kama nilivyosema ni imani isije ikawa haikuwa ukaniambia nimekuingiza siko

Mmm sio kama unamuelekeza aje kwako?
 
Forget about hiyo tv asilia.cha muhimu we move on na maisha vitu utatafuta tu vingine mkuu!
 
Jamani mimi ni muhanga wa kuibiwa kwa kweli ni karibu mwaka sasa umepita kuna mwizi alivunja gari na kuondoka na vitu muhimu sana sasa kila mahali na kila ninayemuhadithia anasema ni kwamba ni mchoro uliochorwa na mtu aliye karibu na mimi sasa bila kuzunguka maneno nasiikia kuna waganga wana tv ya asili ambayo inaonyesha tukio zima lilivyofanyika naomba mtu anejua sehemu nzuri ya kupata huduma hii na yenye uhakika anijuze na pia kama kuna madhara ya kuangalia iyo tv niambie najua humu kuna watu washa experience kuibiwa vitu muhimu
Mkuu seki6 Waganga ambao wanao uwezo wa kukufanyia dawa ukamuona huyo mwizi wako. Mimi ninauliza swali unijibu wewe Je ukionyeshwa huyo Mwizi aliyekuibia je utaweza kuvumilia?au ndio tena vurugu mechi kupigana mapanga na kuuwana sababu ni ya kuonyeshwa kwa huyo mwizi wako? ukiweza Sema................

MziziMkavu njoo utoe ufafanuzi ulioshiba kwenye hili jambo plz!
Mkuu Billie Elimu ya kumuona Mwizi aliyekuibia au Mwizi kumvimbisha tumbo mpaka arudishe kitu alichokuibia ipo ila huyu mkuu seki6 amechelewa sana amekaa mwaka mzima kisha ndio analeta hapa malalmiko yake?Elimu ya kuwaona Wachawi Mtu aliye kuroga pia ipo hiyo ni TV asilia.
 
Yaha mambo yana kwenda na imani kama una imanisana ya kishirikina unaweza kuona lakini kama huna imani hizo utapoteza muda wako.
Niliwahi ibiwa tena tulikwenda mbagala tukanywa hiyo dawa tulikuwa wawili hatukuona kitu ila nilsha sikia watu wana sema walisha ona .
Ushauri achana na dawa hizo siyo nzuli kwani kichwa kiliniuma sana nikatapika ,na nafikili zile dawa huwa siyo safi unajua mambo ya kichawi ni tofauti na mambo ya kibina damu na mungu vile ninavyo onekana vichafu ktk hali ya kawaida kwenye uchawi ndiyo vina fanya kazi na kinacho kuwa hakitakiwi kabisa ktk hali ya kawaida basi kule kwao ndiyo lulu.
In short,chochote ambacho kwa mungu hakitakiwi basi kwa shetani ni ibada
 
ni imani tu, mie niliwai kuibiwa, cha kwanza nilienda polisi kutowa ripoti na siku ya pili yake nikaelekezwa kwa mzee mmoja magomeni mapipa, akaniuliza siku ngapi zimepita toka uibiwe, nikamwambia ni jana tu, akasema vitu vyako utavipata, ajanipa dawa wala nini,siku ya iliyofuata polisi wananipigia simu kwamba mwizi ameenda polisi kujisalimisha na vitu vyangu vyote. sasa sijui mkwala wa huyo dingi ama nini,

yapili niliwai kuibiwa spea dukani kwangu, mwizi aliiba turbo, nikasema ngoja niende tena kwa huyo mdingi, kilichofuata siku ya pili tumeikuta turbo imewekwa nje ya duka, mdingi ajanipa dawa yoyote ninywe wala chochote sijui nifanye nini.

Nielekeze niende kwani kwangu wamefanya shamba la bibi
 
mkuu seki6 waganga ambao wanao uwezo wa kukufanyia dawa ukamuona huyo mwizi wako. Mimi ninauliza swali unijibu wewe je ukionyeshwa huyo mwizi aliyekuibia je utaweza kuvumilia?au ndio tena vurugu mechi kupigana mapanga na kuuwana sababu ni ya kuonyeshwa kwa huyo mwizi wako? Ukiweza sema................

Mkuu billie elimu ya kumuona mwizi aliyekuibia au mwizi kumvimbisha tumbo mpaka arudishe kitu alichokuibia ipo ila huyu mkuu seki6 amechelewa sana amekaa mwaka mzima kisha ndio analeta hapa malalmiko yake?elimu ya kuwaona wachawi mtu aliye kuroga pia ipo hiyo ni tv asilia.

kurusha ngumi apana sitarusha ninachotaka ni kujua mtu exactly ndocho ninachokihitaji maana watu wengi wananiambia aliyekufanyia mchezo huu ni rafikiyako wa karibu sasa nina marafiki kibao naweza nikawa namuhisi mtu ambaye si yeye nikaona ni bora nikapata iyo elimu ya utambuzi lakini bila kuhusisha mwili wangu kutumika kwa kunywa dawa au vinginevyo ninachofahamu mimi kuna watu wanao uo uwezo wakukuonyesha kwenye kiyooo au beseni la maji .swala la kukaa mwaka sikua nakaa bure nilikua nahangaika lakini sijapata hiyo technology nayohitaji mimi wengi wanasema tu kwa ishara mfano aliyekuibia mfupi ,mwemba ect sasa ukiangalia kwa uhasilia wembamba wako wengi au kama ni mweusi wako wengi pia.
sasa kama unajua jambo hili linawezekana ni bora bila kupoteza muda nielekeze nianze kufuatilia
 
Back
Top Bottom